Ushabiki wa Simba na Yanga umewapumbaza Watanganyika

Ushabiki wa Simba na Yanga umewapumbaza Watanganyika

Wacha watu wa enjoy maisha hasira za nini? wewe unayetaka fujo mbona option nyingi, iko Kenya, Burundi hata Congo kaandamane tu fanya fujo wa Tanzania watu wanapenda starehe na amani.
Nadhani hujaelewa msingi wa joja zangu.
 
Mfumo wa maisha ni mpana sana!
Tusilazimishane wote kuwaza siasa na uchumi pekee.
Mambo ya kijamii tunayapenda pia
 
Tunatengeneza taifa la hovyo sana. Na viongozi uchwara tayari wameshaijua hiyo code, wanatembea nayo.. Tanganyika yetu 😭
 
Mfumo wa maisha ni mpana sana!
Tusilazimishane wote kuwaza siasa na uchumi pekee.
Mambo ya kijamii tunayapenda pia
Neno maisha tu kwa karne ya 21 tafsiri yake ni Siasa na uchumi, Saizi hata ukienda kuoga mtoni unakatazwa, unaambiwa unaharibu vyanzo vya maji 😀
 
Kwa nchi yetu ushabiki wa Yanga na Simba ni wa miaka na miaka!
Sema kwa kizazi hiki umepitiliza mno mpaka inaboa!
Miaka yote Usimba na Uyanga unatumika kisiasa
Mungu anawaona na atatenda na hawatakuwa na peace of mind maisha yao yote kama hawatafanya vile vinavyostahili kutendewa Wananchi wa Nchi hii na mali Asili zao walizobarikiwa na Mungu wa Mbinguni !!

They will have to bear it in their minds kwamba Mungu yupo na anawaona na pia anawasikia !!
Kumuachia MUNGU masuala kama haya ni kumkosea sana. Ingekuwa anashughulika nayo angeshatatua ya Israel na Palestine.

People caused problems are well solved by people themselves!
 
Nadhani hujaelewa msingi wa joja zangu.
Nimeelewa vizuri ila lazima ujue pia sio kila mtu ni mshabiki wa siasa na hii hoja ya kila siku bandari imeuzwa ni hoja dhaifu na wazi ushabiki wa upande fulani. Watu wanajuwa madhaifu ya serikali na chama tawala lakini pia wanajuwa vizuri ni bora ya hawa kuliko wale. Ndio maana nimesema wa Tanzania sio watu wanaopenda fujo ni hulka yetu, hatufanani na nchi yoyote Africa hapa hawa majirani zetu tu hatufanani nao.

Ni vizuri tukapishana kauli lakini huwa sipendi mimi binafsi hizi kauli za kuchochea mtafuruku. Tuitunze amani kwa gharama yoyote mengine tutaelewena tu.
 
Heshima sana wanajamvi,

Katika miaka ya karibuni ( labda 2020 - 2024) umekuwepo ushabiki mkubwa wa mpira baina ya Club mbili kubwa Simba Na Dar Young Africa.

Ushabiki wa mpira,ngoma,kwaya,sarakasi,sana saana nyinginezo si jambo baya hasa katika kuburudisha na kuboresha afya ya akili.

Nimeanza kubaini kupitia ushabiki wa Simba na Yanga limezaliwa tatizo lingine jipya,Vijana hawajui au hawataki kufahamu kuhusu nchi yao.
Hawajui Bandari zimeuzwa kwa Waarabu.
Hawajui Uwanja wa ndege wa Kimatiafa Kilimanjaro umeuzwa.
Hawajui Ngorngoro imeuzwa kwa waarabu.
Hawajui Zanzibar inaitawala Tanganyika (Tanzania Bara)
Hawajui Ardhi ya nchi yao Tanganyika inauzwa kwa wageni.
Hawajui lolote kuhusu nchi yao.
Wakilala wakiamka Simba day,Yanga day huu upuuzi wa hizi team umewadumaza vijana wengi wa kiTanganyika badala ya kufikiri kuhusu nchi yao inavyoporwa kama wenzao wa Kenya wao wanakuambia "UBAYA UBWELA" siku wakistuka watakuta kila kitu kimeuzwa.

Ngongo kwasasa Gairo.
Suluhisho nini kifanyike mkuu manake ni hatari kwa kweli.

Mimi ninapenda sana mpira hata kuucheza naujua ila sina ushabiki wa namna hiyo, kuna wakati huwa nashangaa sana huu ushabiki uliopitiliza ila najisemea hatuwezi kufanana wote.
 
Kwanza hata huwa siwaelewi wanazungumzia nini.

"Oyaa mwanangu jana simba wamekiwasha"........ "oyaa mwaka huu Yanga noma"

Ndo nini yaani, mimi mbona hata sielewagi wanachoongea?? Hata huo mpira wenyewe nikijaribu kuangalia naona makorokocho matupu.

Nimejitahidi kuwaelewa wanazungumziaga nini lakini nashindwa! I have used all my intellectual power trying to understand their rubbish but i DON'T seem to get it.

Wako kama MAZOMBI fulani yenye mabetri kichwani...

Cc: DR Mambo Jambo Nyani Ngabu min -me NAMBA MOJA AJAYE NCHINI mshamba_mwingine Poor Brain FaizaFoxy Kiranga Lamomy Extrovert dronedrake Mzee wa kupambania Mufti kuku The Infinity
Mpira ni cover kubwa sana na eneo kuu la propaganda Duniani!

Mfano Leo siku ya wananchi promo ikapigwa ya kutosha wakati nyuma ya pazia Kuna mtu mkubwa anashughulikiwa aondoke duniani!!!!?Hakuna yeyote atakaejua Hadi mission imekamilika tunakuja kushangaa kaenda!!

Jana siku ya simba unashangaa Raise anaongelea kwenye simu na Leo nadhani itakua hivyo hivyo!!

Huku kwetu mpira ni siasa hata huko majuu ni hivyo hivyo japo imejificha sana!!

Mpira ni ki Chaka cha wakubwa kutakatisha pesa na hadaa ya uchafu uliopo nyuma ya pazia Kwa sasa!
 
Wewe mleda mada na wanaokuunga mkono ni wazi mnachuki na waarabu na si vinginevyo,uwekezaji ktk madini wametawala wazungu lakini ktk mifano yako umeishia kulalamikia sehemu walizowekeza waarabu tu na kusema waneuziwa.acha chuki binafsi kwanza nawe utaupenda tu mpira hasa huu wa Tanzania unaokuwa kwa kasi.na mifano yenu yakufananisha uchumi wa tanzania na kenya hebu fuatilieni taarifa sio kupiga porojo tu!,ktk nchi za ukanda huu kiuchumi kenya anaihofia tanzania tu ndio iliyomuashia taa nyekundu.kuhusu mpira na vyombo vya habari, ilewa hiyo ndio biashara yenye kuwapa matangazo mengi ndio maana wanaipa kipao Mbele.tambua kuna mtajiri wengi wameona fursa ktk soka.mfano biashara ya jezi na hawa bet ving'amuzi kama azam nawengine wengi ndio maana unaona inapewa kipaumbele kuhusu serikali inanufaika na kodi nyingi zilizopo ktk soka
 
Kuna muda natamani bora hata nchi ingeongozwa na jeshi
 
Tangu kitambo sana. Na matapeli ya ccm yanatumia umbumbumbu wa mashabiki wa soka kuwa-brain wash zaidi.
Watu wana matatizo chungu mbovu lakini wapo radhi kuandamana kupinga madudu ndani ya timu zao kulikoni kupinga maovu kwenye siasa za Taifa!
Ni ajabu na kweli
 
Huna mamlaka na waacheni vijana watulize akili zao kwenye ushabiki wa mpira, kero ni nyingi na wakiendelea kuzifikiria tutatengeneza kundi kubwa la wenda wazimu huko mitaani.

Hawana pesa, hawana michongo ya kuingiza pato na bado wakiushabikia mpira mnakuja na makelele yetu ya kuwalalamikia wakati hamna uwezo wowote wa kuwapunguzia machungu yao.

Acheni upuuzi huu.
Kweli!
Na hiyo ndo furaha ya CCM. Wanajua kabisa kina Mbowe, Lisu, Zito hawana uwezo wa kufanya mageuzi wao bila vijana. CCM imewashika vijana papaya, hawawezi tena kuwasikiza kina Zito. Wao wakilala wakiamka ni Yanga, Simba, Kubeti, Diamond na Wema baaaaas
 
Majuzi kulikuwa na mashindano ya pikipiki kwenye viwanja vya Laki laki Arusha... Yaani ilikuwa ni party ya vijana wa mihadarati, makahaba na chokoraa... Yaani uhuru ulipitiliza!
Nadhani ni strategy ya Makonda kuwa-win vijana wa Chuga!
 
Kweli!
Na hiyo ndo furaha ya CCM. Wanajua kabisa kina Mbowe, Lisu, Zito hawana uwezo wa kufanya mageuzi wao bila vijana. CCM imewashika vijana papaya, hawawezi tena kuwasikiza kina Zito. Wao wakilala wakiamka ni Yanga, Simba, Kubeti, Diamond na Wema baaaaas
Wanaoupenda mpira TZ ni zaidii ya milioni 30 kati ya milioni 60.

Wanaopiga kura na kujishughulisha na siasa za uchaguzi hawazidi milioni 10 nchi nzima.

Kuna zaidi ya vijana wenye nguvu za kufanya kazi milioni 20 wasiojua Mbowe anafanana vipi na maisha yao yanaendelea bila ya kufuatilia ulaghai wa wanasiasa.

Jifunze kuheshimu faragha za watu kuliko kujifanya wewe ni mpangaji wa maisha yao ya kila siku. Kwenda Uwanjani wanajua pesa wamepata wapi na hawana haja ya kuja kukuomba wewe uwaruhusu wafuatilie mpira!.

Achana na hizi akili za kinoko, za kishamba.
 
Heshima sana wanajamvi,

Katika miaka ya karibuni ( labda 2020 - 2024) umekuwepo ushabiki mkubwa wa mpira baina ya Club mbili kubwa Simba Na Dar Young Africa.

Ushabiki wa mpira,ngoma,kwaya,sarakasi,sana saana nyinginezo si jambo baya hasa katika kuburudisha na kuboresha afya ya akili.

Nimeanza kubaini kupitia ushabiki wa Simba na Yanga limezaliwa tatizo lingine jipya,Vijana hawajui au hawataki kufahamu kuhusu nchi yao.
Hawajui Bandari zimeuzwa kwa Waarabu.
Hawajui Uwanja wa ndege wa Kimatiafa Kilimanjaro umeuzwa.
Hawajui Ngorngoro imeuzwa kwa waarabu.
Hawajui Zanzibar inaitawala Tanganyika (Tanzania Bara)
Hawajui Ardhi ya nchi yao Tanganyika inauzwa kwa wageni.
Hawajui lolote kuhusu nchi yao.
Wakilala wakiamka Simba day,Yanga day huu upuuzi wa hizi team umewadumaza vijana wengi wa kiTanganyika badala ya kufikiri kuhusu nchi yao inavyoporwa kama wenzao wa Kenya wao wanakuambia "UBAYA UBWELA" siku wakistuka watakuta kila kitu kimeuzwa.

Ngongo kwasasa Gairo.
Ww ambae hujapumzika umemsaidia nn taifa
 
Simba na Yanga ni Ugonjwa mkubwa sana kwa sasa...unaweza kuweza Tozo yeyote wasisikie maumivu kwa sababu ya mpira...
Nmeongia dar toka juzi nkijuwa jana naonana na mtu mitaa ta tabata anipe vifaa fulani,kumpigia asubuhi aka niambie kaenda simba day leo namcheki tena ananiambia kafunga ofisi wenzake wameenda siku ya mwananchi....nkaambia nyie ni maf@l kbsa
Nikajiongeza nkaenda huku nyerere Road ofisi ya mdosi mmoja nkamaliza chap

Ova
 
Wanaoupenda mpira TZ ni zaidii ya milioni 30 kati ya milioni 60.

Wanaopiga kura na kujishughulisha na siasa za uchaguzi hawazidi milioni 10 nchi nzima.

Kuna zaidi ya vijana wenye nguvu za kufanya kazi milioni 20 wasiojua Mbowe anafanana vipi na maisha yao yanaendelea bila ya kufuatilia ulaghai wa wanasiasa.

Jifunze kuheshimu faragha za watu kuliko kujifanya wewe ni mpangaji wa maisha yao ya kila siku. Kwenda Uwanjani wanajua pesa wamepata wapi na hawana haja ya kuja kukuomba wewe uwaruhusu wafuatilie mpira!.

Achana na hizi akili za kinoko, za kishamba.
Sawa,leo nendeni mkatambulishwe azz k na mobeto

Ova
 
Heshima sana wanajamvi,

Katika miaka ya karibuni ( labda 2020 - 2024) umekuwepo ushabiki mkubwa wa mpira baina ya Club mbili kubwa Simba Na Dar Young Africa.

Ushabiki wa mpira,ngoma,kwaya,sarakasi,sana saana nyinginezo si jambo baya hasa katika kuburudisha na kuboresha afya ya akili.

Nimeanza kubaini kupitia ushabiki wa Simba na Yanga limezaliwa tatizo lingine jipya,Vijana hawajui au hawataki kufahamu kuhusu nchi yao.
Hawajui Bandari zimeuzwa kwa Waarabu.
Hawajui Uwanja wa ndege wa Kimatiafa Kilimanjaro umeuzwa.
Hawajui Ngorngoro imeuzwa kwa waarabu.
Hawajui Zanzibar inaitawala Tanganyika (Tanzania Bara)
Hawajui Ardhi ya nchi yao Tanganyika inauzwa kwa wageni.
Hawajui lolote kuhusu nchi yao.
Wakilala wakiamka Simba day,Yanga day huu upuuzi wa hizi team umewadumaza vijana wengi wa kiTanganyika badala ya kufikiri kuhusu nchi yao inavyoporwa kama wenzao wa Kenya wao wanakuambia "UBAYA UBWELA" siku wakistuka watakuta kila kitu kimeuzwa.

Ngongo kwasasa Gairo.
Unataka unalotaka wewe ndiyo liwe-POLE
 
Back
Top Bottom