Bro Lemutuz
Heshima kwako.
Naomba nichangie mada kwa kurekebisha kuwa Wahabeshi si wa Israeli au wayahudi. Wahabeshi waliokuwa na vinasaba [DNA] vya kiyahudi wote walichukuliwa na Wayahudi wenzao mwaka 2007 - 2009. Israeli haija wekeza kwenye shirika hilo. 'Ethiopian Airline' inamilikiwa 100% na serikali ya Ethiopia.....hakuna mbia wa nje!
Pamoja na matatizo ya hapa na pale shirika hilo linapiga hatua sana.....hii inatokana na kwanza kuweka UZALENDO mbele (hata kama ni wa kulazimishwa mwisho hukubalika), kutowalea mafisadi, wahujumu, wazembe nk nk. Suala la kiongozi wa shirika kuwekwa ndani ili tu apate "mafunzo" na baada ya hapo kurejeshwa kazini ni la kawaida.
Mishahara ya pilots and flight Engineers ni ya kawaida tu lakini kwa sababu ya kusomeshwa na serikali unatakiwa kulipia "mikopo" ya shule kwa kufanya kazi kwa miaka kadhaa ndani ya shirika hilo. Kutokana na sheria kali, uangalizi wa karibu wa taasisi husika hakuna hujuma, wizi, ufisadi nk vinavyotokea.
Vile vile, mikataba ya ununuzi wa ndege mpya huangaliwa na wadau wengi wa serikali kwa lengo la kuzuia ufisadi....pia uzalendo upo na si kupiga dili tu kenye kila kitu.
Waethiopia wamepiga hatua katika nyanja ya miundo mbinu na usafirishaji kwa sababu hawacheki na kenge yoyote hasa kwenye mikataba. Ethiopian ina ndege Zaidi ya 60! shirika la meli (hawana bandari) lakini wanamiliki meli 15 (sisi hatuna hata boti!!)
Juzi amezindua majaribio ya city train!! iliyojengwa ndani ya miaka 2!.....kwetu?
Na wanajenga bwawa la kuzalisha umeme litakapo malizika litazalisha megawati 6000!
KITU MUHIMU: Uzalengo wa dhati kwa kila mwananchi na kuwa na vipaumbele vichache vinavyotekelezeka.
Amen