Jiongeze kidogo basi, au wewe ni product wa hii elimu yetu iliyologwa nini? Maana kizazi cha shule hizi ni majanga.
1. Umeona hapo sikutaja ugali wala makande, nimesema bites. Hilo umeshindwa kuona inamaanisha nini?
2. Haya, umetoka Moro na gari ya kwanza. Yani ukae mdomo unanuka na njaa mpaka Dar kisa kuna mtu kama wewe anasema safari ya saa tatu huhitaji kula? Siku hizi chai unauziwa kwenye kibobo chako safi, unaingia nacho garini.
3. Kwahiyo, ushawaza na kuona kuwa ulionao wote ndani ya gari mpo sawa. Wamekula kama wewe, wanajisikia haja kama wewe n.k. na hivyo,vile unajisikia wewe,abiria wote wanajisikia hivyo.
Ninadhani hapa umeathiriwa na mawazo yetu yale ya kudhani unachowaza wewe ndiyo ulimwengu. Walimwengu hatupo sawa kama ulivyokariri. Aidha, maisha yamebadilika, mengine tuliyafanya sababu ya kukosa uwezo, fursa na sehemu za kufanya haya. Mwaka 80 si sawa na 2021.
Tafakari, chukua hatua