Usajili wa Simba ni bora kabisa, kama ni ukweli

Mimi nadhani Simba ndio timu ambayo haina presha kabisa kwenye kusajili wachezaji wa kigeni.
Wanatakiwa kumrejesha Fraga (kama yuko fit) ili aje kuchukua nafasi ya Chikwende na Kahata (ili ku restore idadi ya wachezaji 10 wa kigeni).

Kama wanaweza kupata better option ya beki wa kati kuliko Wawa basi wafanye replacement. Japokua sio muhimu sana kwenye nafasi hii.

Kama wanaweza kupata better option ya mshambuliaji mmoja wa kum replace Mugalu au Kagere basi wafanye hivyo. Japokua sio muhimu sana kwa aina ya nafasi na aina za magoli ambayo Simba wanafunga (Viungo wanachangia magoli mengi sana)

Uwepo wa Morrison na Miquissone unamfanya Chikwende akose namba automatically kwenye kikosi cha kwanza. Wachezaji wa kutokea benchi kwenye nafasi hizi hata wa ndani akina Dilunga wanatosha.

1 Onyango
2 Wawa (au mgeni mwingine bora zaidi yake)
3 Fraga
4 Lwanga
5 Bwalya
6 Chama
7 Morrison
8 Miquessone
9 Kagere
10 Mugalu

Kati ya Kagere na Mugalu Simba wanaweza kuweka mshambuliaji mgeni mmoja bora zaidi.

Kwa maoni yangu hao jamaa wataisaidia sana Simba, na kwa minajili hiyo Simba inahitaji mgeni mmoja wa lazima (FRAGA or any of the like).
Ikiamua inaweza kuongeza wawili nafasi ya Wawa na Medie/Mugalu.

Kwa maoni yangu pressure ni ndogo.
Mimi bado kwa mtizamo wangu presha bado ni kubwa sana kwa Simba kwa usajili wa wachezaji wa kigeni. Ukiangalia kwa haraka haraka kwa hao wachezaji wa kigeni utaona wapo sawa lakini ni kwa ligi ya ndani tu pale unapopambana na Yanga mbovu na akina Ihefu huko lakini sio kwa CL. Pia mpira unabadilika na mwakani fedha za udhamini zimeongezwa kwa hiyo usitegemee kabisa ligi itakuwa rahisi. Pia usitegemee Yanga na Azam mbovu mwakani kwani kwa mafanikio iliyopata Simba mwaka huu kwenye CL jua wazi timu hasa Yanga wanakwenda kujiimarisha sana tu vinginevyo wasipotoa ushindani msimu ujao lazima bakora zitembee Jangwani na ni lazima GSM atatafutiwa mlango wa kutokea.

Tukija kimataifa bila kupepesa macho Simba itahitaji isajili wachezaji watatu wa kimataifa:-
1. Beki wa kati mmoja mwenye uwezo zaidi ya Onyango na Wawa. Kwenye CL japo Simba ilifika robo fainali kulikuwa na makosa yanaonekana wazi hasa kwenye krosi na kona hivyo inahitajika beki ambaye ataweza kufuta hayo makosa kwani wakati mwingine ilikuwa ni bahati tu washambuliaji wa timu pinzani walishindwa kuyatumia hayo madhaifu ya mabeki wa kati wa Simba.
2. Kiungo mmoja mwenye uwezo wa kukaba kweli kweli na ujuzi wa kushambulia "box to box midfield" ambaye ana umbo kubwa. Ukiangalia kwenye CL Simba ilikuwa inapata shida sana katikati kutokana na viungo wengi wa timu ya Simba wana maumbo madogo na wa timu pinzani wengi wao walikuwa mafundi lakini pia walikuwa na kitu cha ziada ambacho ni maumbo makubwa. Na hapa ashukuriwe sana aliyemleta Lwanga kwani kwa kiasi kikubwa ndiye mchezaji pekee wa Simba aliyekuwa na uwezo wa kupambana nao kwenye zile 50/50.
3. Simba pia itahitaji mshambuliaji wa kimataifa mmoja mwenye uwezo zaidi ya Kagere na Mugalu. Ukiangalia kwenye CL Simba ilitengeneza nafasi nyingi sana lakini zilikuwa zinapotea. Kwa hiyo basi kuna uhitaji wa kumuondoa mshambuliaji mmoja kati ya Kagere na Mugalu na kuleta mwingine ambaye atakuwa anatumia hizo nafsi kwa usahihi sana. Pia uwezo mdogo wa Kagere na Mugalu kwenye kufunga kwa vichwa ni tatizo ukizingatia mabeki wa pembeni na viungo wa pembeni wa Simba wanapiga krosi nyingi sana tena kwa usahihi mkubwa.

Kwa vyovyote ilivyo kwa wachezaji kigeni waliopo Simba wanaweza leta ushindani kwenye ligi ya ndani na Simba ikafanya vizuri hata kwa misimu miwili ijayo. Lakini iwapo kweli Simba inataka kufika zaidi ya robo fainali kwenye CL basi lazima ilete wachezaji wapya wa kimataifa wasiopunguwa watatu. Sasa presha kwa Simba inakuja aachwe nani kati ya waliopo? Mbaya zaidi ni huu uswahili wetu kuwa Simba ikimuacha fulani ataenda Yanga. Lakini ili Simba wafanikiwe kwenda zaidi ya robo fainali ya CL ni lazima uongozi ujilipuwe ulete wachezaji wapya watatu wenye uwezo zaidi ya waliopo. Na kujilipuwa maana yake unaweza acha mchezaji akaenda fanya vizuri na yule uliyemleta japo mzuri zaidi akashindwa kuingia kwenye mfumo wako kama ilivyotokea kwa Chikwende. Haya ni maoni tu lakini naamini viongozi wa Simba wapo makini zaidi na watafanya yaliyo sahihi kwenye usajili ujao.
 
Yaani anavyojadiliwa hapa unaweza ukasema ni bonge la mchezaji!!
 
Kocha kishingo kipindi yuko simba alitamani sana kupata beki mrefu wa kati anayetumia mguu wa kushoto kama ilivyokuwa kwa Ally Sonso ambaye shida yake ni mistakes nyingi, mwingine ni Abdi Banda ambaye kwa kweli sidhani kama kuna mtu anataka kuiona sura yake pale Msimbazi.

Sasa leo nasikia Edward Manyama kasaini miaka miwili, kama ni kweli HONGERENI SANA KAMATI YA USAJILI huyu abadilishwe awe anacheza nne au tano na sababu naturally ni namba 3 atakuwa ana mpa back up kubwa sana gadiel michael na zimbwe jr.

Hapo sasa kabaki Michael Phiri attacking midfielder wa zanaco kazi kweisha kabisa, na kiungo mkabaji mrudisheni fraga, wachukue nafasi za chikwende na kahata. Issue za shabi juma achana nazo namba mbili hata onyango na nyoni wanacheza hata ame Ibrahim aanze kuzoeshwa hiyo namba.
Simba wanahitaji sana namba nane bora zaidi ya Bwalya pendekezo langu ni Morlaye Sylla wa Horoya Fc
 
Umechambua vizuri sana. Nakuunga mkono asilimia 100.
Kitu ambacho kinanipa matumaini makubwa ni uwezo mkubwa wa mbinu na kuusoma mchezo ambao kocha wa sasa wa Simba ameuonyesha so far, kwa hiyo nina uhakika kabisa tayari kocha kichwani kwake anajua ni wachezaji gani/aina gani awaongeze kwenye usajili na kina nani awaache. Cha muhimu tu, uongozi umsikilize anachotaka kocha, wasilete mambo ya Kiswahili.
Ili Simba itoboe beyond robo fainali next CL ni MUHIMU SANA isajili wachezaji wasiopungua WATATU wa KIMATAIFA ambao ni wazuri zaidi ya hawa waliopo. WAZURI ZAIDI!! Yaani Simba sasa hivi haitakiwi kabisa kwenda kusajili mchezaji wa level ya Mugalu kwa mfano,au Wawa....! Sio kwamba ni wabaya, bali kutoboa zaidi ya robo fainali inahitajika timu wawe na wazuri zaidi ya hawa!!
Umeeleza vizuri sana mkuu!!
 
Mimi bado kwa mtizamo wangu presha bado ni kubwa sana kwa Simba kwa usajili wa wachezaji wa kigeni. Ukiangalia kwa haraka haraka kwa hao wachezaji wa kigeni utaona wapo sawa lakini ni kwa ligi ya ndani tu pale unapopambana na Yanga mbovu na akina Ihefu huko lakini sio kwa CL. Pia mpira unabadilika na mwakani fedha za udhamini zimeongezwa kwa hiyo usitegemee kabisa ligi itakuwa rahisi. Pia usitegemee Yanga na Azam mbovu mwakani kwani kwa mafanikio iliyopata Simba mwaka huu kwenye CL jua wazi timu hasa Yanga wanakwenda kujiimarisha sana tu vinginevyo wasipotoa ushindani msimu ujao lazima bakora zitembee Jangwani na ni lazima GSM atatafutiwa mlango wa kutokea.

Tukija kimataifa bila kupepesa macho Simba itahitaji isajili wachezaji watatu wa kimataifa:-
1. Beki wa kati mmoja mwenye uwezo zaidi ya Onyango na Wawa. Kwenye CL japo Simba ilifika robo fainali kulikuwa na makosa yanaonekana wazi hasa kwenye krosi na kona hivyo inahitajika beki ambaye ataweza kufuta hayo makosa kwani wakati mwingine ilikuwa ni bahati tu washambuliaji wa timu pinzani walishindwa kuyatumia hayo madhaifu ya mabeki wa kati wa Simba.
2. Kiungo mmoja mwenye uwezo wa kukaba kweli kweli na ujuzi wa kushambulia "box to box midfield" ambaye ana umbo kubwa. Ukiangalia kwenye CL Simba ilikuwa inapata shida sana katikati kutokana na viungo wengi wa timu ya Simba wana maumbo madogo na wa timu pinzani wengi wao walikuwa mafundi lakini pia walikuwa na kitu cha ziada ambacho ni maumbo makubwa. Na hapa ashukuriwe sana aliyemleta Lwanga kwani kwa kiasi kikubwa ndiye mchezaji pekee wa Simba aliyekuwa na uwezo wa kupambana nao kwenye zile 50/50.
3. Simba pia itahitaji mshambuliaji wa kimataifa mmoja mwenye uwezo zaidi ya Kagere na Mugalu. Ukiangalia kwenye CL Simba ilitengeneza nafasi nyingi sana lakini zilikuwa zinapotea. Kwa hiyo basi kuna uhitaji wa kumuondoa mshambuliaji mmoja kati ya Kagere na Mugalu na kuleta mwingine ambaye atakuwa anatumia hizo nafsi kwa usahihi sana. Pia uwezo mdogo wa Kagere na Mugalu kwenye kufunga kwa vichwa ni tatizo ukizingatia mabeki wa pembeni na viungo wa pembeni wa Simba wanapiga krosi nyingi sana tena kwa usahihi mkubwa.

Kwa vyovyote ilivyo kwa wachezaji kigeni waliopo Simba wanaweza leta ushindani kwenye ligi ya ndani na Simba ikafanya vizuri hata kwa misimu miwili ijayo. Lakini iwapo kweli Simba inataka kufika zaidi ya robo fainali kwenye CL basi lazima ilete wachezaji wapya wa kimataifa wasiopunguwa watatu. Sasa presha kwa Simba inakuja aachwe nani kati ya waliopo? Mbaya zaidi ni huu uswahili wetu kuwa Simba ikimuacha fulani ataenda Yanga. Lakini ili Simba wafanikiwe kwenda zaidi ya robo fainali ya CL ni lazima uongozi ujilipuwe ulete wachezaji wapya watatu wenye uwezo zaidi ya waliopo. Na kujilipuwa maana yake unaweza acha mchezaji akaenda fanya vizuri na yule uliyemleta japo mzuri zaidi akashindwa kuingia kwenye mfumo wako kama ilivyotokea kwa Chikwende. Haya ni maoni tu lakini naamini viongozi wa Simba wapo makini zaidi na watafanya yaliyo sahihi kwenye usajili ujao.

Napingana na wewe kwamba mafanikio ya Simba yamechagizwa na ubovu wa Yanga na Azam. Naamini ubora wake Simba ndio umeleta mafanikio katika msimu huu. Kama Simba isingekua bora basi isingeweza kupata matokeo mbele ya Ahly, AS Vita, Platnum, Plateau na Kaizer (marudiano). Vinginevyo unambie kwamba hizo timu nazo ni "mbovu" kama Azam na Yanga.

Kwenye hoja zako namba 1, 2 na 3 mimi na wewe tuna mtazamo mmoja.

Ila najiuliza tu, hivi kigugumizi kinatoka wapi kumwacha mchezaji bora kama umepata mchezaji bora zaidi ?
Kama Simba inampata beki MATHOHO wa Kaizer then ugumu wa kumwacha Wawa unatoka wapi hata kama ataenda Yanga ?

Suala jingine, unaposema kwamba Simba ndio ina presha zaidi kwenye suala la kusajili wachezaji wa kigeni maana yake umeilinganisha na Yanga.
Kwa maneno yako hapo juu, Simba inatakiwa kufanya ukarabati kwenye nafasi TATU.
Nikiangalia kikosi cha Yanga naona wanatakiwa kufanya ukarabati kwenye nafasi SITA au SABA za wageni (ukimtoa Mukoko, Kisinda na Yacouba, wageni wengine sioni kama wataisaidia chochote Yanga kwenye mechi za kimataifa. Saido anaweza kuingia hapa au kutoka kutokana na kigezo cha umri).

Sasa timu yenye kutakiwa kuboresha nafasi tatu inawezaje kuwa na presha kubwa kuliko ile yenye nafasi sita au saba za kuboresha ?

NB: Kiuhalisia katika nafasi ya ushambuliaji pale Simba, kuamua kuboresha kwa kubadili mshambuliaji ni hitaji la kianasa (leisure) wala sio hitaji la msingi maana "attacking system" ya Simba inafunga sana magoli.
Na hili limedhihirika si tu kwenye ligi ya ndani, hata kwenye mashindano ya CAF.
Ni washambuliaji wachache sana wanaofunga japo 70% ya nafasi wanazozipata, wachache sana.

Bado ninaamini Simba wana presha ndogo katika usajili wa mwaka huu, hasa wachezaji wa kigeni.
 
Simba wanahitaji sana namba nane bora zaidi ya Bwalya pendekezo langu ni Morlaye Sylla wa Horoya Fc
Hivi mkuu, kwa mfano nikasema "Simba inahitaji golikipa bora zaidi ya Manula, pendekezo langu mimi ni El Shenawy wa Al Ahly" ninaweza kuwa sahihi ?
Najaribu kuuelewa mchango wako hapo juu.
 
Nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa sana tu. Inawezekana tunazungumza kitu kimoja katika lugha tofauti. Presha ya Simba ni kubwa sana kwenye usajili wa wachezaji wa kigeni kutokana na "standard" iliyoweka Simba kwenye mashindano mbalimbali hasa kimataifa. Kwani kwa sasa ukiizungumzia Simba unakuwa unazungumzia robo fainali ya CL na mtizamo sasa ni kwenda zaidi ya hapo yaani nusu fainali. Ukiangalia kwa asilimia kubwa wachezaji wa kigeni wa Simba wote wanafanya vizuri lakini Simba inatakiwa iende zaidi ya robo fainali ya CL. Presha inakuja kuwa utamuacha nani wakati waliopo wanafanya vizuri? Na jee huyo atakayeletwa atakuwa bora zaidi ya aliyeondoka na ataendana na mfumo wa Simba?

Pili Yanga na Azam mbovu zimeisaidia sana Simba kushiriki kimataifa "comfortably". Kwa sababu wakati Simba inashiriki kimataifa huku nyumbani Yanga na Azam walikuwa wanavurunda sana. Hii iliwapa Simba utuilivu mkubwa mno kwenye ushiriki wao kimataifa. Ndio maana mpaka leo Simba hajamaliza viporo lakini anaoongoza ligi kwa zaidi ya pointi sita. Iwapo Yanga na Azam wangekuwa vizuri kwa vyovyote vile ingekuwa inavuruga utulivu wa Simba kwani ingekuwa ndani moto na nje moto. Na ili ushiriki CL ni lazima ushinde ligi ya ndani na si vinginevyo.

Kwa Simba kuhitaji mshambuliaji tena yule anayetumia "half chance" ni muhimu kuliko kitu kingine chochote kile kwa msimu ujao. Ukiangalia mechi nyingi za CL utaona nafasi za wazi ni adimu sana saa nyingine hazizidi hata tatu kwenye mchezo mzima. Sasa kwa hao washambuliaji wa kati wa Simba wanaokosa mpaka nafasi nne za wazi kwenye mechi moja unategemea Simba itatoboa kirahisi kwenda zaidi ya robo fainali Afrika.
 
Kwa maoni yako ni kwamba kwenye nafasi ya ushambuliaji tusibadili chochote ?

Kama itafanyika kama ulivyopendekeza bado idadi ya wageni itazidi 10, kama ifuatavyo:
1. Onyango
2. Wawa
3. Lwanga
4. Bwalya
5. Chama
6. Morriston
7. Milestone
8. Kaveri
9. Mugalu
10. Fraga
11. Michael Phiri

Itakuaje hapo ?
Namba 7 na 8 mbona hata sijawahi kuwaona wakicheza??
 
Nakubaliana na wewe kwa sehemu kubwa sana tu. Inawezekana tunazungumza kitu kimoja katika lugha tofauti. Presha ya Simba ni kubwa sana kwenye usajili wa wachezaji wa kigeni kutokana na "standard" iliyoweka Simba kwenye mashindano mbalimbali hasa kimataifa. Kwani kwa sasa ukiizungumzia Simba unakuwa unazungumzia robo fainali ya CL na mtizamo sasa ni kwenda zaidi ya hapo yaani nusu fainali. Ukiangalia kwa asilimia kubwa wachezaji wa kigeni wa Simba wote wanafanya vizuri lakini Simba inatakiwa iende zaidi ya robo fainali ya CL. Presha inakuja kuwa utamuacha nani wakati waliopo wanafanya vizuri? Na jee huyo atakayeletwa atakuwa bora zaidi ya aliyeondoka na ataendana na mfumo wa Simba?

Pili Yanga na Azam mbovu zimeisaidia sana Simba kushiriki kimataifa "comfortably". Kwa sababu wakati Simba inashiriki kimataifa huku nyumbani Yanga na Azam walikuwa wanavurunda sana. Hii iliwapa Simba utuilivu mkubwa mno kwenye ushiriki wao kimataifa. Ndio maana mpaka leo Simba hajamaliza viporo lakini anaoongoza ligi kwa zaidi ya pointi sita. Iwapo Yanga na Azam wangekuwa vizuri kwa vyovyote vile ingekuwa inavuruga utulivu wa Simba kwani ingekuwa ndani moto na nje moto. Na ili ushiriki CL ni lazima ushinde ligi ya ndani na si vinginevyo.

Kwa Simba kuhitaji mshambuliaji tena yule anayetumia "half chance" ni muhimu kuliko kitu kingine chochote kile kwa msimu ujao. Ukiangalia mechi nyingi za CL utaona nafasi za wazi ni adimu sana saa nyingine hazizidi hata tatu kwenye mchezo mzima. Sasa kwa hao washambuliaji wa kati wa Simba wanaokosa mpaka nafasi nne za wazi kwenye mechi moja unategemea Simba itatoboa kirahisi kwenda zaidi ya robo fainali Afrika.
Nakubaliana na wewe, (tunakubaliana kwenye hoja karibia zote).

Hapo mwishoni, ni lazima tukubaliane kwamba aina hiyo ya washambuliaji ni wachache sana (sio Afrika tu, bali duniani kwa ujumla) na they are very hard to find and sign.

Sijui kama una pendekezo lolote ambalo liko feasible, karibu tafadhali...
 
Kocha kishingo kipindi yuko simba alitamani sana kupata beki mrefu wa kati anayetumia mguu wa kushoto kama ilivyokuwa kwa Ally Sonso ambaye shida yake ni mistakes nyingi, mwingine ni Abdi Banda ambaye kwa kweli sidhani kama kuna mtu anataka kuiona sura yake pale Msimbazi.

Sasa leo nasikia Edward Manyama kasaini miaka miwili, kama ni kweli HONGERENI SANA KAMATI YA USAJILI huyu abadilishwe awe anacheza nne au tano na sababu naturally ni namba 3 atakuwa ana mpa back up kubwa sana gadiel michael na zimbwe jr.

Hapo sasa kabaki Michael Phiri attacking midfielder wa zanaco kazi kweisha kabisa, na kiungo mkabaji mrudisheni fraga, wachukue nafasi za chikwende na kahata. Issue za shabi juma achana nazo namba mbili hata onyango na nyoni wanacheza hata ame Ibrahim aanze kuzoeshwa hiyo namba.
Striker simba hatuna
 
Nakubaliana na wewe, (tunakubaliana kwenye hoja karibia zote).

Hapo mwishoni, ni lazima tukubaliane kwamba aina hiyo ya washambuliaji ni wachache sana (sio Afrika tu, bali duniani kwa ujumla) na they are very hard to find and sign.

Sijui kama una pendekezo lolote ambalo liko feasible, karibu tafadhali...
Jaribu kumfatilia Moses Phiri wa Zanaco ya Zambia anaweza kufaa au wavunje benki wamchukue Prince Dube,ingawa Dube itakuwa ngumu kwa kuwa ameongeza muda kwenye mkataba wake.
 
Hawa wanaotajwa sijui bwalya na makusu kwasasa yamebaki majina tu,lazima tujue kua tayari tumetengeneza standard ktk champions league ya kufika robo fainali na kubaki ktk standard hiyohiyo ni kazi ngumu zaidi,kwangu kama mdau na mshabiki wa Simba zipo nafasi ambazo zinahitaji watu wa maana pale,nafasi ya kapombe inahitaji mtu atakayempa challenge yule duchu ni mzuri ila sio kwa champions league msimu huu tunashukuru shomari hajapata injury,nafasi za shabalala Kama kweli amekuja manyama ni usajili mzuri.Beki wa kati Wawa tumpe mkono wa kwaheri tunahitaji mtu wa nje tena awe zaidi ya wote pale kwa nafasi yao,kiungo mkabaji awepo mtu mzoefu wa ligi ya mabingwa ambaye atamzidi vitu vingi tadeo,kiungo mshambuliaji sioni tatizo,ushambuliaji inabidi tukubali kumuacha kagere aende ila tusajili mshambuliaji mkali kuliko bocco na mugalu hao wakina makusu bado hawajarudi ktk viwango vyao inabidi tusiijaribu hii nafasi.
 
Hivi mkuu, kwa mfano nikasema "Simba inahitaji golikipa bora zaidi ya Manula, pendekezo langu mimi ni El Shenawy wa Al Ahly" ninaweza kuwa sahihi ?
Najaribu kuuelewa mchango wako hapo juu.
Morlaye Sylla anamaliza mkataba wake this June.

Pili Bwalya anashindwa kucheza mechi physical ndiyo maana mechi zinazohitaji nguvu hupoteana.

Kamuangalie Morlaye Sylla kijana mwenye 22 years uje ulinganishe na Bwallya.
 
Huyu dogo akisajiliwa Simba, tutakuwa tumesajili Miquissone mwingine lakini anayejua kukaba vizuri.
 
Yes sema yeye anacheza namba nane na kumi anaweza pia kucheza wing ya kushoto kifupi ni midfielder bora sana kwa level ya Simba anamaliza mkataba wake soon.
 
Jaribu kumfatilia Moses Phiri wa Zanaco ya Zambia anaweza kufaa au wavunje benki wamchukue Prince Dube,ingawa Dube itakuwa ngumu kwa kuwa ameongeza muda kwenye mkataba wake.
Simba wamchukue Prince Dube ni striker ambaye kwenye kikosi badala ya kwenda mbali sana.
 
Hawa wanaotajwa sijui bwalya na makusu kwasasa yamebaki majina tu,lazima tujue kua tayari tumetengeneza standard ktk champions league ya kufika robo fainali na kubaki ktk standard hiyohiyo ni kazi ngumu zaidi,kwangu kama mdau na mshabiki wa Simba zipo nafasi ambazo zinahitaji watu wa maana pale,nafasi ya kapombe inahitaji mtu atakayempa challenge yule duchu ni mzuri ila sio kwa champions league msimu huu tunashukuru shomari hajapata injury,nafasi za shabalala Kama kweli amekuja manyama ni usajili mzuri.Beki wa kati Wawa tumpe mkono wa kwaheri tunahitaji mtu wa nje tena awe zaidi ya wote pale kwa nafasi yao,kiungo mkabaji awepo mtu mzoefu wa ligi ya mabingwa ambaye atamzidi vitu vingi tadeo,kiungo mshambuliaji sioni tatizo,ushambuliaji inabidi tukubali kumuacha kagere aende ila tusajili mshambuliaji mkali kuliko bocco na mugalu hao wakina makusu bado hawajarudi ktk viwango vyao inabidi tusiijaribu hii nafasi.
Kwa Beki wa Kati Simba options zetu ni hawa watatu.

1.Salomon Bidnjeme Banga wa Cotton Sports

2. Adrian Chama wa Zesco United.

3. Mohamed Quattara wa Al Hilal Omdumarn.

Hao watakuwa ni mbadala wa Wawa kwetu.
 
Back
Top Bottom