Niseme tu binafsi jana nilikwazika sana tena mnoo, na wanasimba wengi sana na Watanzania tulikwazika.
Kitendo cha Mo Dewji kutumia platform ya michezo ambayo mashabiki wake tuna itikadi tofauti za kisiasa na kuanza kuwanadi wagombea wa CCM ni kitu cha hovyo sana.
Nimekitafsiri kama ubakaji wa ushabiki, maana kabla ya tukio hatukuambiwa kwamba kutakuwa kuna habari za kuwanadi wagombea wa CCM.
Wametusubiri tumeingia mule halafu wametupaka kinyesi na mambo yao ya CCM. Haikuwa sehemu yake ile, ni kutudharau wana Simba na watanzania, kutuchukulia kama wapumbavu.
Binafsi sio mtaalamu wa sheria, ila kama ikipendeza naomba wataalamu wa sheria, msilifumbie macho hili suala. Fanyeni hima hima, tulipeleke FIFA hili suala.
Please please wadau wote, hili suala lianzishiwe petition lifike FIFA. Inapaswa iwe mwisho wa upuuzi kama huu kwenye soka letu.
Hatuwezi kukubali, Mo Dewji lazima kuna consequences ya ulichokifanya jana. Haiwezi kupita kimya kimya.
Huu mwaka sasa basi, hakuna kitu kitapita bure bure.
Mmetuzoea vibaya wananchi. Sasa basi