Ushahidi kuntu kuhusu utapeli uliojificha ndani ya biashara ya dada wa kazi (house girls)

Ushahidi kuntu kuhusu utapeli uliojificha ndani ya biashara ya dada wa kazi (house girls)

Ilibidi uwe mpole tu sema awamu ijayo jitahidi walau hata both team to score😅 hakikisha umemtafuna huyo mshamba
Kweli bora hata ingekuwa droo kuliko away win, inauma sana. Na kumbuka mtu unakuwa umeweka stake kubwa 🤣 🤣 🤣
 
Kweli bora hata ingekuwa droo kuliko away win, inauma sana. Na kumbuka mtu unakuwa umeweka stake kubwa 🤣 🤣 🤣
Hahahahahah kiande wa kiembe samaki anakuwa kamenya “haji manara wa kutosha” inachoma sana
 
Sijamaliza kusoma maelezo yote ila nilipoelewa tu unachokizungumzia basi inatosha

Ushauri wangu chukueni kijijini kwenu wadada wa kazi... au ndo kizazi chenu chote kimezaliwa jijini hamna mjomba wala shangazi kule mkoani akawatafutia dada wa kazi
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Dada wa kazi wa kizazi hiki ni zaidi ya majanga. Ndugu zangu, wasichana wa kazi za ndani (house girls/maids) ni hitaji muhimu sana kwa familia nyingi za mijini, hasa wale wanafamilia wanaofanya kazi zinazowalazimu kuamka asubuhi na kurejea jioni. Ni kwa sababu hii familia hulazimika kutafuta msichana wa kuwasaidia kazi za ndani, kama vile kufua, kusafisha na kudeki nyumba, kuangalia mtoto/watoto, kulinda nyumba na kufanya shughuli nyingine mbalimbali kadri atakavyopangiwa na mwajiri wake.

Kwa bahati mbaya sana, upatikanaji wa wasichana hawa umeingiliwa na matapeli (madalali) wanaoshirikiana na wasichana au wazazi wa wasichana kuwatapeli waajiri. Mimi ni mmoja wa wahanga waliolizwa na matapeli hawa pakubwa. Kuna matukio takribani manne ambayo nimelizwa na utapeli unaohusiana na wasichana wa kazi.

Sitasahau siku ambayo dada wa kazi aliiba simu na mshahara wote wa mke wangu na kutokomea kusikojulikana. Binti huyu alipatikana kutoka kwa dalali anayejihusisha na biashara ya kutafuta mabinti wa kazi kutoka mikoani na kuwasambaza kwa wahitaji. Tangu mwanzo watu walikuwa wakimshangaa binti kwa kuwa ni msichana mrembo, alimiliki simu kali ya smartphone hata kuliko “bosi” wake, na alipendelea kunyoa kiduku. Akiwa hana hili wala lile, boss lady alipitia benki akachukua mshahara na kuutia kwenye kipochi. Alipofika nyumbani akaweka simu na kipochi chumbani kwake na kuwahi kwenye TV kuangalia tamthlia (kama ilivyo kawaida kwa akina mama wengi kufuatilia tamthlia za kifilipino zilizotafsiriwa kwa Kiswahili kupitia Azam TV). Huku nyuma, binti akaingia chumbani akakomba mshahara na simu akatokomea kusikojulikana. Kumbe alikuwa tapeli mkubwa na aliyekubuhu. Baada ya tukio, boss lady alienda kufuatilia kwa dalali akaangukia patupu. Hasara haina mwisho!

Mbali na huyo mwizi, kuna binti mwingine wa kazi pia alipatikana kutoka kwa dalali; nakumbuka aliingia nyumbani majira ya saa 7 mchana. Ilipofika saa 10 tu akaanza kupandisha mashetani na kugalagala chini akisema: “Hii nyumba mashetani yangu hayataki nikae”. Basi, ikabidi tumruhusu aondoke, ijapokuwa tuliishaingia gharama kubwa kumlipa dalali na kumtumia nauli. Tulikuja kugundua maigizo ya mashetani ni njama walizokula na dalali wake ili apate sababu ya kuondoka “akauzwe” kwingine. Kumbe ni dili iliyopangwa ikapangika!

Mwingine alikuja siku ya leo; kesho akaonekana akinyata kuelekea getini akiwa na mizigo yake kwenye rambo.....boss lady alimchungulia kupitia dirishani......akamwambia wewe ondoka tu usipate shida ya kunyata. Alishachoshwa na vituko vya dada wa kazi.

Na wa mwisho aliletwa na dalali kutoka hapo karibu lakini akatudanganya amemtoa mbali.....dalali akalamba pesa ya udalali na nauli pia. Baada ya mwezi mmoja tu, dalali akamtorosha akaenda “kumuuza” kwingine. Hawa washenzy wanatia hasira sana.

Rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia dada wa kazi aliye naye kwa sasa anatokea Morogoro. Alipofika tu babake akadai eti mtoto wake mbona kaenda mbali sana; na mbona sehemu aliko akiuliza kwa kila mtu anasema hapafahamu. Alimjibu kwa mkato: “Kwa hiyo sie tunaishi msituni? Unataka ufahamu kila sehemu huwa unasafiri mara kwa mara? Huyu aliyemwomba kwako humuamini? Yeye ndo anafahamu tulipo na kama unasema arudi, sawa kabisa. Mtumie nauli na mtu wa kumsindikiza na urudishe nauli yangu ya kumtolea huko hadi hapa na ya aliyemsindikiza, basi mwanao hata kesho arudi”. Anasema toka hapo baba katia heshima; anasisitiza tu mwanaye awe anaenda kusali. Inawezekana baba mtu alitaka kumfanyia utapeli lakini alipoona hatapeliki akawa mpole.

Hivi visa vichache ni ushahidi kwamba wahitaji wengi wa wasichana wa kazi, hasa kupitia madalali, hulizwa sana. Ninafikiri kuna mashuhuda wengine hapa JF mliowahi kulizwa na dada wa kazi kama ilivyo kwangu. Nanyi pia mnaweza kusimulia visa mlivyowahi kutapeliwa katika biashara hii kongwe. Mbali na simulizi za visa hivi, naomba tupeane uzoefu jinsi ya kukabiliana na utapeli huu wa kimjini.
yaani ni shida dada anakuja asubuhi ,jioni katoroshwa
 
Biashara nzima imejaa UTAPELI.

Siyo biashara rasmi.

Mishahara yenyewe mabosi wanalipa 20,000. Halafu wanaajiri sana watoto.

Muhimu.serikali ingerasmisha tu hii kazi ili watu wafanye kazi kama kazi rasmi na walipwe stahiki zao.
Kwa kipato gani
 
Endeleeni kuibiwa. Kama una hela weka mlinz wa kampuni na ufunge kamera.

Watoto peleka day care!
Au bek3 mlipe laki kama atakuibia.

Tatzo weng wenu mnalipa elfu 30, na matusi juu ataachaje kuiba na kutokomea?
Tena hawa wanawake wetu ndo uongoza kuwaumiza hawa mabinti kwa hako ka mshahara wa elf 30 au 50,Kazi nyingi,matusi,manyanyaso kibao.
Hawa mabinti sio kwamba wanapenda kufanya Kazi hizi ni kwa sababu ya umasikini wa familia zao msiwatende.
Wakati mwingine mnajipatia laana bure kwa kuumiza madada hawa.
 
Citaki ma bint wa kazi tena majuzi kafanya mpango na mpezi wake kijana moja muhuni anajulikana mtaani wakapanga kuiba TV yetu, mschana alicha fanya ni kufungua dilisha lilopo karibu na flat ya ukutani bila sisi kujua usiku wa manane akaja akaibeba inchi 55, duh ukaenda hivo, nilifanikiwa kumpata mwizi ni kampeleka police, ila tu na police wetu pia wezi baada ya siku 3 huyu huyu kijana nikamuina mtaani, ni kakubali hasara......... paka kesho huyu bint hajaonekana tena.
Cha msingi TV irudi, hao mamwela ni wakuwaogopa uliko hata mwizi mwenyewe
 
Cha msingi TV irudi, hao mamwela ni wakuwaogopa uliko hata mwizi mwenyewe
Tv imegoma kirudisha unacheza na hao police, walianza kunitishwa eti mwizi alipigwa sana angefia lookup kwahiyo tukampa bondi, nawaulizia TV iko wapi wananiuliza uliona wapi? Wakati walimpiga wenyewe.
 
Endeleeni kuibiwa. Kama una hela weka mlinz wa kampuni na ufunge kamera.

Watoto peleka day care!
Au bek3 mlipe laki kama atakuibia.

Tatzo weng wenu mnalipa elfu 30, na matusi juu ataachaje kuiba na kutokomea?
Hiyo ya kufunga camera ni wazo zuri
 
Tv imegoma kirudisha unacheza na hao police, walianza kunitisha eti mwizi alipigwa sana angefia lookup kwahiyo tukampa bondi, nawaulizia TV iko wapi wananiuliza uliona wapi?
Hawa ndio maana nazinguana nao sana huku mtaani, yani kupitia tatizo lako wanataka nao watatue matatizo yao hapo hapo

Kuna wale anaitwa sungusungu, kila nyumba mwisho wa mwezi wanapitia buku mbili kwa ajili ya ulinzi. Siku ukiibiwa ukasema uwaite wakusaidie kupatikana mali yako wanakupiga hela tena halafu hawajishughulishi na kutafuta

Hiyo TV mpaka hapo imeibiwa na hao mamwela
 
Mkuu, tatizo sio mishahra midogo isipokuwa ni utapeli unaofanywa na madalali kwa sbabu njaa zao binafsi.
Hiki visa vimekutokea wewe? Unatakiwa unajirebishe la sivyo utakuja kupata hasara kubwa zaidi. Kuna ule msemo unaosema ukiona mtu anarudia kufanya jambo lile lile, kwa namna ile ile, tena na tena, huku akitegemea matokeo tofauti basi ujue ana walakini. Hivi kweli kosa ulilofanya mara moja halikutosha kuku-alert? Hapa tunajadili kila siku hatari za kutumia madalali kwenye kutafuta wasichana wa kazi, unaweza kupekuwa na kukuta visa vingi sana. Ninachowaasha members ni hiki: mtu unayemkabidhi watoto wako, nyumba yako na kila kitu chako akutunzie wakati wewe hupo ni lazima umjue vya kutosha. Anatakiwa afanyiwe vetting na testing kubwa sana. Kumbuka anakuwa na access na siri za nyumbani kwako, unachokula nk.
 
Mmeyataka wenyewe, kila kitu dalali unashindwa kutafuta dada wa kazi wewe mwenyewe?

Halafu Dada atakae hakikisha unakula chakula salama, anakaa na mtoto wako nafamilia yako nzima! Unaachaje kumfanyia vetting ya kutosha..? Unawezaje ukaokota mtu wa namna hiyo barabarani tuu?? Hebu tuweni serious kidogo.

Nyumbani kwa wazaz wako kijijin kwenye asili yenu mliko tokea hakuna watu?? Chukueni watu ambao mna ukaribu nao hata kwa asilimia chache, mtu hupajui hata aliko zaliwa we unaokota tuu... akikuibia unaenda kumkaba dalali.. watu wa mjini wengi mnakua ni wapumbavu sana.. kwa Nyie mnatakiwa muibiwe sana hadi mshike akili.
 
Biashara nzima imejaa UTAPELI.

Siyo biashara rasmi.

Mishahara yenyewe mabosi wanalipa 20,000. Halafu wanaajiri sana watoto.

Muhimu.serikali ingerasmisha tu hii kazi ili watu wafanye kazi kama kazi rasmi na walipwe stahiki zao.
Asilimia nadhani 2% ndio watakuwa na jeuri ya kumlipa house girl mshahara.
 
Hiki visa vimekutokea wewe? Unatakiwa unajirebishe la sivyo utakuja kupata hasara kubwa zaidi. Kuna ule msemo unaosema ukiona mtu anarudia kufanya jambo lile lile, kwa namna ile ile, tena na tena, huku akitegemea matokeo tofauti basi ujue ana walakini. Hivi kweli kosa ulilofanya mara moja halikutosha kuku-alert? Hapa tunajadili kila siku hatari za kutumia madalali kwenye kutafuta wasichana wa kazi, unaweza kupekuwa na kukuta visa vingi sana. Ninachowaasha members ni hiki: mtu unayemkabidhi watoto wako, nyumba yako na kila kitu chako akutunzie wakati wewe hupo ni lazima umjue vya kutosha. Anatakiwa afanyiwe vetting na testing kubwa sana. Kumbuka anakuwa na access na siri za nyumbani kwako, unachokula nk.
Mkuu una busara sana.
 
Back
Top Bottom