Usaliti ulivyogharimu maisha ya watu niliowapenda

Usaliti ulivyogharimu maisha ya watu niliowapenda

Mapenzi ni mashenzi sana 😅😅😅siku nikawa namuota kwa kumuita majina hadi dada yangu akaniambia ntakupiga 😜😜😜unamuota kwa kipi cha maana alichonacho, ndo akili ikafunguka 😅😅😅
Hatari mapenzi matamu nyie acheni tuu
 
Inaendelea No 4,
Huo ndio ukawa mwanzo wa kuuona upande wa pili wa mrembo Lily, alifika hadi ofisini kwangu kila mtu akajua kua nilikua na mahusiano nae wakati mwanzo ilikua ni siri yetu kubwa, maneno yalikua mengi ofisini hadi nikatamani kuacha kazi,
Hofu yangu ilikua mpenzi wangu asijue maana ataumia sana pia itayumbisha mahusiano yetu,
Lily akawa mtu wa kuvuta bangi na pombe, akawa muhuni asiyeweza hata kutambulishika kwa watu, kila mtu aliyekutana nae alimuhadithia kuhusu mimi, hatimae miezi ikapotea bila kunirudisha akajenga chuki kali kwangu, akaanza kunitumia meseji za matusi, alikua akibadili namba kila leo baada ya kua namblock kila namba ngeni aliyotumia, akaanza kunitishia kuniua, nikawa nakuta getini nguo nyeupe zimefutiwa damu, mara getini kuchorwe matusi na jina langu nikashindwa kuvumilia nikaenda kushtaki polisi, akapigiwa simu anahitajika haraka kituoni kweli akaja, lakini nilimuomba askari wasimfunge bali wamuonye kwanza sababu huyo sio yeye ni mental issue amepata kweli alinielewa, basi alivyofika akazungumza nae na kumpiga mkwara akae mbali na mimi, kwangu asifike, akate mawasiliano na lolote litakalonitokea yeye ndie atawajibika, akaomba msamaha na kuahidi kubadilika tena kwa maandishi, wakati tunatoka kituoni niliambiwa nianze mie kuondoka akafatia yeye, nikiwa njiani akanitumia meseji "hii vita uliyoianzisha jiandae kushindwa" sikumjibu nikatulia, kumbuka yote hayo yanatokea sikumshirikisha mtu yoyote hata babe wangu, nilikua napambana mwenyewe, hata kazini nikapunguza kwenda nikawa nafanyia kazi zangu nyumbani zaidi,

Ulipita mwezi mmoja kimya sikupokea simu yake wala meseji yake, nikashukuru sana na kuhisi amebadilika,
Siku hiyo jioni naongea na babe wangu video call akanambia "ooh babe kuna mtu kanitumia picha yako upo na binti flani akasema nyie ni wapenzi na anao ushahidi wenu wote wa meseji na calls, akasema huyu mtu aliniomba urafiki a week ago na hana picha wala marafiki sikumpokea ndio katuma hiyo meseji na kusema nikireply tu ananitumia huo ushahidi mimi nimemblock" akanionesha hiyo picha kupitia simu yake nyingine alikua ni Lily na mimi tukiwa Znz, uzuri kipindi chote cha mahusiano na Lily nilikua nakwepa sana kupiga picha/video na kuwasiliana kwa meseji/voice, ilikua nampigia zaidi, na hiyo picha ilikua ni selfie ya kawaida sana ni ngumu kuwekea maneno, nikafarijika kuona babe wangu alimblock lakini nilijua angemtafuta tena kwa akaunti nyingine,
Nikawaza sanaaa nikaona labda nionane nae, nizungumze nae nijue namsaidia vipi ajitambue tena, nikampigia akapokea chap kwa bashasha akaniuliza umeachwa eeeh, nikamwambia nahitaji kuonana nae kesho nikachagua eneo la beach tuliokua tunapenda kwenda, akakubali.....

Itaendelea
 
Aliniambia mtu mwenyewe ana macho kama chura ndo wa kumuota. 😅😅😅 ndo nikaanza kumuangalia vzr na kumtoa moyoni 😅😅😅
Utaniua mbavu🤣🤣🤣Kiukweli ukiwa kwenye fatiki la kuachwa unatakiwa kuwa na ntu pembeni wa kumsagia kunguni ex wako...am sure baada kumuangalia vizuri ndio uligundua yale macho yake ni kama ya chura
 
🤣🤣🤣🤣haaa we kusemaje?niliachwa live bila chenga
Yaani hata sijui nisemeje ..........wakati mimi tendo la kuachwa nalipinga balaa sasa sijui nyie kwenu inakuaje?? Mi nishamchana najua kuoa sijui kutoa talaka kwanza huko zamani niliwaacha watoto wazuri walionipenda sana nikamuoa yeye sasa asilete ushubwada wake hata kidogo haachiki mtu..........nilighaili mpaka kwenda ughaibuni kisa &#^#^#^&#&# yake harafu arete ungese.......
 
Wakuu kwanza leo ndio nimejua kua nimetimiza miaka 10 jamii forum, mnipigie makofi tafadhaliiii🥳🥳🤣
Okay, nashare na ninyi hadithi hii ya kweli iliyonitokea mimi mwenyewe, hua naumia sana kila nikiwaza kwa ujinga wangu nilivyohatarisha mahusiano yangu na kuharibu maisha ya huyu binti,

Mwaka 2020, nilienda kwenye semina ya vijana juu ya uelewa wa Afya ya Akili, kulikua kuna taasisi nyingi zilialikwa ikiwemo na sisi, basi muda wa kupata chakula cha mchana nikamuona binti mmoja mrembo amekaa meza ya peke yake anakula taratiibu, akilini nikahisi anajitenga kwa hiyo nilibeba chakula changu na kuwaacha wenzangu wanaelekea kukaa meza nyingine nikaenda kukaa na yule binti, nilimsamlimia na kumuuliza kama ninaweza kukaa akanikaribisha kwa tabasamu zuri, basi tukaanza kupiga story za hapa na pale hadi tulipomaliza kula tukaagana na kila mmoja akarejea alipokaa awali, kiukweli mimi sikumtilia maanani tena,
Semina ilivyoisha wakati najiandaa kuondoka yule binti akaja mbio na kuniomba namba ya simu, nilisita kidogo akadai ana shida ya ushauri basi nikampa chap nikaondoka,
Nilivyofika home mida ya saa moja jioni sms ikaingia muhusika akajitambulisha anaitwa LILY (sio jina halisi) tulikutana kwenye semina hapo ndipo mawasiliano yalipoanza rasmi,

Nitajaribu kuifupisha maana sina kipaji cha uandishi,
Mimi na Lily tukawa marafiki sana, mimi nilimchukulia kama mdogo wangu (alikua chuo mwaka wa pili) huku yeye akitengeneza hisia za mapenzi kwangu licha ya kujua nipo kwenye mahusiano,

Siku moja akanipigia simu niende kwake alikua anaumwa sana, nakumbuka jioni baada ya kumaliza kazi nikanunua matunda na mazaga mengine nikaenda kumuona mdogo wangu mgonjwa, ilikua mara ya kwanza kufika kwake, alikua amepanga chumba master na jiko, alifurahi sana kuniona kila mara alisema hakuamini kama ningeenda, nakumbuka alivyoifakamia chocolate niliyomletea, anapenda sana chocolate, nilikaa kama masaa mawili nikaaga, akaniomba aoge kisha anisindikize japo nje tu, nikasema poa, alipotoka kuoga dah! hata sielewi ilikuaje nikajikuta namsaliti babe wangu 😭😭 pia nikanasa kwenye mtego mbaya sana ambao unanitesa hadi leo, just one mistake 🙌🏻.......

Mnisamehe siwezi kuandika yote hapa itakua ndefu sana itawaboa.

Itaendelea
Nasikia harufu ya kusuguana na kusagana hapa
 
Back
Top Bottom