Usajili wa chama cha siasa cha National Economical Reformation Socialist Party -NERP

Usajili wa chama cha siasa cha National Economical Reformation Socialist Party -NERP

Kama kichwa cha habari hapo juu, tuko mbioni kusajili chama cha siasa kitakachosimia rasilimali za taifa kuwanufaisha wananchi wote wa Taifa hili.
Chama kiwe HALFCAST, mixture ya UJAMAA na UBEPARI, ktk Katiba yake, kichukue strengthes za CCM na CDM.

Kiachane na Weaknesses za vyama hivyo, kireflect maoni ya wananchi ktk KATIBA mpya. Amen
 
Japan haina Resources zozote zaidi ya kuwa na teknolojia na inaendelea.Resouces zote wanaagiza nje.Ulichoandika porojo tupu.Ulaya na Marekani wameendelea sio sababu wana resources bali wana teknolojia. Resources zote zinatoka Afrika nk

Huwezi kuendelea bila kuwa na teknolojia yako ya hali ya juu.Kongo Madini yamejaa kibao lakini ni kama takataka tu sababu teknolojia hawana anatakiwa yaende ulaya ,marekani na Japan na Asia kwa wenye teknolojia za kujua wayafanyaje ili yawe nini

Tanzania pia kelele tu za ohh tuna resources za kutosha so what teknolojia hatuna
Kufaidi resources cha kwanza uwe na teknolojia
Mfano una chuma kinatumika kutengeneza sehemu mojawapo ya injini za magari lile block la injini teknolojia unayo ya kutengeneza hizo block za injini? Lakini injini kukamilika haihitaji hilo block peke yake ndani kuna vikorokoro vingi ambavyo huagizwa nchi zingine ili injini ikamilike Teknolojia unayo ya kuunda injini uuze injini za magari na ndege?

Bila teknolojia resources hazikufikishi mbali.Nchi zote zilizoendelea walijipanga uwezo wa teknolojia kwanza
Hakika, bila teknolojia resources hakufikishi popote, mashine za kuchimbia madini hatuna,
Hata majembe na mapanga tunaagiza china,
 
Vyama vya ubwabwa vitazaliwa vingi sana kipindi hiki. Shida ni moja tu, hamuaminiki na pia mjiandae chama kuwafia kabla ya uchaguzi ujao. Muulize Zitto and company waliyopitia pamoja na kupata support kutoka kulee
 
Ni kama vile unavyosikia Massachusetts Institute of Technology(MIT) ila wanafundisha Uchumi pia au unavyosikia SUA ila wanafundisha Rural development ambayo ni siasa kwa wingi. Jina la chama lisikupoteze.

Tanzania tuna Chama cha Mapinduzi ila hakijwahi kufanya mapinduzi yoyote na Katiba yetu ya mwaka 1977 inasema sisi ni taifa la kijamaa ila ujamaa ulikufa tangu mwaka 1985
Ni chama kipi kinachotawala China?

Na hivi kweli unaelewa maana ya 'Ujamaa'?
 
China pia hakuna demokrasia ya vyama vingi kiko chama kimoja tu cha siasa lakini huwezi sikia mzungu akiongelea China kuwa iruhusu demokrasia ya vyama vingi

Wanasema sana, ila kwakuwa China ina ubavu ndio maana wanakosa huo mwanya, na uoga uliopandikizwa kwa wachina juu ya chama cha kikomunisti hautoki haraka.
 
Hili ni genge la wahuni wachache wenye lengo la kutapeli maskini wa Tanzania
ushauri wa bure ni bora ungewekeza nguvu katika kujifunza kuandika.
 
Jamii gani iliyonufaika na ujamaa hao wachina c wamesambaa dunia nzima wanaokota makopo raia wa Magharibi omewaona wapi wakiokota makopo na mavyuma mabovu aacha ujamaa ni shida tupu ndio maana tanzania tulikuwa shida tupu wakati wa Nyerere au kijana ulikuwa bado hujazaliwa.

Wakati tunapanga foleni kununua mchele, sukari kutoka Ugawaji na NMC, tulipitia kipindi kigumu sana, ujamaa ni umaskini
 
China haina ujamaa tena,ni mabepari watupu.
Tena China na Urusi balaa
Njia zote za kumiliki uchumi zilikuwa chini ya Serikali. Wakaachana na huo mfumo wakaamua kubinafsisha nyingi wakajibinafsishia viongozi

Akina Putin na ma Oligarchs wake ndipo wakaibuka matajiri wa kutisha
 
Jina tu limeshawaondoa mchezoni, pili National Economical Reformational au..... Economic reforms.... Bora hata mngeiweka kiswahili
 
Chama kiwe HALFCAST, mixture ya UJAMAA na UBEPARI, ktk Katiba yake, kichukue strengthes za CCM na CDM.

Kiachane na Weaknesses za vyama hivyo, kireflect maoni ya wananchi ktk KATIBA mpya. Amen

Kinaweza kufanya yote hayo na bado kisipate wafuasi. Hiyo CDM na Ccm ni kama Simba na Yanga. Azam imechukua usimba na Uyanga kidogo lakini haipati washabiki bado.
 
Kinaweza kufanya yote hayo na bado kisipate wafuasi. Hiyo CDM na Ccm ni kama Simba na Yanga. Azam imechukua usimba na Uyanga kidogo lakini haipati washabiki bado.
Aim ni kuwa na vyama 3 strong, tupate balance wananchi, vyama vya mfukoni vifutwe vyote.

Ni maoni yangu ktk kuandika KATIBA mpya,ipi idadi inafaa ya vyama vya siasa vilete tija ktk Taifa.
 
Aim ni kuwa na vyama 3 strong, tupate balance wananchi, vyama vya mfukoni vifutwe vyote.

Ni maoni yangu ktk kuandika KATIBA mpya,ipi idadi inafaa ya vyama vya siasa vilete tija ktk Taifa.

Vyama serious nchi hii havizidi vitatu. Hivyo vingine ni kujazia hesabu ili kuhadaa dunia kuwa kuna demokrasia ya vyama vingi.
 
Wakati tunapanga foleni kununua mchele, sukari kutoka Ugawaji na NMC, tulipitia kipindi kigumu sana, ujamaa ni umaskini
Huku zenj kulikuwa na maduka ya ukoo ambako wiki mara moja unaruhusiwa kununua chakula kwa kiwango maaluum kutokana na familia yako ambayo imeotodheshwa kwenye kadi maaluum.
 
Kama kichwa cha habari hapo juu, tuko mbioni kusajili chama cha siasa kitakachosimia rasilimali za taifa kuwanufaisha wananchi wote wa Taifa hili.
Tanzania HAINA TATIZO la chama cha siasa kitakachosimia rasilimali za taifa kuwanufaisha wananchi wote wa Taifa hili. Vyama vilivyopo vinatosha kabisa.

TATIZO kuna chama dola (CCM) ambacho kinazuia vyama vingine kushika madaraka na/au kuwa na uwakilishi mkubwa bungeni. Kinazuia na/au kuchelewesha kuandikwa kwa katiba mpya itakayosimika misingi ya DEMOKRASIA MAKINI na UTAWALA BORA nchini. TATIZO ZAIDI ni kuendelea kwa propaganda za wapambe (bootlickers) kwamba BADO HAKUNA CHAMA MBADALA kinachoweza kuongoza nchi badala ya CCM!

Ni wananchi ndio wanaomua CHAMA SAHIHI cha kuongoza nchi kwa NGUVU YA KURA ZAO kupitia CHAGUZI HURU period. Wananchi kukosea ni haki yao na wanatakiwa kuwa na fursa kadhaa kurekebisha makosa kupitia chaguzi zinazofuatia na hatua kadhaa za kikatiba zinazokubalika kidemokrasia. Hayo ndiyo mabadiliko yanayotakiwa: KUWAPA WANANCHI NGUVU YA UAMUZI ya kuchagua wanaofaa na kuadhibu wasiofaa all the time.

Sio kazi ya majukwaa ya kisiasa yaliyojaa wapambe (SYCOPHANTS) kuamua nani au chama gani cha siasa kinafaa kuongoza milele.
 
Kinaweza kufanya yote hayo na bado kisipate wafuasi. Hiyo CDM na Ccm ni kama Simba na Yanga. i
Simba na yanga na CCM wana washabiki Tanzania bara na Zanzibar .Chadema Zanzibar haina kitu imezidiwa na washabiki wa simba, yanga na CCM

Chadema acha kuilinganisha na simba au yanga au CCM sio saizi ya Chadema
 
ujamaa ndio chanzo cha umaskini wa Tanzania. Ni ideology ambayo watu wengi hawailewi! Ni ujinga eti mitaala yetu inafundisha kugawana (sharing) wakati hatuna utajiri wa viwanda badala ya mitaala kufundisha kutafuta (capitalism = investment)!

hivi Nyerere alituonaje? bahati yake namheshimu alituletea uhuru na pia umaskini!@

nb: wazungu hawakumuelewa Nyerere pamoja na kuandika vitabu kibao nao wakaacha ibaki inasomeka "ujamaa" japokuwa yeye Nyerere "ujamaa" alimaanisha "socialism". This means Nyerere ali implement ideology ambayo hakuilewa!

Marxist theory is very complex ideology which tries to analyse ill effects of capitalism and offers solutions to exploitation and unequal distribution of means of production.

Sasa we Nyerere unaanzishaje ujamaa wakati huna utajiri wa viwanda katika nchi , utajiri unaowanufaisha wachache wenye viwanda au makampuni kupitia kulipa wafanyakazi mishahara midogo huku wakibeba faida yote wao?

Unaanzishaje socialism kupinga capitalism ambayo it doesn't exist?

unaanzishaje ujamaa wakati jamii yako ina many classes? Kuna wakulima, wafanyabiashara wadogo, wenye viwanda na makampuni, waajiriwa serikalini, waajiriwa sekta binafsi , na hapo hapo class ya waajiriwa wa serikali na sekta binafsi nao wameajiri houseboys housegirls, wana saluni na maduka,mashuleni, makampuni nk? ni vurugu mechi!

a true capitalist society inayoumiza vibarua wanaonyonywa "proletariat" ina two classes "capitalIst" or bourgeoisie na workers " proletariats" sasa Nyerere alipoanzisha "Ujamaa" je tulikuwa na capitalist society? je nchi ilikuwa imeendelea kwa viwanda?

yaani Nyerere alizingua kinoma!

Mimi naamini nauelewa ujamaa kuliko Nyerere!! nikizeeka nitaandika "socialism" kwa kiswahili ili kutofautisha na "ujamaa" wa Nyerere

in short "ujamaa" sio "socialism" na huwezi kufanya "socialism" bila kwanza nchi kuwa "capitalist" na ukilazimisha lazima ufeli maana sio muundo wake!!

huwezi kutembea bila kuanza kukaa na kusimama
Siupendi ujamaa. Nikisikia ujamaa nakuwa kama nimesikia umasikini
 
Kifupi Tanzania hatuna vyama serious vya upinzani hakiko vinavyobeba agenda ya wananchi

Chadema kipindi cha Dk Slaa akiwa katibu mkuu kilibeba agenda ya wananchi ambao kwa jumla wao walichoshwa na ufisadi

Chadema ikajipambanua kama mbeba agenda ya kupambana na ufisadi na wananchi wakakikubali sana .Baadaye Chadema ikageuka ikakumbatia mafisadi .Sasa inabweka tu ohh katiba mpya hilo sio Tatizo sugu Kero kwa watanzania wengi


Vyama vyote vya upinzani kifupi hakuna kibeba hoja za wananchi ni wachumia tumbo tu wasaka fursa tu
 
Kifupi Tanzania hatuna vyama serious vya upinzani hakiko vinavyobeba agenda ya wananchi

Chadema kipindi cha Dk Slaa akiwa katibu mkuu kilibeba agenda ya wananchi ambao kwa jumla wao walichoshwa na ufisadi

Chadema ikajipambanua kama mbeba agenda ya kupambana na ufisadi na wananchi wakakikubali sana .Baadaye Chadema ikageuka ikakumbatia mafisadi .Sasa inabweka tu ohh katiba mpya hilo sio Tatizo sugu Kero kwa watanzania wengi


Vyama vyote vya upinzani kifupi hakuna kibeba hoja za wananchi ni wachumia tumbo tu wasaka fursa tu
Wanasaka ruzuku tu hao haha

NGO,sacos fulani tu

Ova
 
Back
Top Bottom