Lee Van free
JF-Expert Member
- Aug 14, 2024
- 2,833
- 8,777
Ninaposema Usalama wa Taifa,Jeshi na Polisi hapa namaanisha nyinyi wakubwa viongozi wa Vyombo hivi,mnatukosea sana sisi Watanzania wenzenu.
Hata hivyo bila kusahau hata ma junior wa Vyombo hivi, mnatukosea sana sisi Watanzania wenzenu.
Mnatukosea kwa sababu tumekua tunaongea miaka nenda miaka Rudi juu ya nchi yetu hii sote nyinyi na sisi kua Kuna tatizo kubwa la haki za kisiasa katika nchi yetu hii.
Tumetumia njia za haki kudai haki kama BUNGE, MAHAKAMA,mikutano,makongamano na Kila aina ya mikusanyiko halali lkn kikundi kidogo TU kinachoitwa CCM kimekua kikikwamisha upatikanaji wa haki hizo.
Sehemu kubwa ya haki hizo zinahusu uandikwaji wa Katiba mpya itakayokidhi matakwa ya Watanzania wote.
Wananchi kupitia makundi mbalimbali wamepiga kelele juu ya hitajio hili lkn hakuna aliejali juu ya kelele hizo.
Nyinyi Usalama wa Taifa na Jeshi na hata polisi mlikaa kimya TU.
Watu wakawaomba muingilie kati lkn hamkuchukua hatua zozote.
Matokeo yake kwa mara ya kwanza Watanzania waliuwawa kwa maelfu,nyie mko kimya TU.
Amini nawaambia Kuna maafa mengine makubwa yatakuja kama msipochukua hatua.
Haijaisha Ile,Mimi sio nabii lkn Kwa kuangalia TU body language za Watanzania bado Wana kiu na mahitaji Yao ambayo ni Katiba.
Katiba ndio itatututliza na kutuunganisha Watanzania yaani wa bara na visiwani.
"Naomba niweke sawa,hapa sisemi kupindua serikali,hapana".
Hapa nazungumzia nguvu za ushawishi wenu hasa Usalama wa Taifa na JWTZ na nguvu za utaalamu wenu hasa usalama wa Taifa na nguvu za ushwawishi wenu Polisi.
Kwa kifupi sana mnaweza mkaishauri Serikali ya CCM juu ya hatari na madhara ya machafuko makubwa yanayoweza kuikumba nchi na nchi ikasamabaratika kama ilivyosambaratika Somalia kipindi kile.
-JWTZ,Usalama na Polisi nyinyi washaurini serikali ya CCM kua mmechoka kutumika kisiasa kwa ajili ya kuwatisha Raia wasiokua na silaha wanaodai haki zao za kisiasa,
- washaurini serikali ya CCM kua mmechoka kuishi katika hali ya Tahadhari muda mwingi kwa hofu ya
kuogopa maandamano ambayo pengine yanasababishwa na mapungufu ya katiba,mapungufu ya Tume Ya Taifa ya Uchaguzi.
Washaurini kua mmechoka kulinda matokeo ya uchaguzi yasiyo halali,ambayo yanaweza kupelekea machafuko ya nchi.
Ambayo madhara yake mtajikuta mkikabiliana na wadogo zenu,kaka zenu,dada zenu,mama zenu,baba zenu,ndugu zenu wa damu huko mabarabarani wasio na silaha wala mafunzo ya kivita na mwisho wake mtaishia kuwaua.
Hii ni kazi ya Usalama na Jeshi la Wanchi.
POLISI nyie kazi yenu ni moja TU,kuwaambia serikali ya CCM ukweli kua ,mmechoka,
-mmechoka kuua wadogo zenu,kaka zenu,dada zenu,mama zenu na Watanzania wenzenu.
-mmechoka kuwapiga wapinzani wanapofanya mikutano Yao wakiwa hawana silaha yoyote.
-mmechoka kubebeshwa lawama za kuteka Watanzania,wenzenu,kuwatesa,kuwapiga na kuwapoteza wakati wakidai haki zao za kisiasa.
-kuishi kwa kulinda barabarani kuzuia maandamano
Enyi ndugu zetu wa damu mlio katika Vyombo hivyo nilivyovitaja hapo juu.
Hebu niambieni ni nani kati yenu ambae hakupoteza hata mtu mmoja kutoka katika ama famialia ama jirani katika mauaji ya MO 29?.
Enyi Usalama wa Taifa na JWTZ mnaotoka upande wa Zanzibar,mnayo nafasi kubwa ya kushauri mabadiliko ya katiba mapema kwa faida ya watu wetu wa pande zote mbili za Muungano,msifurahie zamu ya uongozi kua kiongozi Mkuu anatoka Zanzibar,kumbuka hii ni furaha ya muda TU.
Shaurini mabadiliko ya katiba Leo kwa sababu uongozi huu hautakuwepo milele.
Kumbukeni anaweza kuja RAIS chizi kutoka bara akaamua kuwatesa na nyie.Nyini mnayo nafasi ya kushauri mageuzi ya Usawa kitaifa.
Muungano huu ukivunjika kwa hasira za wananchi kabla ya katiba mpya kupatikana ni nyinyi Wazanzibari ndio mtakaoathirika na kuuumia zaidi,kuliko watanganyika.Chukueni hii.
Enyi Usalama wa Taifa na JWTZ kutoka bara shaurini mabadiliko ya kikatiba Leo Kwa ajili ya kuiokoa Tanzania,huko tunakoenda Watu watakuja kuumizana sana,mtapoteza watoto,wenu,ndugu zenu na majirani zenu kwa idadi kubwa kuliko ya MO29.
Tulisema haya mkatudharau lkn hatimae yalitooea Tanzania kwa mara ya kwanza.
Hebu fikirieni uchaguzi Mkuu utakaofuata mwaka wowote ule, je utakua na Hali Gani?
Nashauri kama Mtanzania mwenye mapenzi na nchi yangu na mwenye hofu ya Mungu.
Nashauri kwa uwoga mkubwa kutokana na yake yaliyotokea 2025.
Huu ni ushauri TU ndugu zangu hii ni nchi yangu Mimi Sina pa kukimbilia.
Natamani sana tuishi kwa amani bila chuki ya Uzanzibari wala Utanganyika,bila U CCM wala Upinzani,bila Uislam wala Ukristu.
Hapa tulipofikia nchi imeshakorogeka.
Huku makamu wa RAIS anajiuzulu kwa kutoelewana na mkubwa wake ,
Huku Tundu Lisu ameshitakiwa kwa uhaini,
Huku Mwalimu ameshitakiwa kwa ugaidi,
Huku kanisa linatuhumiwa kwa uchochezi,
Huku waislamu wanashutumiwa kwa kupendelewa
Huku Wapinzani wanakatazwa kufanya siasa,
Huku GenZ wanauwawa kwa kudai haki zao.
Nawaomba ndugu zangu pelekeni ushauri mkiwa mmekaza sura kuonesha nchi imekorogeka.
Nyie watawaelewa.
Iokoeni nchi hii.