USAID yatangaza kusitisha misaada nje ya nchi

USAID yatangaza kusitisha misaada nje ya nchi

Net was business from someone,dawa ilikua kuua vyanzo vya mazalia ya mbu na wadudu wanaotambaa,mengine yote ni upigaji tu
Hiyo ya Net niliipata kutoka Kwa mtu wa Jikoni kabisa

Shida ya Viongozi wetu hawapo kwaajili ya kusaidia raia wao bali maslahi yao binafsi
 
USAID ilishakuwa ya kihuni watu wanatoa project grants kwa kujuana sio kuzingatia vigezo.
 
Kina haja ya kuachana na biashara ya kula vya nje, hatari inayokuja ni kubwa.
Ni kweli

Kuna vyakula vingi fake vinaliwa hapa DSM

Binafsi nimeamua kuagiza Mchele wa kula kutoka Mbeya na Morogoro baada ya Mwezi Uliopita wife kununua Mchele ambao baada ya kuupakua na kubaki ukoko, ukiumwagia Maji huo ukoko unajaza sefulia Kwa wingi

Nimeona hapa tutaanza kulishwa Mchele wa plastiki kisha nguvu za kiume zituishie tusingizie Uzee 🙌
 
Ujamaa na Kujitegemea ulikuwa unaishi kwenye nyimbo majeshini na kwenye shule za msingi tu zikiwaandaa vijana waje kuwa masikini jeuri.

Kiuhalisia USAID na SIDA wapo tangu 1961.
Hoja yangu tuanze kujenga mentality ya Kujitegemea

Haiwezekani una rasilimali lukuki lakini Ujenzi wa matundu ya choo tu tunaomba msaada Kwa Wahisani
 
Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) limetangaza kusitisha utoaji wa fedha mpya na usambazaji wa fedha chini ya makubaliano ya malengo ya maendeleo (DOAGs) hadi uhakiki wa programu za msaada wa nje zinazofadhiliwa na USAID utakapokamilika.

Wakati mchakato wa kuhakikisha msaada wote wa nje unalingana na ajenda ya sera ya nje ya Rais Donald Trump ukitarajiwa kutolewa ndani ya siku 30, uhakiki huu unatarajiwa kukamilika ndani ya siku 85 kuanzia Januari 24, 2025.

Kutokana na hilo, USAID imewaagiza maofisa wote kusimamisha kazi, mishahara, na safari kwa asasi na taasisi zote zilizopokea misaada kupitia shirika hilo.

Hayo yamebainishwa kupitia barua rasmi kwa maofisa wa mikataba na makubaliano ya USAID na washirika wake, iliyotolewa na shirika hilo Januari 24, 2025.

Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manunuzi wa USAID, Jami J. Rodgers, imeeleza uamuzi huo unatokana na utekelezaji wa agizo la Rais Trump la kurejelea na kurekebisha misaada ya nje ya Marekani.

Soma kwa undani katika tovuti ya Mwananchi.

View attachment 3215692
Oyi Oyiiiiiii Massive Unemployment once again..... Dah
 
Safi sana,wakati tunampigia debe Kamala,mkasema mwanamke hafai kuongoza kabisa,sasa jiandaeni kuanguka kwa H..IV na kufa kama kuku wa kideri
Sasa Mimi umenijumuisha hapo nina kosa gani 😂😭
 
D.Trump wants to help Amerika, cha ajabu tanzagiza ambapo >50% ya fedha ni msaada ndiyo inaongoza kwa kuchezea fedha, raisi ikulu 3, magari kila siku land cruiser mpya, USA inabana matumizi kusaidia wananchi, tanzagiza shopping kwa kwenda mbele …
Kwa uzi unaweza kumwelewa Trump kwanini kachukua maamuzi haya
 
Hakutakuwa na ArVs za bure tena huko mbele ya safari

Kuna hatari maambukizi mapya ya HIV kushamiri miongoni mwa Watanzania

Hii itapelekea Serikali kutumia gharama kubwa kuyanunua hayo madawa, otherwise tutarajie ule Ukimwi aliouimba Ferouz kwenye nyimbo ya "Starehe" kurudi tena Mtaani
Tupunguze bajeti ya ma VX new model tunajiweza mbona?
 
Back
Top Bottom