Inaendelea No 4,
Huo ndio ukawa mwanzo wa kuuona upande wa pili wa mrembo Lily, alifika hadi ofisini kwangu kila mtu akajua kua nilikua na mahusiano nae wakati mwanzo ilikua ni siri yetu kubwa, maneno yalikua mengi ofisini hadi nikatamani kuacha kazi,
Hofu yangu ilikua mpenzi wangu asijue maana ataumia sana pia itayumbisha mahusiano yetu,
Lily akawa mtu wa kuvuta bangi na pombe, akawa muhuni asiyeweza hata kutambulishika kwa watu, kila mtu aliyekutana nae alimuhadithia kuhusu mimi, hatimae miezi ikapotea bila kunirudisha akajenga chuki kali kwangu, akaanza kunitumia meseji za matusi, alikua akibadili namba kila leo baada ya kua namblock kila namba ngeni aliyotumia, akaanza kunitishia kuniua, nikawa nakuta getini nguo nyeupe zimefutiwa damu, mara getini kuchorwe matusi na jina langu nikashindwa kuvumilia nikaenda kushtaki polisi, akapigiwa simu anahitajika haraka kituoni kweli akaja, lakini nilimuomba askari wasimfunge bali wamuonye kwanza sababu huyo sio yeye ni mental issue amepata kweli alinielewa, basi alivyofika akazungumza nae na kumpiga mkwara akae mbali na mimi, kwangu asifike, akate mawasiliano na lolote litakalonitokea yeye ndie atawajibika, akaomba msamaha na kuahidi kubadilika tena kwa maandishi, wakati tunatoka kituoni niliambiwa nianze mie kuondoka akafatia yeye, nikiwa njiani akanitumia meseji "hii vita uliyoianzisha jiandae kushindwa" sikumjibu nikatulia, kumbuka yote hayo yanatokea sikumshirikisha mtu yoyote hata babe wangu, nilikua napambana mwenyewe, hata kazini nikapunguza kwenda nikawa nafanyia kazi zangu nyumbani zaidi,
Ulipita mwezi mmoja kimya sikupokea simu yake wala meseji yake, nikashukuru sana na kuhisi amebadilika,
Siku hiyo jioni naongea na babe wangu video call akanambia "ooh babe kuna mtu kanitumia picha yako upo na binti flani akasema nyie ni wapenzi na anao ushahidi wenu wote wa meseji na calls, akasema huyu mtu aliniomba urafiki a week ago na hana picha wala marafiki sikumpokea ndio katuma hiyo meseji na kusema nikireply tu ananitumia huo ushahidi mimi nimemblock" akanionesha hiyo picha kupitia simu yake nyingine alikua ni Lily na mimi tukiwa Znz, uzuri kipindi chote cha mahusiano na Lily nilikua nakwepa sana kupiga picha/video na kuwasiliana kwa meseji/voice, ilikua nampigia zaidi, na hiyo picha ilikua ni selfie ya kawaida sana ni ngumu kuwekea maneno, nikafarijika kuona babe wangu alimblock lakini nilijua angemtafuta tena kwa akaunti nyingine,
Nikawaza sanaaa nikaona labda nionane nae, nizungumze nae nijue namsaidia vipi ajitambue tena, nikampigia akapokea chap kwa bashasha akaniuliza umeachwa eeeh, nikamwambia nahitaji kuonana nae kesho nikachagua eneo la beach tuliokua tunapenda kwenda, akakubali.....
Itaendelea