Tetesi: Usajili wa Mabasi ishirini mapya ya Abood

Kwa comfortability kiukweli BM yuko vema sanaa kwa hiyo route na ile ya Moro to Arusha...
 
Ndiyo zake route ndefu zote huwa anapeleka mingalangala... Bus mpya anapeleka Dar to Moro
 
Pia ameshindwa kujiongeza kwamba kwenye Bus la watu 60 huwezi kukosa wazee, wenye magonjwa mbalimbali kama vidonda vya tumbo, kisukari etc ambao huwezi kumburuza masaa 3 mpaka 4 bila ya kutia chochote mdomoni au kupata huduma bora ya maliwato. Yaani anajifikiria yeye tuu...
 
300 hayafiki mkuu, muda mwingine tusipende kukuza mambo. Hata mm nipo moro hapa na sehemu zake zote garage nk nazifahamu. Utajiri anao ila mabus miatatu uongo kabisa.
Kweli mkuu ile gereji yake pale mbele ya wauza mbao wa Fire ibebe Bus 300?
 
Waluguru huwaambii kitu kwa abood
Utawasikia: Ausindilee, anajibiwa anogaaa.... Anaendelea: mwenzio nimerudi juzi toka Daa na Abudii... Mweeee safari hii bwana Kobelo si nikawakomesha deleva na konda wake... Ilikuwa mzigo wangu nishushie Kimara mi nikabana kinaenda mpaka Ubungoo, yaani nimewakomesha kweli kweli...
 
Ahaaa in mkude simba voice
 
Basi halitakiwi kupark,linatakiwa kuwa barabarani au garage,isitoshe tanzania kuna stand kila mkoa,abood ana stand zake binafsi na garage zake binafsi
Kampuni pekee ambayo iliweza kuwa na stend zake binafsi kwa Morogoro ni Scandinavia (stend yake ilikuwa pale Msamvu round about ambapo sasa hivi imejengwa kituo cha mafuta). Mwingine alikuwa ni Hood Bus, ambaye sasa anachechemea. Abood pale mjini ilikuwa ni kushusha parcels tuu na kule gereji ni services na kujaza mafuta.
 
Ajabu kweli mi nafikiri hakuna umuhimuwa kusimama kwa safari ya saa. 3-4
Kwa hiyo wewe kama uko vizuri Kiafya unahitimisha kwamba kwenye kundi la abiria 60 wote wako fiti kama wewe? Hakuna wenye vidonda vya tumbo, kisukari, tezi dume na kadhalika?
 
[emoji1666][emoji1666][emoji1666]
 
Huo ni utajiri ambao ni manual mimi nimezungumzia digital......
matajiri wote wa sasa duniani wapo kwenye digital........
in combination with little manual
Abood ameanza biashara ya Bus 1990s huko, alikuwa na vi bus vichache na duka la jumla pale ilipo main office (nadhani hilo duka lilikuwa la baba yao, na hata hizo bus). Sasa hivi amekuwa mzoefu na katoa mpaka kumtoa kwenye gemu Hood na Islam halafu unashauri aache kitu alichozoea?
 
kumchamba tajiri kunakupa unafuu gani mlalahoi mwenzangu??
Kuna vitu Magufuli alikuwa anasema ukweli, na nilikubaliana naye. Mfano Magufuli alimpa makavu live Abood kwamba amenunua viwanda badala ya kuviendeleza aliuza mitambo na kuvitumia kuchukulia mikopo na pesa akanunulia ma Bus, kwa walio Moro wanajua hiyo ni kweli. Hata lile jengo ilipokuwa Redio Abood na TV yake nilisikia Magu alielekeza lirudishwe serikalini, nadhani limerudishwa. Pia vijembe alivyopigwa na Magu kwamba badala ya kununua ambulance yeye anawaletea watu Bus iliyochoka kubeba maiti (almaarufu Bundi) vilisaidia akajiongeza na kununua ambulance (nilisikia kanunua, am not sure).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…