USAID yatangaza kusitisha misaada nje ya nchi

Hivi tunahitaji misaada kweli? Au ni akili zetu finyu tuu
Tuna bandari tegemezi kwa nchi nane
Tuna madini nchi nzima
Tuna vivutio vya utalii kila kona ya nchi
Tuna bahari
Tuna bandari za kutosha
Tuna ardhi ya kutosha
Tuna moto na maZiwa mengi tuu
Tuna gesi asilia
Tuna mafuta nknk
Tulichokosa/tulichonyimwa ni akili
Yaani nimesoma huu uzi nilikuwa sielewi kwa nini watanzania tumejawa na uoga na malalamiko,yaani wadau wanavyolaumu utasema ni haki yao,hivi inakuwaje?kweli tumepewa vyote tumenyimwa akili.
 
Tufe tu
Watakaobaki watakuwa makini zaidi
Kazi ya Serikali ni pamoja na kulinda Usalama wa raia wao, kwahiyo lazima itapambana kuhakikisha wanaendelea kuwapatia hayo madawa hata kama yatakuwa ni ya akina Madabila wa CCM
 
Yaani nimesoma huu uzi nilikuwa sielewi kwa nini watanzania tumejawa na uoga na malalamiko,yaani wadau wanavyolaumu utasema ni haki yao,hivi inakuwaje?kweli tumepewa vyote tumenyimwa akili.
Ni hatari sana sema basi tu,kama tulilogwa basi aliyetuloga alitumia uchawi mkali sana sana Mungu atusaidie tu.
 
Msiba wa jirani ni wangu pia hatuwezi kujua itakuwaje, wengi tunawategemea sana wao wakisema suu Hali kwetu ni mbaya sana
 
As a Lissu backer, I agree. Lakini nina wasiwasi na Batanzani wenziwangu just because wengi banasema Lissu has Dictatorial tendencies just as was Magufuli.

But As a Tanzanian First, we made a big mistake to challenge the late Magufulis Policies on Natural Resources. And this is not only coming from me, hata MAGA niliokutana nao D.C washington walikuwa wakitushangaa.
Nilimdharau Lissu alipoanza kwenda kinyume katika harakati za rasimali enzi za magufuli nilimuona ni kama Chawa wa wazungu .. Nchi inapigana imiliki Rasimali kama anavyofanya Trump .. American First yeye anakuwa mpingaji ..
 
Kuna haja turudie zile Siasa enzi za Mwalimu

"Ujamaa na kujitegemea"

Vinginevyo tutakopa ili kufidia bajeti za Serikali hadi Nchi ipigwe mnada 🙌
Screenshot_2025-01-17-15-16-56-603_com.mi.globalbrowser-edit.jpg
 
Nilimdharau Lissu alipoanza kwenda kinyume katika harakati za rasimali enzi za magufuli nilimuona ni kama Chawa wa wazungu .. Nchi inapigana imiliki Rasimali kama anavyofanya Trump .. American First yeye anakuwa mpingaji ..
Walikuwa wanataka waungwe mkono, na waliungwa mkono kweli kweli. Ndio maana walishindwa mwanzoni mwa awamu hii kumsema Rais na Serikali ya CCM.

Mbowe alitupoteza mno.
 
Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) limetangaza kusitisha utoaji wa fedha mpya na usambazaji wa fedha chini ya makubaliano ya malengo ya maendeleo (DOAGs) hadi uhakiki wa programu za msaada wa nje zinazofadhiliwa na USAID utakapokamilika.

Wakati mchakato wa kuhakikisha msaada wote wa nje unalingana na ajenda ya sera ya nje ya Rais Donald Trump ukitarajiwa kutolewa ndani ya siku 30, uhakiki huu unatarajiwa kukamilika ndani ya siku 85 kuanzia Januari 24, 2025.

Kutokana na hilo, USAID imewaagiza maofisa wote kusimamisha kazi, mishahara, na safari kwa asasi na taasisi zote zilizopokea misaada kupitia shirika hilo.

Hayo yamebainishwa kupitia barua rasmi kwa maofisa wa mikataba na makubaliano ya USAID na washirika wake, iliyotolewa na shirika hilo Januari 24, 2025.

Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manunuzi wa USAID, Jami J. Rodgers, imeeleza uamuzi huo unatokana na utekelezaji wa agizo la Rais Trump la kurejelea na kurekebisha misaada ya nje ya Marekani.

Soma kwa undani katika tovuti ya Mwananchi.

View attachment 3215692
Wako sawa 100% kusitisha,kwani wengine wamelala kusubiri misaara,wengine wanafia kazini wakifanya kazi
 
Attachments

  • VID-20250128-WA0033.mp4
    3.9 MB

Back
Top Bottom