Usafiri wa ndege TZ: Wahabeshi/Ethiopian Airlines wamewezaje, tukashindwa sisi?

Usafiri wa ndege TZ: Wahabeshi/Ethiopian Airlines wamewezaje, tukashindwa sisi?

Tutapaa mpaka Dubei kupitia BUKOBA. Iwee
 
Wana miaka 70 sasa katika biashara hii na wanaongoza Africa kwa kuwa na destinations nyingi.

Hakuna cha mzungu wala nini asilimia mia ni ya serikali. Board chairman, CEO, CFO, CCO, wote ni wazalendo, hatujarogwa na MTU ila tabia ndio tofauti
 
Inasikitisha na kuhuzunisha. Rwanda wanapeleka vijana kujifunza Ethiopian airlines sisi tunapeleka vijana Jei Kei Tii kulima mchicha
 
tubadilishe jina la kampuni itakayoendesha hizo ndege mpya kuwa Kilimanjaro Airlines maana nina wasiwasi huenda ATC zinadaiwa huko nje so tukitumia jina hilo hilo huenda zikazuiwa huko nje
 
tubadilishe jina la kampuni itakayoendesha hizo ndege mpya kuwa Kilimanjaro Airlines maana nina wasiwasi huenda ATC zinadaiwa huko nje so tukitumia jina hilo hilo huenda zikazuiwa huko nje

Naunga mkono hoja.

Hii itasaidia pia kuutangaza mlima wetu ambao wazungu wanajua uko Kenya.
 
Dawa ni kuajiri waumini wafia dini
 
Merit merit merit! Tatizo Tanzania kadi ya CCM ndio necessary and sufficient qualification. Je tutafika?
 
Tuajiri wachina hapo ATCL enzi za awamu ya 4 tuliambiwa kuna mwarabu toka OMAN atakuja kuwekeza kulikon?
 
Naiona ATC ikitua Paris kisha unaunga Stockholm
Itachukua mda kufikia huko lazima uwe na ndege yakuruka na kwenda masafa marefu mfano Airbus A330-Airbus,Airbus A340,Airbus A350,A380 au Boeing 747-400,Boeing 748-8i,Boeing 777-200,777-300,Boeing 787-9 kama taifa tukiwa na hizi tutafika huko.Na hizi zote kununua ni gharama kubwa sana na mipango madhubuti
 
jamani mimi huwa nakiuliza hivi iweje Tanzania kweli tunakosa shirika la ndege lenye ndege za kuruka sehemu ambazo kimsingi ni potential kwa biashara kama DUBAI, JOHANNESBURG, LAGOS/ACCRA ENTEBBE, LUSAKA hata LONDON etc?

mbona hawa wahabeshi/ET wameweza pamoja na kuwa sisi tuna kila kitu? tumilogwa? ukipita ADDIS ABABA ukiona jinsi hawa wahabeshi walivyo na ndege nyingi zinazoruka duniani kote ndo utashangaa!!


TANGANYIKA HAIWEZI KWENDA MPAKA ITAKAPOACHANA NA ZANZIBAR : KUIKUMBATIA ZANZIBAR NI LAANA ; MTALALAMIKA SIKU ZOTE
 
Usiseme wezi ni CCM pekee, sikatai wapo lakini tuuseme ukweli, Watanzania wengi sana wezi na wengi wapo kwenye vyama na wasiokuwepo kwenye vyama. Kuna walioiibia Serikali na kuuwa mashirika ya umma Tanzania hii zaidi ya Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa? Tuseme kweli.
Uwezi conclude wachaga,wahaya na wanyakusya ndio walioiba serikalini na kuuwa mashirika ya umma,napingana na we we kwa sababu kuna wachaga,wahaya na wanyakuswa wazuri sana walio litumikia hili taifa,ungekuwa vizuri kama ungetaja majina ya hao walioiba na kuuwa hayo mashirika kwani kipindi hicho hakukuwa na serikali?.Hakuna kitu kibaya kama kupandikiza mbegu ya ukabila nakubagua baadhi ya makabila kwa kosa alilofanya mtu mmoja mnachafua kabila zima.Au maendeleo mnayo yaona kwenye hayo maeneo mnajua wameiba,nijufikirishe wakati wao wakilima na kufanya biashara hili wapate kubadilisha mfumo wao wa maisha na kuwekeza kwenye elimu ya vizazi vyao upande mwingine wao wanacheza ngoma au awajishughulishi wanawaza leo na kutafuta shibe ya leo awafikirii kesho itakuwaje wao na watoto wao.Nafikiri sio vizuri kusema kabila sema Fulani ndio alifanya hivi.
 
sisi tunahitaji mtaalam wa biashara za masuala ya usafirishaji wa anga/aviation/commercial flights, nafasi itangazwe kimataifa, afanyiwe interview na panel ya wataalamu (si wanasiasa) wa ndani na nje atakayeshinda kwa haki apewe kazi na Vigezo vya muda maalum kuongoza ATCL kwa ufanisi.
 
Kama blessings ulivosema naunga mkono hoja ingependeza tupate mtu mwenye uzoefu wa Biashara za ndege za kimataifa pale ATCL ama kwenye bodi ama kwenye menejimenti. Kwa kuanzia hata tumuibe Ethiopian ama ndege za uarabuni hukooo
 
sisi tunahitaji mtaalam wa biashara za masuala ya usafirishaji wa anga/aviation/commercial flights, nafasi itangazwe kimataifa, afanyiwe interview na panel ya wataalamu (si wanasiasa) wa ndani na nje atakayeshinda kwa haki apewe kazi na Vigezo vya muda maalum kuongoza ATCL kwa ufanisi.
tuwaepuke PhD holders na makada katika shirika la ndege hili
 
inawezekana kila mtu akitimiza wajibu wake. Emirates miaka ya katikati ya 1980 waliazimwa ndege katika kuanza shirika lao. Leo hii wapo mbali sana.
 
Back
Top Bottom