Usalama wa Taifa, JWTZ na Polisi mnatukosea sana Watanzania

Director wa TISS unataka apige kelele kama Heche?
 
Unajua ni Kwa Nini wananchi hua wanaamua kuandamana kwa nguvu na kufanya vurugu?
Ni kwa sababu serikali hua haitaki wananchi hata waandamane kwa amani TU.

Na hii ni kwa sababu serikali ya CCM hua haitaki jumuiya ya kimataifa Ione wananchi wengi Kwa maelfu wameandamana au wamekusanyika kudai haki Yao Fulani.

Serikali hua inataka jumuiya ya kimataifa Ione kua, Tanzania mambo ni shwari hakuna shida zozote.
Hii sio kwa wananchi TU,hii hawataki iqe kwa Wana vyuo,wafanyakazi,wafabyabiashara n.k.
Maandamano ambayo serikali hua inayakubali ni ya kuunga mkono hotuba au hatua za kiongozi Fulani wa serikali.
Sasa wananchi wakiwa na madai Yao,wakitaka kuonesha hisia zao kwa maanadamno ya amani ambayo kikatiba yanaruhusiwa,hapo ndipo utasikia kauli za vitisho kutoka serikalini na viongozi wa polisi wakianza kutisha watu.hapo ndipo wananchi nao hujibu kwa jeuri kua tutaandamana kwa njia yoyote Ile,
Mwisho wa siku ni vurugu TU.
 
Zote hizo ni idara za chama kinachokufa kilichoachana na wananchi siku nyingi.
 
Hakuna mtanganyika yoyote asietaka Muungano popote,isipokua Watu wanailalamikia Muundo wa Muungano,na hiyo sio kosa maana hata Zanzibar nao Wana malalamiko Yao ya muda mrefu juu ya Muungano.
Kwa hiyo wote bara na visiwani Wana malalamiko Yao.
Hii ya kutaka sijui znz iwe mkoa wala isikutishe ni maoni ya watu wachache,na hii imeshawekwa vizuri kwenye Rasimu ya Jaji Warioba.
Nadhani rasimu ya Warioba inapendeleza serikali tatu.na hii ndio ilikuabaliwa na Watanzania wengi toka bara na visiwani.
Tume ya katiba ya Jaji Warioba ilizunguka nchi mzima pamoja na Znz wengi walitaka serikali tatu.
Chama chako Cha CCM ndio tatizo.
Mkiwndelea kukaza shingo nyingi CCM nchi itawavunjikia.
 
Wewe unataka haki ukiwa umejifunika na shuka lako Geto.
Toka nje...
Wewe zuzu Mimi sihubiri vurugu,wewe akili Yako inawaza vurugu na kuua TU.
Hivi Tutusa wewe nani aliekufundisha kudai haki ni vita?
Halafu watu hamnazo kama wewe ndio CCM inawapenda sana,na mtu kama wewe ukiomba kazi ya upolisi hukosi kwa sababu ya akili kama zako.
Ndio maana nchi inafeli hii.
 

Watanganyika mnataka huu uvamizi na ndio wacha yawafike. Sisi Wazanzibari tumesema zamani tokea wakati wa Mzee Karume , akaja Jumbe akaondolewa kwa kukataa huu uvamizi unaoitwa muungano. Kwa hivyo msilalamike mkipata raha hizo Za uvamizi ambazo mnazipenda , Endeleeni kufaidi matunda ya Muungano mnaoutaka . Kwenye hizo rasimu Za Warioba. Sisi tunataka nchi yetu hatutaki rasimu ya mtu yeyote. Kaunganeni na Kenya , Uganda au Burundi hata Zambia pia maana mlisaidia kuleta figisufigisu hivi majuzi
 
Director wa TISS unataka apige kelele kama Heche?
Kwa akili hizi zako,halafu mtu kama wewe ndio upate kazi serikalini sioni kama nchi hii itatoka Kwenye tope hili ilipozama.
Mtu kama wewe Huna msaada wowote katika Taifa hili zaidi ya uchawa TU.
 
Aisee kumbe naongea na mtu mwenye mawazo ya ajabu.

Kwani Samia atatawala milele?

Je ataipa Zanzibar uhuru wake?
Mbona una mawazo ya kitoto sana?

Maana Kwa katiba hii ya kijinga inataka raisi akiwa mtanganyika makamu anakua mzanzibari.

Kwa hiyo mwaka 2030 atakuja. RAIS mtanganyika makamu mzanzibari Sasa huoni bado haikusaidii kitu wewe?
Ndio maana nakuambia omba katiba mpya kwa manufaa ya Tanzania mzima.
 
Sema Usalama wa Genge
 
Viongozi wanaposhiriki kuua wananchi na sometime kuwalawiti, na tena wanapokataa kabisa kuwajibika kwa mauaji wanayoyafanya na wanapofuja kodi za wananchi kwa kununua magari ya kifahari mabently, gwagon, royce royce, na kutorosha pesa ng'ambo, wananch wakichoka na kuchukua hatua je utawalaum? Je wananchi wakae kimya kisa wanatunza amani? amani ya kuwatunza viongozi wezi walawiti hiyo ni amani?
 
Hoja yako ina upande wa kutafakari sana. Mara nyingi mvutano kati ya wananchi na vyombo vya dola huongezeka pale ambapo pande zote zinashindwa kupata nafasi ya kusikilizana kwa utulivu.

Hata hivyo, ni muhimu kutenganisha haki ya kufanya maandamano ya amani na vitendo vya vurugu. Wananchi wanapaswa kuwa na nafasi ya kueleza malalamiko na madai yao kwa njia za kisheria na za amani, huku mamlaka nazo zikitakiwa kuhakikisha usalama bila kutumia nguvu kupita kiasi.

Kuzuia kabisa watu kujieleza kunaweza kuongeza hasira na msuguano, lakini pia kurusha mawe, kuharibu mali au kuwadhuru watu siyo suluhisho. Njia bora ni serikali na wananchi kujenga mazingira ya mazungumzo, kuheshimu sheria na kusikiliza tofauti za maoni.

Demokrasia yenye afya haimaanishi kila mtu anakubaliana na serikali; inamaanisha hata wale wenye malalamiko wanapata nafasi salama ya kuyatoa. Mazungumzo na kuheshimiana ni bora kuliko vitisho na vurugu.
 
Ninaelewa hasira na maumivu yaliyomo kwenye hoja hii. Hakuna amani ya kweli pale ambapo kuna tuhuma nzito za mauaji, ubakaji au ulawiti, ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za umma, halafu wahusika hawawajibishwi.

Lakini pia, wananchi wanapodai haki zao hawapaswi kulazimishwa kuchagua kati ya kunyamaza au kuingia kwenye vurugu. Kuna haki ya kudai uwajibikaji, haki, uchunguzi huru na matumizi sahihi ya kodi za wananchi.

Amani ya kweli si ukimya wa wananchi wanaoogopa kusema. Amani ya kweli inajengwa kwa haki, uwajibikaji, kusikilizwa kwa wananchi na sheria kutumika sawa kwa kila mtu.

Kwa hiyo, wananchi hawapaswi kukaa kimya mbele ya uovu au tuhuma nzito; lakini mapambano ya kudai haki yafanyike kwa njia zinazolinda maisha ya watu wasio na hatia na kusukuma uwajibikaji wa kweli. Serikali nayo ina wajibu mkubwa wa kusikiliza wananchi na kuchunguza kila tuhuma nzito kwa uwazi.

Kwa kifupi: amani bila haki huwa ni utulivu wa muda; haki na uwajibikaji ndiyo msingi wa amani ya kudumu.
 
Hebu fikirieni uchaguzi Mkuu utakaofuata mwaka wowote ule, je utakua na Hali Gani?

Nashauri kama Mtanzania mwenye mapenzi na nchi yangu na mwenye hofu ya Mungu.
 
Hivi vi Id vyenu vipya mbona vimekuwa vingi sana recently?

Mmejiunga kwa kazi maalumu?
 
Hivi vi Id vyenu vipya mbona vimekuwa vingi sana recently?

Mmejiunga kwa kazi maalumu?
😂 Hapana mkuu, hatujajiunga kwa kazi maalumu. Kila mtu ana sababu zake za kujiunga na kushiriki mijadala. Kama ID zimekuwa nyingi recently, labda ni bahati tu ya muda—ila tusihukumu watu kwa ID zao kabla ya kujua wanachokileta kwenye mjadala. Hoja ndiyo muhimu zaidi kuliko lini mtu amejiunga. 👍
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…