Ushabiki wa siasa katika taasisi za soka: Wakati umewadia sasa kwa FIFA kushusha rungu lake kwa vilabu vya Yanga na Simba

Ushabiki wa siasa katika taasisi za soka: Wakati umewadia sasa kwa FIFA kushusha rungu lake kwa vilabu vya Yanga na Simba

Unajua maana ya mwenyekiti? Au unabwabwaja tu? Yeye ndiye alfa na omega. Leo akitoa mguu tu mtajikojolea mapajani. Aliwabeep tu kidogo kwamba anajihuzuru si mlimlamba miguu nyie nyie?
Mkuu kwahiyo unataka kusema Mo alikuwa sawa?
 
How FIFA Defines "Political" in Ban on "political...slogans, statements or images"

[https://static][https://static]

The rules of soccer are published in a document called The Laws of the Game. According to the Laws of the Game (2018/2019), Law 04, Section 5:


"Equipment must not have any political, religious or personal slogans, statements or images...For any offence the player and/or the team will be sanctioned by the competition organiser, national football association or by FIFA.”


"Whilst ‘religious’ and ‘personal’ are relatively easily defined,‘political’ is less clear but slogans, statements or images related to the following are not permitted:

any person(s), living or dead

any local, regional, national or international political party/organisation/group, etc.

any local, regional or national government or any of its departments, offices or functions

any organisation which is discriminatory

any organisation who [whose] aims / actions are likely to offend a notable number of people

any specific political act / event

"When commemorating a significant national or international event, the sensibilities of the opposing team (including its supporters) and the general public should be carefully considered."
Nimukukubali mkuu!
 
bMpaka sasa yeye ndio mmiliki, hakuna mwanachama hata mmoja aliyetoa japo kijiko kama sehemu ya hisa 51% za wanachama. Mo kaweka mezani 20B, jaribu kumpinga uone.
Je Mo alikuwa sahihi?

Usijaribu kuhalalisha haramu!
 
Ninyi ni hovyo tu, viongozi wenu walitangaza kususia Vodacom lakini baadae wakasema mtumie M-pesa kuchangia viongozi.... Sasa ni hovyo tu hamna msimamo
Busara ilitumika. Hata hapa ni onyo tu. Hawajasema watu wasusie. Usijaribu kuwachokoza chadema.
 
Mimi ni mpenzi mkubwa wa Simba Sports Club, lakini kwa upumbavu aliofanya Mo jana nimepunguza mapenzi yangu kwa Simba kwa 50%. Nimekereka sana huyu ponjoro kutuletea upuuzi wake wa kiccm.
 
Niseme tu binafsi jana nilikwazika sana tena mnoo, na wanasimba wengi sana na Watanzania tulikwazika.

Kitendo cha Mo Dewji kutumia platform ya michezo ambayo mashabiki wake tuna itikadi tofauti za kisiasa na kuanza kuwanadi wagombea wa CCM ni kitu cha hovyo sana.

Nimekitafsiri kama ubakaji wa ushabiki, maana kabla ya tukio hatukuambiwa kwamba kutakuwa kuna habari za kuwanadi wagombea wa CCM.

Wametusubiri tumeingia mule halafu wametupaka kinyesi na mambo yao ya CCM. Haikuwa sehemu yake ile, ni kutudharau wana Simba na watanzania, kutuchukulia kama wapumbavu.

Binafsi sio mtaalamu wa sheria, ila kama ikipendeza naomba wataalamu wa sheria, msilifumbie macho hili suala. Fanyeni hima hima, tulipeleke FIFA hili suala.

Please please wadau wote, hili suala lianzishiwe petition lifike FIFA. Inapaswa iwe mwisho wa upuuzi kama huu kwenye soka letu.

Hatuwezi kukubali, Mo Dewji lazima kuna consequences ya ulichokifanya jana. Haiwezi kupita kimya kimya.

Huu mwaka sasa basi, hakuna kitu kitapita bure bure.

Mmetuzoea vibaya wananchi. Sasa basi
 
Je Mo alikuwa sahihi?

Usijaribu kuhalalisha haramu!
Siongelei matamshi mkuu, naongelea umiliki wa timu. Kwa upande wa matamshi, timu ya mpira ni kama taasisi za kidini tu, zina waumini wenye itikadi tofauti. Nadhani umeelewa
 
Simba ni mali yake na familia yao, Azim Dewji, Kassim Dewji, sasa Mo Dewji hao ni ukoo mmoja kama vp njoo kwa wananchi ili usijione unadharauriwa na wenye mali yao.
 
Pambana upate pesa wewe, Mo ni level nyingine. Siasa za CDM na CCM zinawafanya vijana wa Tanzania muwe wajinga wajinga, nani aende FIFA kuongea huo upuuzi wako?, baada ya kufatilia mambo ya maana mnahangaika na vitu vilivyo nje ya uwezo wenu. Hamna wa kumfanya lolote Mo, sio Simba,TFF wala FIFA.
 
Kwani uwanjani mlilipa kiingilio hadi mnalalamika?

Mmeingia uwanjani bure kwa ufadhili wa mwanaccm Mo.....sasa kuna ubaya gani akiwaomba muisapoti CCM?

Bure gharama bwashee!
 
Pambana upate pesa wewe, Mo ni level nyingine. Siasa za CDM na CCM zinawafanya vijana wa Tanzania muwe wajinga wajinga, nani aende FIFA kuongea huo upuuzi wako?, baada ya kufatilia mambo ya maana mnahangaika na vitu vilivyo nje ya uwezo wenu. Hamna wa kumfanya lolote Mo, sio Simba,TFF wala FIFA.
Wewe hujui unachokiongea maana hata shule hukwenda. Hujui mamlaka ya FIFA wewe..

Hii mbungi imekuzidi uwezo. Kuwa mpole
 
Ukiwa masikini acha wenye pesa wajimwambafai.

Hilotamasha la simba day unafahamu limegharimu kiasi gani?

Wewe ni shabiki tu wa simba hufahamu biyo simba unayoishabikia imetengenezwa na nani.

Amlipaye mpiga zumari ndiye mchagua wimbo
 
Kwani uwanjani mlilipa kiingilio hadi mnalalamika?

Mmeingia uwanjani bure kwa ufadhili wa mwanaccm Mo.....sasa kuna ubaya gani akiwaomba muisapoti CCM?

Bure gharama bwashee!
Hiyo bado sio tiketi ya kutuletea siasa kwenye mpira. Uzuri sheria za FIFA zipo wazi.

Ikiwa hili likisimamiwa vizur, tunaweza kuja kulaumiana baadae.

Ni makosa kuweka siasa na michezo kwenye kapu moja
 
Ukiwa masikini acha wenye pesa wajimwambafai.

Hilotamasha la simba day unafahamu limegharimu kiasi gani?

Wewe ni shabiki tu wa simba hufahamu biyo simba unayoishabikia imetengenezwa na nani.

Amlipaye mpiga zumari ndiye mchagua wimbo
Kwahiyo CCM ndo wamefadhili Simba day? Acha kujitoa ufahamu
 
Back
Top Bottom