Inaendelea No 3,
Nilirudi Dar na babe wangu aliondoka kurudi kazini, ndio nikapata nafasi ya kumpigia simu Lily na kumwambia tukutane kwenye mgahawa flani upo town, alifurahi sana akasema kwanini nisiende kwake amenimiss and stuff nikamwambia nope, tunahitaji kuonana pale basi jioni kweli tukakutana, alionekana mchangamfu kupita maelezo hadi nilimshangaa nikajiuliza kanywa pombe lakini hapana hua hanywi pombe basi nikajisemea labda alinimiss sana, ilikua ngumu sana kumwambia kua nataka kukatisha usaliti wangu nilizunguka sana hatimae nikampasulia ukweli, alitulia tuliiii, aliniangalia usoni kama dakika 2 hivi akacheka kidogo kisha akasema niende nyumbani atanitafuta baada ya siku 5, akaongeza kua sio akili yangu ni hiyo vacation imenichengua akili, ila nitarudi kua normal after sometimes kisha akaondoka haraka nikama hakutaka nimuone akilia, niliganda pale nikimtafakari nikaona isiwe shida nikamblock tena nikarudi home, alipiga akakuta block lakini mimi naona kua alinitafuta,
Baada ya siku 5 nikapokea simu kwenye namba ngeni akajitambulisha ni yeye na angependa twende Bagamoyo amesha arrange kila kitu, nikamjibu politely kabisa nimetingwa na kazi hadi wakati mwingine, akasema basi walau nimuone hata dakika 5 nikamwambia sina muda nikakata simu, baada ya muda mlango ukagongwa kutoka nje ni kijana anayetufanyia usafi anasema kuna mgeni wangu getini mmh nikapata wasiwasi kidogo sababu kwanza hua sileti mtu nyumbani kwangu akiwemo Lily hakuwahi kupajua kwangu, pili kwa wanaopajua hawawezi kuja bila kunipigia simu, nikamwambia kijana anisindikize, nafika nje namkuta Lily amebadilika sana, nywele zake ndefu na nzuri kazinyoa sijui kiduku sijui kijogoo, yule msichana mrembo mwenye uso usio na hatia alibadilika na kua kwenye muonekano wa kiume, alichora tattoo kubwa mkononi yenye jina langu, nilishangaa hadi nilitaka kudondoka, akavunja ukimya wa mshangao wangu kwa kunisalimia na kunitaka radhi kwa kuja bila taarifa, hapo ndio aliponizindua na kumuuliza amefikaje pale, akasema alikua anapajua maana alinifatilia siku nyingi kujua ninapoishi na mara kadhaa alifika pale bila kuniambia, kiufupi mchepuko alikua ananispy kama nachepuka dah😄
Nikamwambia aondoke haraka na asinisumbue nina kazi nyingi, wakati nataka kuondoka akanishika mkono kwa nguvu niliona moto mkali kwenye macho yake yaliyojaa hasira, nikasema kwa nguvu NIACHEEEE yule kijana akaingilia kati na kumtaka aondoke mara moja, mimi nikakimbilia ndani na kuwaacha nje, akasema nitakusubiri hapa hapa hadi utakapoamua kuondoka na mimi, geti lilifungwa na yeye alibaki nje.....
Itaendelea