Ushahidi CHADEMA inatumiwa na TICTS kukwamisha uboreshaji wa bandari

Mkuu, pingeni kama hamhujumu nchi
Ungekuwa na ushahidi konki wa tuhuma zako kwa unaowahisi ungeziweka hapa.Usiongozwe kwa hisia hasi tu dhidi ya wakinzani wa kimtazamo.Usijifanyie dunia ngumu kwa kuukubali ukweli kwamba mkataba ni wa kiwehu.
 
Huo uthibitisho ni upi? Kwa nini DP inatetewa na watu wenye upeo duni wa akili?

Mtu mwenye akili, hata akiamua kusema uwongo, hauwezi kukaa kwa namna ya kijinga kama hii!!
 
Huo uthibitisho ni upi? Kwa nini DP inatetewa na watu wenye upeo duni wa akili?

Mtu mwenye akili, hata akiamua kusema uwongo, hauwezi kukaa kwa namna ya kijinga kama hii!!
Piga
1. Mdude Chadema hakupost hiyo memo?
2. CHADEMA hamuendi Kagera kwenye +255 KATIBA MPYA NA OKOA BANDARI ZETU?
3. Hamkua mmesitisha +255 kwa kukosa hela? mmezipata wapi? mmeuza nini?
 
Watumiwe au wasitumiwe, hoja zijibiwe...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Anae kuzuia kwenda Mahakamani Nani wakati ushahdi unao??
Tuende mahakamani?! Sisi tunahakisha tunawasema kwa MUNGU ili nia zenu ovu zisifanikiwe
 
unataka ushahidi gani zaidi ya huo mkuu? mkishikwa pambaya mnaanda kuwa nit pickers
Kajifunze kwanza kuandika na kusoma, ndipo ulete mada kwa watu wenye weledi.

Kuandika kwenyewe shida. Hata kuelewa maana ya ushahidi, ni shida! Lakini unaamini umefikia kiwango cha kuleta mada.

Wewe unaonekana ni mtu unayetakiwa kuutumia muda wako mwingi zaidi kwa kujifunza kutoka kwa watu wenye uelewa. Hujafikia kiwango cha kumfundisha yeyote.
 
Sasa ushahidi upo wapi?
 
Ungekuwa na ushahidi konki wa tuhuma zako kwa unaowahisi ungeziweka hapa.Usiongozwe kwa hisia hasi tu dhidi ya wakinzani wa kimtazamo.Usijifanyie dunia ngumu kwa kuukubali ukweli kwamba mkataba ni wa kiwehu.
John Pambalu
@John_Pambalu
·
9m

Tumejadiliana kwa kina kuhusiana na namna ya kukomboa Bandari zetu. Tumehitimisha kuwa azimio la Kamati kuu la kuunganisha nguvu za wadau kuishikisha adabu serikali ndiyo njia pekee ya kukomboa Rasilimali zetu. Bado tuko jijini Mwanza kwa mapambano zaidi.




Mdau wa kwanza ni TICTS mhanga wa maboresho ya bandari
 
Na wananchi wengi wanaoupinga mkataba huo nao waliketi chini na TICTS?Mtatafutiza hadi vijikaratasi vya kwenye mapipa ya takataka mtuletee ili tuoneshe huruma kwenu!
Umeusoma mkataba wa kuuza bandari za Tanganyika?

Una maslahi kwa taifa? CHADEMA wanahusikaje hapo?

Bila shaka una shida kichwani wewe, si bure..!!
 

Huo ushahidi uko wapi? Maana umeandika tu maneno but no ushahidi
 
Watashindwa tu hawa mamluki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…