Usajili wa ‘Kanisa la Neema’ uchunguzwe


Yule jamaa ana mafundisho mabaya sana. Halafu anaona wengine wajinga na kuwadharau. Mtu unasemaje kwamba. Hakuna dhambi, dhambi ilishamalizwa?. Anaipinga Biblia waziwazi na kusema kuna kitabu kingine kitakuja huko mbeleni .

Sasa si ajitoe kwenye ukristo aanzishe dhehebu lake nje ya ukristo au dini yake. Mtu anafundisha mambo tofauti na ukristo na kuwaona wasiokubaliana naye ni wajinga. Ninachoshukuru pamoja na kelele zake zote , wakristo hawana muda naye kama walivyompuuza Mfalme Zumaridi.
 
Mimi sijaona kosa lake otherwise kama mnataka yale yale ya kanisa katoliki kupinga wale wote waliokuwa wanataka kufundisha tofauti na walichokuwa wanafundisha wao.
Hata zumaridi walimwonea tu. Maana yeye hakuna sehemu aliwahi sema ni mkristo.
 
kwa kifupi, kama msikini na kanisa vinakaa pamoja na hakuna shida, sio taabu. wala hakuna mwenye chuki na uislam au ukristo kwenye hili. rudi kwenye mada, makanisa ambayo hata mlevi akiwaona anaona wazi kabisa kwamba ni wapigaji, wanawatapeli raia, serikali ikae kimya? au wewe ni mmojawapo. kuna siku watakuja kukuomba unyoe mavvuzi uwapelekee wakuombee na jinsi mlivyoshikwa akili, utapeleka.
 
Mimi sijaona kosa lake otherwise kama mnataka yale yale ya kanisa katoliki kupinga wale wote waliokuwa wanataka kufundisha tofauti na walichokuwa wanafundisha wao.
Hata zumaridi walimwonea tu. Maana yeye hakuna sehemu aliwahi sema ni mkristo.
huoni kosa kwasababu unasali kwake, umeshashikwa masikio. hujielewi. mtu anayetukana ukristo, mtu anayetukana biblia, na anajiita ni mchungaji, kweli huoni kosa? hujui kuna wananchi wengine akili zao sio nzuri kuna siku wanaweza kumshughulikia? wewe kama kiongozi mfano, unachukua hatua gani kuzuia madhara ya mbeleni?

pia, unajua kama amesajili kanisa? kama hajasajili hapo hakuna kosa? kwahiyo hata zumaridi matendo kama yale ni ya kikanisa? akili zenu zote mmewapa mitume mmebaki makopo.
 
Hata kuna watu wengine wanaona mwamposa mpigaji, wakatoliki na sadaka zao wapigaji.
Kwa hiyo kama mtazamo wa watu fulani ndio utahukumu kanisa fulani basi bila shaka yote yatafungwa.
 
Mimi sisali kwake kwanza nimemsoma kwenye thread hii.
As long as hajaua anafundisha maono yake fresh tu. Otherwise makanisa yaliyotangulia hapa nayo yangesema haya makanisa ya kuja yasiwepo mwanzo yanapotosha mafundisho.
 

Yule anatakiwa akatazwe kutumia Biblia atumie kitabu chake. Mtu amekaa kuikosoa Biblia kila saa. Ila nachoshukuru watu hawana time naye, wamempuuza amebaki kudanganya wasiojitambua. Unajiita mkristo halafu unadai hakuna dhambi duniani, hivyo watu wazini wabake nk.
 
anatakiwa asiwe amejisajili kama mkristo, kwasababu matendo yake yote yanapinga ukristo na yanakwaza ukristo na wakristo wote. swali ni je, aliposajili kanisa lake, kama kweli amesajili, alijisajili kama Mkristo? wa dhehebu gani, au anaanzisha dhehebu jipa n.k. shida ni kwamba, ofisi ya usajili kuna watu wazembe kupita kiasi kuna siku hapa yatatokea ya kibwetele na tutabaki midomo wazi. serikali kwanza ianze kuwajibisha watendaji pale kwenye usajili, iweke wale walio makini wanaosajili kanisa na kuanza kulifuatilia kama linaendana na minajili iliyoomba usajili.
 
Hahahaaa Mimi huyu? Nimerespond kwenye mfano WAKO wa ifakara na lawama zako juu ya wizara ya ardhi!
Kuhusu makanisa uchwara kwakweli labda wizara ya mambo ya Ndani ikae tena upya na kupitia sheria na kanuni za usajili wa hivyo' vikundi mana sio makanisa kanisa Lina hadhi yake kitaasisi, kiundeshaji HATA publicity! Naungana na Wewé lazima tuoitie Sheria upya Ili kuweka baadhi ya mambo Sawa asante
 
Hata kuna watu wengine wanaona mwamposa mpigaji, wakatoliki na sadaka zao wapigaji.
Kwa hiyo kama mtazamo wa watu fulani ndio utahukumu kanisa fulani basi bila shaka yote yatafungwa.
basi, kama wewe ni muumini wake, tuanzie tu hapo, mtume wako amelisajili hilo kanisa? au ndo kama vile shamba la bibi unafanya chocote unachopenda kufanya kama vile hakuna serikali.

wakatoliki au wengine hao wote uliowataja, hawajawahi kuukashifu ukristo, na bado wakajiita wakristo.

kama nabii suguye amefungiwa pamoja na uwepo wa waumini 4000, huyo ambaye waumini hata 100 hana, anategemea tv kuumiza mioyo ya wakristo, wanasubiri nini kumfyekelea mbali?
 
na wizara ya mambo ya ndani/ usajili imekaa kimya tu. mtu anajiita mkristo halafu anakosoa ukristo, sasa anahubiri kwa mujibu wa usajili wake au la?
 

Usihamishe mada. Umeelewa anachokiongelea? Mind your business kwenye mambo ya imani. Mtu anasema hakuna dhambi duniani, wewe zini ulishasamehewa is that appropriate.

Ukristo unaanguka kutokana na watu kujifanya hayawahusu mpaka serikali iingilie kati. Watu wanafanya mambo ya hovyo utasema you mind your own business. Juzi hapa Nandy kafunga ndoa mbele ya kanisa huku ana mimba kubwa ila ukiuliza unaambiwa mind your business.

Uislamu unakuwa kwa sababu watu hawatoralete ujinga kwenye imani. Ukifanya ujinga unachukuliwa hatua au kuomba radhi. Huku kwenye ukristo ni shida kila mtu anajiamulia anavyotaka.
 
pima upana wa hilo barabala kutoka msikiti ulipo mpaka kanisa lilipo usiongee kujifurahisha kuishi karibu na kanisa la kirokole ni kazi kuvumilia vilio hivio na mziki sio lazima pia kwa nini mkuu wa wilaya hataki kutusikiza kwani kuna ulazima ganikati ya msikiti na kanisa kuwa sehemu 1 uliwai kuona kanisa la loma na kirokole wanatengenishwa ukuta
 
Akili yako inafurahisha.
Kwa hiyo mimi nikiwa against na mtazamo wako basi nasali kwa huyo jamaa.
We ni nani kujua nini sawa na nini si sawa?
Yani kwa mawazo yako basi lingebaki kanisa katoliki pekee duniani maana mengine yote yalikuwa against it na kwa mtazamo wake hayakuwa sawa.
Mwache jamaa apige pesa mbona akina ngwajima, mwamposa wanapiga pesa kwa bible hiyo hiyo tu
 
Mimi sisali kwake kwanza nimemsoma kwenye thread hii.
As long as hajaua anafundisha maono yake fresh tu. Otherwise makanisa yaliyotangulia hapa nayo yangesema haya makanisa ya kuja yasiwepo mwanzo yanapotosha mafundisho.
unasubiri auwe kama alivyouwa kibwetele ndio uone kuwa anachofanay sio sahihi?
 
basi, kama mnaona mpo karibu sana, aliyetangulia kujenga ndio abaki, aliyekuja baadaye ampishe mwenzake. kwani waliotoa vibali mjenge hawakuona hilo? au watu walijijengea tu?
 
wewe hujielewi,ni zombie wake. ngoja nikupishe tu.
Wewe ndio hujielewi unajifanya unapanga kipi sawa kipi si sawa. Kama wanafuta wafute makanisa yote maana yanawafanya watu wanakuwa mazombie otherwise waache tu watu wajipgie pesa bila double standards
 
Mwenye kanisa, elimu ya chini ni degree ya Theology kutoka chuo kinachotambulika, ikiwezekana na somo la falsafa. Tuige mfano wa Rwanda.

Kweli kabisa. Sio sasa hivi kila mtu anajiita nabii. Anafungua kibanda anaanza maunabii yake yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Tujifunze kwa wenzetu waislamu huwezi kuswalisha mpaka umepata mafunzo ya Quran au kwa wakatoliki ambao ili uwe padri lazima usomee muda mfrefu.

Mtu unaamka asubuhi unajiita nabii Econonist , huna elimu unadanganya watu kuhusu maono. Maoni bila kuijua Biblia utaangusha watu kama walivyofanya akina Kibwetere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…