tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Dada wa kazi wa kizazi hiki ni zaidi ya majanga. Ndugu zangu, wasichana wa kazi za ndani (house girls/maids) ni hitaji muhimu sana kwa familia nyingi za mijini, hasa wale wanafamilia wanaofanya kazi zinazowalazimu kuamka asubuhi na kurejea jioni. Ni kwa sababu hii familia hulazimika kutafuta msichana wa kuwasaidia kazi za ndani, kama vile kufua, kusafisha na kudeki nyumba, kuangalia mtoto/watoto, kulinda nyumba na kufanya shughuli nyingine mbalimbali kadri atakavyopangiwa na mwajiri wake.
Kwa bahati mbaya sana, upatikanaji wa wasichana hawa umeingiliwa na matapeli (madalali) wanaoshirikiana na wasichana au wazazi wa wasichana kuwatapeli waajiri. Mimi ni mmoja wa wahanga waliolizwa na matapeli hawa pakubwa. Kuna matukio takribani manne ambayo nimelizwa na utapeli unaohusiana na wasichana wa kazi.
Sitasahau siku ambayo dada wa kazi aliiba simu na mshahara wote wa mke wangu na kutokomea kusikojulikana. Binti huyu alipatikana kutoka kwa dalali anayejihusisha na biashara ya kutafuta mabinti wa kazi kutoka mikoani na kuwasambaza kwa wahitaji. Tangu mwanzo watu walikuwa wakimshangaa binti kwa kuwa ni msichana mrembo, alimiliki simu kali ya smartphone hata kuliko “bosi” wake, na alipendelea kunyoa kiduku. Akiwa hana hili wala lile, boss lady alipitia benki akachukua mshahara na kuutia kwenye kipochi. Alipofika nyumbani akaweka simu na kipochi chumbani kwake na kuwahi kwenye TV kuangalia tamthlia (kama ilivyo kawaida kwa akina mama wengi kufuatilia tamthlia za kifilipino zilizotafsiriwa kwa Kiswahili kupitia Azam TV). Huku nyuma, binti akaingia chumbani akakomba mshahara na simu akatokomea kusikojulikana. Kumbe alikuwa tapeli mkubwa na aliyekubuhu. Baada ya tukio, boss lady alienda kufuatilia kwa dalali akaangukia patupu. Hasara haina mwisho!
Mbali na huyo mwizi, kuna binti mwingine wa kazi pia alipatikana kutoka kwa dalali; nakumbuka aliingia nyumbani majira ya saa 7 mchana. Ilipofika saa 10 tu akaanza kupandisha mashetani na kugalagala chini akisema: “Hii nyumba mashetani yangu hayataki nikae”. Basi, ikabidi tumruhusu aondoke, ijapokuwa tuliishaingia gharama kubwa kumlipa dalali na kumtumia nauli. Tulikuja kugundua maigizo ya mashetani ni njama walizokula na dalali wake ili apate sababu ya kuondoka “akauzwe” kwingine. Kumbe ni dili iliyopangwa ikapangika!
Mwingine alikuja siku ya leo; kesho akaonekana akinyata kuelekea getini akiwa na mizigo yake kwenye rambo.....boss lady alimchungulia kupitia dirishani......akamwambia wewe ondoka tu usipate shida ya kunyata. Alishachoshwa na vituko vya dada wa kazi.
Na wa mwisho aliletwa na dalali kutoka hapo karibu lakini akatudanganya amemtoa mbali.....dalali akalamba pesa ya udalali na nauli pia. Baada ya mwezi mmoja tu, dalali akamtorosha akaenda “kumuuza” kwingine. Hawa washenzy wanatia hasira sana.
Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia dada wa kazi aliye naye kwa sasa anatokea Morogoro. Alipofika tu babake akadai eti mtoto wake mbona kaenda mbali sana; na mbona sehemu aliko akiuliza kwa kila mtu anasema hapafahamu. Alimjibu kwa mkato: “Kwa hiyo sie tunaishi msituni? Unataka ufahamu kila sehemu huwa unasafiri mara kwa mara? Huyu aliyemwomba kwako humuamini? Yeye ndo anafahamu tulipo na kama unasema arudi, sawa kabisa. Mtumie nauli na mtu wa kumsindikiza na urudishe nauli yangu ya kumtolea huko hadi hapa na ya aliyemsindikiza, basi mwanao hata kesho arudi”. Anasema toka hapo baba katia heshima; anasisitiza tu mwanaye awe anaenda kusali. Inawezekana baba mtu alitaka kumfanyia utapeli lakini alipoona hatapeliki akawa mpole.
Hivi visa vichache ni ushahidi kwamba wahitaji wengi wa wasichana wa kazi, hasa kupitia madalali, hulizwa sana. Ninafikiri kuna mashuhuda wengine hapa JF mliowahi kulizwa na dada wa kazi kama ilivyo kwangu. Nanyi pia mnaweza kusimulia visa mlivyowahi kutapeliwa katika biashara hii kongwe. Mbali na simulizi za visa hivi, naomba tupeane uzoefu jinsi ya kukabiliana na utapeli huu wa kimjini.