Usafiri wa ndege TZ: Wahabeshi/Ethiopian Airlines wamewezaje, tukashindwa sisi?


Wako wapi hao wezi na walifanywa nini??!!!

Usisahau na unafiki pia unatugharimu sana. Yaani sana tu sababu hatuambiani ukweli ila kutafuta wa kumuangushia jumba bovu!!!

Tabia ya hovyo sana sana kuendekeza njaa ya leo bila kujali shamba lililotoa unachokula leo!!!!
 

Hebu tuache chuki za kikabila, kwa hiyo hao uliowataja ndio serikali? Serikali ya ccm inahusika sana kuuwa mashirika ya umma huo ndio ukweli, hutaki unaacha.
 
Hii tuna system ambayo unachukua miaka 3 hadi 4 kupata kibali cha kiwanja sasa tutaweza vipi biashara ya ndege!!!
 
Wahabeshi wanafanya hiyo biashara toka sisi bado tunatawaliwa na mkoloni.hawajakurupuka
 

Hii ni comment ya kijinga kuliko.Pilot kuomba hifadhi ni jambo la binafsi. Nchi aliyeomba hifadhi ni Switzerland sio Sweden. Ma pilots wa E.Airlines wapo wa mataifa mbalimbali nao wanatishiwa kuuliwa? Wenzetu wananunua Ndege mpya kila mwaka wewe umekalia majungu na hearsay. Ethiopian Airlines inaendeshwa kitaalamu na wameajiri wataalamu mbalimbali kutoka pembe za dunia.Ndio maana wamepata tuzo mbalimbali na kushindana na mashirika yenye majina.Tuige mazuri yao kwani ni mfano kwa Airlines za kutoka Bara la Afrika.
 

Upo sawa mkuu!.....swadaktaa!
 
Mkiwa mnacoment mufanye na comparison kati ya maisha ya waethiopia na watanzania pia. jana katika pitapita zangu kwenye vile vikao vya viti vilefu aka bar nilileta hii mada tukiwa na wafanya biashara wakubwa tu wa kariakoo. walichoniambia ni kuwa serikali ya ethiopia ina pesa ila raia wake wana umaskini wa hali ya juu tena wakaongeza ndio maana unaona wahamiaji haramu asilimia kubwa wanatoka huko kwenda kutafuta maisha nchi zingine. ni kwamba serikali ya ethiopia haitaki watu wamiliki pesa za kutosha na ndio maana lile shirika hamna raia mwenye share. nikapewa mfano kwa hapa tz kipindi cha mwinyi nasikia serikali iliwahi kuyumba kwa kukosa pesa kwa kuwa raia walimiliki mkwanja wa hatari. ila pamoja na hayo hata uongozi wetu mbovu unachangia maana tusingeshindwa kuwa hata na ndege tano zenye kueleweka na za uhakika angalau kwenda miji ile ya kibiashara hii ni aibu kwa nchi km hii yenye vivutio vya utalii. lazima apatikane kiongozi ambaye ataangalia maslahi ya taifa cyo kushibisha ndugu zake tuu.
 
Bro Lemutuz
Heshima kwako.
Naomba nichangie mada kwa kurekebisha kuwa Wahabeshi si wa Israeli au wayahudi. Wahabeshi waliokuwa na vinasaba [DNA] vya kiyahudi wote walichukuliwa na Wayahudi wenzao mwaka 2007 - 2009. Israeli haija wekeza kwenye shirika hilo. 'Ethiopian Airline' inamilikiwa 100% na serikali ya Ethiopia.....hakuna mbia wa nje!

Pamoja na matatizo ya hapa na pale shirika hilo linapiga hatua sana.....hii inatokana na kwanza kuweka UZALENDO mbele (hata kama ni wa kulazimishwa mwisho hukubalika), kutowalea mafisadi, wahujumu, wazembe nk nk. Suala la kiongozi wa shirika kuwekwa ndani ili tu apate "mafunzo" na baada ya hapo kurejeshwa kazini ni la kawaida.

Mishahara ya pilots and flight Engineers ni ya kawaida tu lakini kwa sababu ya kusomeshwa na serikali unatakiwa kulipia "mikopo" ya shule kwa kufanya kazi kwa miaka kadhaa ndani ya shirika hilo. Kutokana na sheria kali, uangalizi wa karibu wa taasisi husika hakuna hujuma, wizi, ufisadi nk vinavyotokea.

Vile vile, mikataba ya ununuzi wa ndege mpya huangaliwa na wadau wengi wa serikali kwa lengo la kuzuia ufisadi....pia uzalendo upo na si kupiga dili tu kenye kila kitu.

Waethiopia wamepiga hatua katika nyanja ya miundo mbinu na usafirishaji kwa sababu hawacheki na kenge yoyote hasa kwenye mikataba. Ethiopian ina ndege Zaidi ya 60! shirika la meli (hawana bandari) lakini wanamiliki meli 15 (sisi hatuna hata boti!!)

Juzi amezindua majaribio ya city train!! iliyojengwa ndani ya miaka 2!.....kwetu?

Na wanajenga bwawa la kuzalisha umeme litakapo malizika litazalisha megawati 6000!


KITU MUHIMU: Uzalengo wa dhati kwa kila mwananchi na kuwa na vipaumbele vichache vinavyotekelezeka.

Amen
 

Hee....Ukiwa na nguvu ya kusema wezi sio ccm naanza kukutilia mashaka.
 
Hee....Ukiwa na nguvu ya kusema wezi sio ccm naanza kukutilia mashaka.

Nisome tena kwa utuvu:

By FaizaFoxy

Usiseme wezi ni CCM pekee, sikatai wapo lakini tuuseme ukweli, Watanzania wengi sana wezi na wengi wapo kwenye vyama na wasiokuwepo kwenye vyama. Kuna walioiibia Serikali na kuuwa mashirika ya umma Tanzania hii zaidi ya Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa? Tuseme kweli.
 
Mleta mada unautani sana ivi untaka tuwe na shirika la ndege kama ithopia wakati hatujajua hata sehemu za kukojolea tunakojoa barabarani ovyo..

mbona addis wenyeji walikuwa "wakishusha mizigo" barabarani na bado wakawa na shirika la ndege imara?
 

kwa nyongeza tu, hata haile mariam alipochukuwa nchi hakuligusa kabisa shirika la ndege aliliacha lijiendeshe kibiashara zaidi.
wakati wa vita ndege za shirika zilikuwa hazilali addis ziliwekewa ratiba ya kufika addis asubuhi na kuondoka siku hiyo hiyo
ili kuziepusha na madhara ya vita.
 
Mkuu Tanzania ni nchi ya aina yake. Watu wengi waliopo madarakani ni wachumia tumbo....Kuanzia Rais hadi mtendaji wa mtaa/kijiji. Hakuna mzalendo...kila mmoja anatafuta kushiba, hivyo sio rahisi kama unavyofikiria ili kendesha shirika la ndege. Inasikitisha sana kuona Waziri mwenye dhamana anakubali kununua ndege mbovu ili mradi tu aweke 10 percent yake mfukoni..! It is a big shame...na sijui lini tutajitambua
 

Nadhani hii ni ndoto fulani hivi! Wenzio ndio kwanza wamebook toka Boeing ndege nyingine 10 ambazo zitawezesha ET kufikisha zaidi ya ndege 100, we unasema "itajifia" ni kama yule fisi aliyekuwa akivizia mkono wa mtu ukatike autafune!! Fika Bole International Airport uone kazi!!!
 
wewe bwana mdogo funguka!!!!.Ile inchi ni ya wayahudi.inaendeshwa na wayahudi,wamewekeza wayahudi.jiulize wana nini zaidi ya mifugo?wale ni African jewish na wana uhusiano mkubwa sana.
 
Kaka
Kwakuwa siwezi kukubadili msimamo wako...... sitajaribu. Nimefanya research kwenye ninachokueleza. Habeshas ni watu wa kujivuna sana, kujitambua na kujipenda.....pamoja na kuwa AUC ipo pale..... hawajiiti waafrika wanajiita Ethiopians/Habeshas kwanza ndo Uafrika unafata.

Usibishe tu nachokwambia ndo sahihi.....Israel haina ushawishi wowote katika maisha ya Wahabeshi wala katika utawala wao na hata katika Imani yao!!

Ukiweza kuniambia ni kwanini unaamini kuwa Israel ina ushawish kwa Wahabesh kwa mtazamo wako nitaweza kukusaidia kukuelimisha.

Bro....Usichukulie hii ni challenge bali kukuelimisha kistaarabu tu.

Kwa taarifa yako.....Wataliano ambao waliishi Ethiopia kwa miaka mitano wana influence kubwa kuliko wa Israeli......tafiti
 

Mkuu unaongea kitu gani ? yaani mtu mmoja akizamia inamaana lawama ni kwa wote; kama ni hivyo tuambie na wewe umeshaua maalbino wangapi maana Tanzania inajulikana kwa huo udhalimu na mmpaka sasa hajahukumiwa mtu
 
Ethiopia pamoja na UMASKINI na UKAME/NJAA na kuwa LANDLOCKED baada ya miaka kadhaa watatuacha mbali sana. Tena huyu Waziri Mkuu wa Sasa ni MLOKOLE haswaa asiyetaka kusikia habari ya UFISADI hata chembe ukibainika unaozea jela. Ethiopian Airlines ndo biashara inayowaletea kipato kikubwa mno(NI YA 3 KWA UBORA. Waliona mbali, wakawekeza na sasa wanakula matunda. sisi tumekalia kelele
 
Tuvute subira jitihada zinafanyika mtashuhudia maajabu hivi karibu ATC itarudi hewani kama EMIRATES
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…