johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
ngoja tuwaite FIFA waje.... ndiposa mtajua hizo % ni shubiri au asali!Yanga ni mali ya CCM kwa 100%
Simba ni mali ya CCM kwa 51%
Huwezi kutenganisha vilabu hivi na CCM.
Maendeleo hayana vyama!
Fifa ni wapiga dili tu hawana lolote wale!ngoja tuwaite FIFA waje.... ndiposa mtajua hizo % ni shubiri au asali!
ushasahau FIFA walishatufungiaga huko nyuma pivyu vilitubana?Fifa ni wapiga dili tu hawana lolote wale!
Jaribu unaweza ukashinda kesi yako na umbumbu wako. Tatizo lako umekuwa kipofu unaona tu unakopelekwa hata kama ni shimo la moto.Kweli kabisa wadau wafikishe haya malalamiko kwa FIFA wapewe adhabu zao..
Kwanini tusifanye petition ili habar iwafikie FIFA?
Nilitoa uzi jana kushauri hilo.. wanasheria mpo wapi?
Hawakutugungia kwa sababu za kumpigia kampeni mmiliki wa timu!ushasahau FIFA walishatufungiaga huko nyuma pivyu vilitubana?
ngoja tupeleke petition yetu halafu tuone kifuatacho.
baada ya kifuatacho nitakuita mezani tusemezane!
sawa. tutasemezana baada ya feedback ya petition.Hawakutugungia kwa sababu za kumpigia kampeni mmiliki wa timu!
hao wanaoshabikia chama dola ni kujipendekeza kwa ajili ya maslahi binafsi na si kukipenda chama.Duh , aisee nyie jamaa kweli ni fungu la kukosa yaani mmebanwa kila mahali, sasa hata kwenye football pia nako hola, hamtakiwi, hamjishtukii tu kwamba kuna kitu hakiko sawa, wakati mwingine ni vizuri kujitathmini pia inawezekana kuna mahali hamko sawa, haiwezekani kila mahali Watanzania tuwakatae, ...
ndiyo ukweli wenyeweMhindi alitaka kunyang'anywa mashamba yake ya mkonge kule Mombo hivyo anasifia ili asisumbuliwe.
ajabu!NI kweli Simba tulikosea kuingiza siasa kwenye mpira, ila sasa mikia mbona kama ndio mnatamani sana tupigwe ban
sawasawa kabisa!Nafikiri ni wakati muafaka timu ya Simba na Mo washitakiwe FIFA na wapate adhabu stahiki ili iwe fundisho kwa team zingine, hebu wanasheria na wana Yanga kuweni kitu kimoja ktk hili ili watu hawa waadhibiwe hata kufungiwa maisha
Lazima tuusemendiyo ukweli wenyewe
ni rungu tu hakuna namna!Wanasheria wanatuangusha sana.. hii issue rahisi sana maana ushahidi upo wa wazi.
FIFA washushe rungu lao maana kuna watu wamejisahau
Mkuu nakuunga Mkono kwa hili. Sisi wanachama wa SIMBA tumeumizwa saana na huu upuuzi wa huyu gabachori na amekuwa mbishi saana. Changamoto imekuwa wapi pa kuanzia ila nakuhakikishia tupo tayari kukuunga mkono wewe tuongoze. TuwasilianeTuwekane sawa.
Shirikisho la soka duniani (FIFA) katika moja ya kanuni zake limetoa katazo la siasa kuingizwa katika masuala ya mpira wa miguu (soka).
Katika miaka ya hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia hapa Tanzania vilabu vya Yanga na Simba vikijinasibisha na chama dola CCM. Na hili nimekuwa likifanyika kwa uwazi kabisa bila kificho kupitia watu wenye dhamana ndani ya vilabu hivi.
Mfano ni hapa juzi tu tumemsikia na kumuona mwekezaji katika klabu ya Simba akifanya siasa za wazi kabisa kumpendelea mmoja wa wagombea urais October 2020 mbele ya kadamnasi ya maelfu ya Watanzania wenye itikadi tofauti tofauti za kisiasa. Hii ni siasa ambayo FIFA imeikataza katika soka.
Kwa mnaokumbuka, mwaka 2015 kabla ya uchaguzi pale katika klabu ya Yanga kulikuwa na mabango yamewekwa yaliyosomeka "Chagua Magufuli". Hii ni siasa na katazo la FIFA linahusu.
Ipo mifano mingine mingi ya matukio ya kisiasa kuvihusu vilabu hivi. Sasa ifike mahali tuseme "HAPANA, IMETOSHA!".
Natoa rai kwa wafuasi wa vilabu hivi msiishie tu kulalamika kwenye mitandao kuhusu ubaradhuli huu bali chukueni hatua sasa. Hawa viongozi wanaojihusisha na siasa wawajibishwe wao binafsi, na hili linawezekana kwa kuwasilisha malalamiko yenu rasmi FIFA.
Vinginevyo mnatuachia sisi tusiokuwa wafuasi wa vilabu hivi vyenu kuviripoti FIFA vilabu vyenyewe, kitu ambacho kinaweza kupelekea vilabu kufungiwa kwa kujihusisha na masuala ya siasa na hivyo kuwanyima uhondo wafuasi wake.
TUMECHOKA!
The ball is in your court now. Move it, and FAST!