Ushabiki wa Simba na Yanga umewapumbaza Watanganyika

Mimi niko vizuri 😅🙏
Huwa napenda kuwakumbusha ndugu zetu kwamba upigaji mkubwa mkubwa ni dhambi kubwa na ni Dhulma kubwa maana unasababisha maisha ya watu wengi kuwa ya shida kwa sababu ya ughali wa maisha kutokana na vitu kupanda bei kufidia zile ambazo wanaoitwa wajanja kukwapua zile zilizotakiwa ziende kwenye maendeleo ya Wananchi !!

Mifano ni mingi ila waliozowea vya kunyonga vya kuchinja hawaviwezi !!
Watasema tunawaonea wivu tu 😅

Ndio maana tunawakumbusha kwamba hata wakichuma vingi kiasi gani bado ufunguo wa mtu kuwa na furaha utabaki kwa Mungu pekee !

Ndio maana wapigaji wanaishi kwa stress za kila aina na wale wanaoishi kwa vipato vyao japo vidogo vya halali wanafurahia maisha yao kwa kuzipenda Simba na Yanga. 😅🤣

Na malipo ni hapa hapa Duniani 🙏🙌👍🤠
 
Paragraph yako ya mwisho imebeba ujumbe mzito sana na inawahusu pande zote mbili za shilingi 🙌👍🙏🙏
 
Mo Dewji na wawekezaji wengine wamepewa mpaka wa uwekezaji wa kumiliki asilimia 49 na 51 inakuwa ni mali ya wananchi.

Wanatambua kuwa anayemiliki mpira wa miguu anaweza hata kuipindua serikali kwa wingi wa wanaomuunga mkono.

Masuala ya kiserikali yanakwenda vizuri kama kawaida na ya michezo yanaenda vyema pia.
 
Na wewe uliyejua kuwa haya yote yamefanyika umesaidia nini katika kuyaweka vizuri? Kama hujafanya lolote, una tofauti na ambaye hajui?
 
Sasa nishagundua wewe ni Mshamba haswaaaaa.
Tena limbukeni.
Umeona Yanga na Simba faragha za watu!
We uko tayari hata kuolewa ikifungwa timu.
 
Na wewe uliyejua kuwa haya yote yamefanyika umesaidia nini katika kuyaweka vizuri? Kama hujafanya lolote, una tofauti na ambaye hajui?
Wewe kusoma tayari nimefanya kazi kubwa.
 
Wajinga wakinga wapo Benjamin Mkapa Stadium 🏟.

Wanawasikiliza wanamziki ambao wanaingiza fedha.
 
Natazama nyomi Mkapa muda huu halafu January mtaomba mjengewe matundu ya choo.
 
Sasa nishagundua wewe ni Mshamba haswaaaaa.
Tena limbukeni.
Umeona Yanga na Simba faragha za watu!
We uko tayari hata kuolewa ikifungwa timu.
Mjinga wewe, unatakiwa uelewe kwamba mashabiki wa mpira ni wengi kuliko watu wenye kadi za vyama vya siasa, Mpira ni biashara kubwa sana na ina pesa nyingi ikiajiri mamilioni ya watu.

Wapumbavu kama wewe mpo kila mahali katika kila sekta, hamuelewi upana wa michezo upo vipi mnaishia kufanya maamuzi yanayopitwa na wakati na kuwakosesha mamilioni ya watu riziki zao.
 
Natazama nyomi Mkapa muda huu halafu January mtaomba mjengewe matundu ya choo.
Kuomba kujengewa matundu ya vyoo hakujaanza jana wala juzi. Ni hulka binafsi zetu.

Michezo ni sekta pana sana yenye kuweza kupunguza tatizo la ajira iwapo itasimamiwa kiuweledi.
 
Kweli ushamba umekujaa.
Kuwa shabiki wa soka sio tatizo. Tatizo linaanzia pale ambapo hata washamba kama wewe mnashabikia Yanga na Simba badala ya kushabikia timu ya kijijini kwenu, huo ni ulimbukeni.
Yanga na Simba ni za watoto wa Kariakoo, sasa limbukeni wewe inakuhuu
 
Ushamba unao wewe unaodhani sisi tunaoshabikia timu za kariakoo tunafaidi sana. Wewe umesaidia vipi timu ya kijiji kwenu?.

Nimekulia mtaa wa shaban robert nyumbani kwetu ni pale walipojenga ule ukumbi wa JNCC miaka ya nyuma palikuwa na veterenary pembeni yake ndio nilipoishi kuanzia mwaka 1978.

Historia za maisha yetu zinatufanya tuzipende Simba na Yanga. Mpuuzi ni wewe unayelaumu watu wanaopenda mpira kana kwamba ndio waliokuletea huo umaskini wako.
 
Each and everything happens for a reason
Afu usitake tuwe kama kenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…