Ushahidi kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuhusu tuhuma za wanafunzi kusahihishiana mitihani S/M Kimandafu

saigilomagema

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
5,673
Reaction score
7,811
Ndugu mkurugenzi napenda kukutaarifu kama mtanzania mzalendo na mwenye wivu mkubwa na ubora wa elimu yetu niliandika kupitia mtandao huu wa Jamii Forums juu ya matendo yasiyofaa yanayofanyika ktk shule ya msingi Kimandafu iliyoko ndani ya halmashauri ya wilaya ya Meru unayoiongoza hivi sasa. Najua kwa uhakika kuwa serikali yetu sikivu imefanya makubwa kufuatilia taarifa tajwa. Ila cha kusikitisha wadhibiti ubora waliotumwa na ofisi yako kwenda kufanya ukaguzi kuhakiki ukweli wa tuhuma zile waliishia kunywa chai na pengine kupewa takrima, kwa ufupi wali-collude na mtuhumiwa(mwl. Mkuu). Nayasema haya kwani afisa wa serikali aliyefunzwa na kuaminiwa lazima ajue mbinu za kufanya uchunguzi na ukaguzi, haiwezekani utoe taarifa juu ya ujio wako na nini unachokifuatilia. Kiukweli mwalimu mkuu aliwandaa wanafunzi wake namna ya kuwajibu wale wadhibiti ubora, ile ni aibu na fedheha kubwa. Kwanza umetumwa kuchunguza tuhuma inawezekanaje na unapewa chain a takrima zingine? Je kwa maana hiyo ingekuwaje kama na polisi wangekuwa wanafanya uchunguzi kwa style ile? Ofisa ametokea Usa River yaliko makao makuu ya Halmashauri umbali wa kilomita isiyofika 10 amejisikia njaa saa ngapi na ametumia usafiri wa serikali. Ni aibu!

Jambo la pili mwalimu mkuu aliitisha kikao cha wazazi mnamo tarehe 05.06.2025, kikao kilichohudhuriwa na baadhi ya maafisa kutoka ofisini kwako. Ajenda ya kikao kile kilikuwa kujadili maendeleo ya shule. Kikao kilitakiwa kuanza saa 2 asubuhi, bahati mbaya mwalimu mkuu na mwenyekiti wa kamati ya shule waliitumia kikao kile kwa maslahi yao binafsi. Kikao kilijaa uzushi, uwongo, vitisho, upandikizaji wa chuki, uenezi wa chuki hasa kwa kushambulia familia moja anayoihisi mwalimu mkuu kuwa ndio walioandika taarifa zile ktk huu mtandao. Mimi ni mtanzania nisiyependa uzembe, uonevu, unyanyasaji na dhuluma dhidi ya haki za wanafunzi wa shule ile. Nimekuwa nikiandika post mbalimbali kuhusu changamoto mbalimbali ndani ya nchi yetu. Ikiwa Rais wa nchi anaandikwa kila siku saa zingine kwa uwongo, uzushi lakini Rais hajawahi kumtafuta mchawi. Yule mwalimu mkuu anakosa sifa ya msingi ya kuwa kiongozi, ukiambiwa uko uchi busara ni kuchutama siyo kupambana na aliyekupata taarifa. Kwanini alinde walimu wazembe.

Inavyoonekana ni mtu amekaa kile kituo pengine kwa muda mrefu unaokaribia miaka 20, ndio maana yuko karibu sana na viongozi wa kijiji na kata na wanamtetea kwa mambo waiyoyajua, mtendaji wa kata alicheza ngoma asiyoijua, kuna mzee moja kwa vyovyote vile atakuwa alinunuliwa kwa jinsi alivyokuwa anatukana na kutishia kuwa watamloga anayeandika mambo ya shule, mara tutamlaani, sasa sijui hiyo laana wanamwomba Mungu watakayemchonga wao au huyu mungu tunayemjua sisi. Kwa ufupi Yule mwalimu mkuu alitumia kile kikao cha wazazi kutafuta huruma ya wazazi, kuwapotosha, kuwapumbaza, kuwadanganya, kupandika na kueneza chuki baina ya wananchi jambo ambalo ni hatari sana. Kwa kuwa yeye ana jukwaa la kuzungumza yaani anaweza kuwaita wazazi na kuwatumia kujisafisha, sisi watanzania wa kawaida hatuna jukwaa lingine zaidi ya jukwaa km hili la Jamii Forums kwa hiyo asitutishie, asitishie wasiohusika.

Msingi wa uzi wangu wa kwanza ulikuwa ni wanafunzi wa madarasa ya juu kama la sita na la saba kusahihisha mitihani ya wanafunzi wa madarasa ya chini na vilevile wanafunzi wa darasa la saba kusahihishiana mitihani wenyewe kwa wenyewe km inavyoonekana ktk mtihani wa English darasa la VII 2024. Ni kwamba kinachomsumbua yeye ni ushamba tu, habari zinazoandikwa humu nyingi zina ushahidi, hakutakiwa kupanic, kutishia na kuwanyanyasa baadhi ya wanafunzi anaohisi wazazi wao wanahusika. Hata ni kweli watoto wanahusika nini? Unaendaje kuwasimanga, kuwaonea, kuwanyanyasa malaika wasio na hatia. Je kwake yeye itakuwa sahihi kuhukumiwa makosa ya babake? Yule mama ni katili lisilo na punje ya huruma.

Kwa yaliyojadiliwa katika kile kikao cha wazazi kipi cha uwongo:

  1. Mitihani haisahihishwi na wanafunzi? Nitakuambatanishia baadhi ya vielelezo vya awali
  2. Je hajawaondoa wanafunzi wawili waliokuwa wanafanya usafi ktk ofisi yake? Yeye mwenyewe alikiri mbele ya kikao cha wazazi na kusema kuwa baba wa moja wa watoto ndio mimi, jambo linalohitaji ushahidi usioacha shaka
  3. Je watoto halishwi makukuru(makande yasiyokobolewa)?. Ingawa jambo la ajabu aliwasuka watu waliojiita wazazi kuwa wao wanapenda watoto wao kula makukuru na ugali wa dona na maharage km mbpga, hii ni ajabu sana na iko wazi wale watu walihongwa, hakuna mzazi angependa kuona mtoto wake akila chakula kibaya. Ni kwasababu tu Yule mwl. Mkuu ni katili hana upendo wala huruma kwa watoto wadogo. Mbona shule zenye wanafunzi zaidi ya 1300 ndani ya kata ille ile ya Maji ya Chai wanalishwa vizuri? Wazazi walipumbazwa na kupotoshwa
  4. Je wanafunzi hawalipii kila mtihani? Yalithibitishwa kwenye kikao cha wazazi
  5. Je unga wa lishe na choroko hakugawana na walimu wenzake? Hata ktk hili nitaleta ushahidi au kafuatilie shule za jirani ndani ya kata hiyo hiyo ya Maji ya Chai.
Vifuatavyo ni viambatanisho vya vielelezo vya awali kuhusu wanafunzi kusahihishiana mitihani:

  1. Baadhi ya mitihani ya English std VII, mwaka 2024
  2. Sehemu ya mtihani wa utimilifu wa Sayansi na Teknolojia, Mei 2024
    Majibu yaliyojazwa na mwanafunzi yametokana na habari iliyoandikwa, je kwa mujibu wa habari husika majibu aliyoyajaza mwanafunzi siyo sahihi? Tukisema kumejaa uchafu tunakosea, tuna wadhibiti ubora au wadhibiti uchafu?
  3. Sehemu ya mtihani wa utimilifu wa maarifa ya Jamii, Mei 2024
    Sehemu C
    Swali 3(i) usahihishaji ni wa kihuni umefanywa na mwanafunzi na iko wazi, ndio tunavyochezea elimu yetu?
  4. Mtihani wa muhula wa wa I wa Hisabati, Mei 2025
    3(c) KDS cha 18 na 30 siyo 90?. Kwanini mwanafunzi kakoseshwa maksi? Hii siyo dhuluma?
    5(e) Je kipeuo cha pili cha 361 siyo 19? Kwanini kakoseshwa? Je ni mwalimu kweli aliyesahihisha huu mtihani?
Hii ni baadhi ya vielelezo vya kuanzia nitaambatanisha vingine kila ninapoona inafaa.
Kama mtumishi wa umma uliyeaminiwa na mh. Rais kushughulikia na kuatatua kero za wananchi natumai utalishughulikia jambo hili ili haki itendeke na ionekane ikitendeka. Ahsante!

Huyo mwalimu wako aache vitisho alimtumia mtendaji wa kata ya Maji ya Chai kutishia wazazi ktk kikao cha wazazi cha tarehe 05.06.2025 kuwa atawashughulikia wanaotuma habari kwenye mitandao, Mtendaji wa kata anahusika vipi na utendaji wa kila siku wa shule? Kwanini anacheza ngoma asiyoijua na isiyomhusu? Vitisho, matusi yanafanyika mbele ya maafisa wako, ni kusema kwamba walibariki vitendo vile visivyo vya kimaadili? Sisi tutaendelea kutumia mitandao ya kijamii yeye aendelee kuwatumia viongozi wa serikali, kamati ya shule na vikao vya wazazi kama jukwaa lake kujitetea, kututishia ila hatashinda. Nitaendelea kukutumia vielelezo vingine kwa njia nitakayoona inafaa ikiwa ni pamoja nah ii ninayoitumia sasa.
Kama kuna mtu atabisha kuwa hiyo mitihani siyo ya shule ya msingi Kimandafu, nitakuletea hard copies original ofisini kwako.

Pia soma
  1. Wanafunzi kusahihishiana mitihani shule ya msingi Kimandafu
  2. Meru: Hii tabia ya wanafunzi kusahihisha mitihani ya wanafunzi wenzao ndio competence-based education?
 
Attachments

wewe mwalimu una shida gani?
 
Msemakweli mpenzi wa Mungu, uovu ndio unatuletea watawala wabovu.

Ni sahihi kurekebisha huko chini kabla hawajaingia UVCC na UWT, maana wakiisha fika kwenye hizo jumuiya wanakuwa miungu watu.
 
Kama na wewe ni mwalimu shuleni hapo unachangia akina Mpwayungu Village wawatukane watu wa kada yenu.

Shule ina wanafunzi 2000, huku walimu wako 7, unategemea nani atamudu kutekeleza majukumu hayo?.

Ukiona elimu anayopata mwanao haina ubora, uko huru kumpeleka mwanao unakoona elimu itolewayo hapo inamfaa mwanao.
 
Sikujua kama hilo ni kosa, shule ya msingi ni kawaida hata mimi nishatumika kusahihisha mitihani ya wenzangu
 
Shule si mama yako, ikizingua hamisha mtoto. Hela yako isiwafanye wanao wateseke kwa kulishwa makukuru, mapalage na dona usivyovipenda; na kusahihishiwa mitihani na wanafunzi wenzao.

Au hiyo ni ST. ELIMU BURE badala ya ST. PETER?
 
Mwlm ana mikondo ya kutosha afundishe asahihishe na aandae azimio la kazi, serikali ajirini Walimu jamani wanaelemewa mno....... Siyo rahisi kama mnavyofikiria.
 
Hii ni kwa shule zilizonyingi wanasahihishiana wanafunzi,sasa si bora wewe wamepigiana tick zimenyooka tena kwa wino mwekundu!
KARIBU MBEYA MJINI mwanafunzi shule ya msingi kila anapokwenda shule lazima apewe buku ya mitihani,mitihani yenyewe wanafunzi husahihishiana tena kwa pen ya blue!hadi alivyokosa huwekewa tick,KWAKWELI MAMBO YAMEHARIBIKA SANA SASA!

TUTAFUTE HELA TUU HIZI SHULE ZA SERIKALI SIYO ZA KUPELEKA MTOTO 😔😔
 
Wewe ni wale wazazi mnaotaka hata sare za shule zinunuliwe na serikali. Acha roho mbaya. Hamishia mtoto wako St Patrick
 
Wewe jamaa una roho mbaya sana kwa jinsi ulivyoandika inaonekana haujatmfanya utafiti kuhusu hali ya shule zetu na hali ya walimu.
Moyoni umejaa visasi sana unahitaji maombi.
Zunguka shule 100 utakuta shule 1 ndio walimu wanasahihisha ntakupa mfano shule zilizopo katani kwangu

Shule 1. Ina wanafunzi 1480 kuanzia drs la 1 hadi saba huku ina walimu 5 tafsiri yake kila mwl ana masomo saba na kuendelea ya kufundisha. Sasa swali linakuja unadhan wakati wa mitihani ya kufunga shule huyu mwl asahihishe mitihan yte hyo pekee yake apange vibutu n.k ndani ya wiki moja? Kuwa na chembe ya aibu wewe mla makande yasiokobolewa wewe.

Nyambafu punguza roho mbaya
 
Ndugu mkurugenzi napenda kukutaarifu kama mtanzania mzalendo na mwenye wivu mkubwa na ubora wa elimu yetu niliandika kupitia mtandao huu wa Jamii Forums juu ya matendo yasiyofaa yanayofanyika ktk shule ya msingi Kimandafu iliyoko ndani ya halmashauri ya wilaya ya Meru unayoiongoza hivi sasa. Najua kwa uhakika kuwa serikali yetu sikivu imefanya makubwa kufuatilia taarifa tajwa. Ila cha kusikitisha wadhibiti ubora waliotumwa na ofisi yako kwenda kufanya ukaguzi kuhakiki ukweli wa tuhuma zile waliishia kunywa chai na pengine kupewa takrima, kwa ufupi wali-collude na mtuhumiwa(mwl. Mkuu). Nayasema haya kwani afisa wa serikali aliyefunzwa na kuaminiwa lazima ajue mbinu za kufanya uchunguzi na ukaguzi, haiwezekani utoe taarifa juu ya ujio wako na nini unachokifuatilia. Kiukweli mwalimu mkuu aliwandaa wanafunzi wake namna ya kuwajibu wale wadhibiti ubora, ile ni aibu na fedheha kubwa. Kwanza umetumwa kuchunguza tuhuma inawezekanaje na unapewa chain a takrima zingine? Je kwa maana hiyo ingekuwaje kama na polisi wangekuwa wanafanya uchunguzi kwa style ile? Ofisa ametokea Usa River yaliko makao makuu ya Halmashauri umbali wa kilomita isiyofika 10 amejisikia njaa saa ngapi na ametumia usafiri wa serikali. Ni aibu!

Jambo la pili mwalimu mkuu aliitisha kikao cha wazazi mnamo tarehe 05.06.2025, kikao kilichohudhuriwa na baadhi ya maafisa kutoka ofisini kwako. Ajenda ya kikao kile kilikuwa kujadili maendeleo ya shule. Kikao kilitakiwa kuanza saa 2 asubuhi, bahati mbaya mwalimu mkuu na mwenyekiti wa kamati ya shule waliitumia kikao kile kwa maslahi yao binafsi. Kikao kilijaa uzushi, uwongo, vitisho, upandikizaji wa chuki, uenezi wa chuki hasa kwa kushambulia familia moja anayoihisi mwalimu mkuu kuwa ndio walioandika taarifa zile ktk huu mtandao. Mimi ni mtanzania nisiyependa uzembe, uonevu, unyanyasaji na dhuluma dhidi ya haki za wanafunzi wa shule ile. Nimekuwa nikiandika post mbalimbali kuhusu changamoto mbalimbali ndani ya nchi yetu. Ikiwa Rais wa nchi anaandikwa kila siku saa zingine kwa uwongo, uzushi lakini Rais hajawahi kumtafuta mchawi. Yule mwalimu mkuu anakosa sifa ya msingi ya kuwa kiongozi, ukiambiwa uko uchi busara ni kuchutama siyo kupambana na aliyekupata taarifa. Kwanini alinde walimu wazembe.

Inavyoonekana ni mtu amekaa kile kituo pengine kwa muda mrefu unaokaribia miaka 20, ndio maana yuko karibu sana na viongozi wa kijiji na kata na wanamtetea kwa mambo waiyoyajua, mtendaji wa kata alicheza ngoma asiyoijua, kuna mzee moja kwa vyovyote vile atakuwa alinunuliwa kwa jinsi alivyokuwa anatukana na kutishia kuwa watamloga anayeandika mambo ya shule, mara tutamlaani, sasa sijui hiyo laana wanamwomba Mungu watakayemchonga wao au huyu mungu tunayemjua sisi. Kwa ufupi Yule mwalimu mkuu alitumia kile kikao cha wazazi kutafuta huruma ya wazazi, kuwapotosha, kuwapumbaza, kuwadanganya, kupandika na kueneza chuki baina ya wananchi jambo ambalo ni hatari sana. Kwa kuwa yeye ana jukwaa la kuzungumza yaani anaweza kuwaita wazazi na kuwatumia kujisafisha, sisi watanzania wa kawaida hatuna jukwaa lingine zaidi ya jukwaa km hili la Jamii Forums kwa hiyo asitutishie, asitishie wasiohusika.

Msingi wa uzi wangu wa kwanza ulikuwa ni wanafunzi wa madarasa ya juu kama la sita na la saba kusahihisha mitihani ya wanafunzi wa madarasa ya chini na vilevile wanafunzi wa darasa la saba kusahihishiana mitihani wenyewe kwa wenyewe km inavyoonekana ktk mtihani wa English darasa la VII 2024. Ni kwamba kinachomsumbua yeye ni ushamba tu, habari zinazoandikwa humu nyingi zina ushahidi, hakutakiwa kupanic, kutishia na kuwanyanyasa baadhi ya wanafunzi anaohisi wazazi wao wanahusika. Hata ni kweli watoto wanahusika nini? Unaendaje kuwasimanga, kuwaonea, kuwanyanyasa malaika wasio na hatia. Je kwake yeye itakuwa sahihi kuhukumiwa makosa ya babake? Yule mama ni katili lisilo na punje ya huruma.

Kwa yaliyojadiliwa katika kile kikao cha wazazi kipi cha uwongo:

  1. Mitihani haisahihishwi na wanafunzi? Nitakuambatanishia baadhi ya vielelezo vya awali
  2. Je hajawaondoa wanafunzi wawili waliokuwa wanafanya usafi ktk ofisi yake? Yeye mwenyewe alikiri mbele ya kikao cha wazazi na kusema kuwa baba wa moja wa watoto ndio mimi, jambo linalohitaji ushahidi usioacha shaka
  3. Je watoto halishwi makukuru(makande yasiyokobolewa)?. Ingawa jambo la ajabu aliwasuka watu waliojiita wazazi kuwa wao wanapenda watoto wao kula makukuru na ugali wa dona na maharage km mbpga, hii ni ajabu sana na iko wazi wale watu walihongwa, hakuna mzazi angependa kuona mtoto wake akila chakula kibaya. Ni kwasababu tu Yule mwl. Mkuu ni katili hana upendo wala huruma kwa watoto wadogo. Mbona shule zenye wanafunzi zaidi ya 1300 ndani ya kata ille ile ya Maji ya Chai wanalishwa vizuri? Wazazi walipumbazwa na kupotoshwa
  4. Je wanafunzi hawalipii kila mtihani? Yalithibitishwa kwenye kikao cha wazazi
  5. Je unga wa lishe na choroko hakugawana na walimu wenzake? Hata ktk hili nitaleta ushahidi au kafuatilie shule za jirani ndani ya kata hiyo hiyo ya Maji ya Chai.
Vifuatavyo ni viambatanisho vya vielelezo vya awali kuhusu wanafunzi kusahihishiana mitihani:

  1. Baadhi ya mitihani ya English std VII, mwaka 2024
  2. Sehemu ya mtihani wa utimilifu wa Sayansi na Teknolojia, Mei 2024
    Majibu yaliyojazwa na mwanafunzi yametokana na habari iliyoandikwa, je kwa mujibu wa habari husika majibu aliyoyajaza mwanafunzi siyo sahihi? Tukisema kumejaa uchafu tunakosea, tuna wadhibiti ubora au wadhibiti uchafu?
  3. Sehemu ya mtihani wa utimilifu wa maarifa ya Jamii, Mei 2024
    Sehemu C
    Swali 3(i) usahihishaji ni wa kihuni umefanywa na mwanafunzi na iko wazi, ndio tunavyochezea elimu yetu?
  4. Mtihani wa muhula wa wa I wa Hisabati, Mei 2025
    3(c) KDS cha 18 na 30 siyo 90?. Kwanini mwanafunzi kakoseshwa maksi? Hii siyo dhuluma?
    5(e) Je kipeuo cha pili cha 361 siyo 19? Kwanini kakoseshwa? Je ni mwalimu kweli aliyesahihisha huu mtihani?
Hii ni baadhi ya vielelezo vya kuanzia nitaambatanisha vingine kila ninapoona inafaa.
Kama mtumishi wa umma uliyeaminiwa na mh. Rais kushughulikia na kuatatua kero za wananchi natumai utalishughulikia jambo hili ili haki itendeke na ionekane ikitendeka. Ahsante!

Huyo mwalimu wako aache vitisho alimtumia mtendaji wa kata ya Maji ya Chai kutishia wazazi ktk kikao cha wazazi cha tarehe 05.06.2025 kuwa atawashughulikia wanaotuma habari kwenye mitandao, Mtendaji wa kata anahusika vipi na utendaji wa kila siku wa shule? Kwanini anacheza ngoma asiyoijua na isiyomhusu? Vitisho, matusi yanafanyika mbele ya maafisa wako, ni kusema kwamba walibariki vitendo vile visivyo vya kimaadili? Sisi tutaendelea kutumia mitandao ya kijamii yeye aendelee kuwatumia viongozi wa serikali, kamati ya shule na vikao vya wazazi kama jukwaa lake kujitetea, kututishia ila hatashinda. Nitaendelea kukutumia vielelezo vingine kwa njia nitakayoona inafaa ikiwa ni pamoja nah ii ninayoitumia sasa.
Kama kuna mtu atabisha kuwa hiyo mitihani siyo ya shule ya msingi Kimandafu, nitakuletea hard copies original ofisini kwako.

Pia soma
  1. Wanafunzi kusahihishiana mitihani shule ya msingi Kimandafu
  2. Meru: Hii tabia ya wanafunzi kusahihisha mitihani ya wanafunzi wenzao ndio competence-based education?
Kimsingi hiyo shule haina uongozi, wanachezea elimu ya watoto wetu, nani atawafanyia urekebu hao watoto waliopotoshwa? Leo umemkosesha mtoto jibu sahihi kuwa KDS ya 18 na 30 siyo 90, kesho anaambiwa na mtu mwingine jibu lake lilikuwa sahihi, mpk kipeuo cha pili cha 361 eti siyo 19? Hv ingelikuwa shule ya private huo upumbavu ungefanyika? Walimu wameharibu shule za serikali halafu wao hao hao wanazitukana kuwa ni Kayumba watoto wao hawasomi hizo shule kumbe wanajua sababu kuwa wanafunzi ndio husahihisha mitihani na si walimu. Bado kuna watu wanaitwa wadhibiti ubora, kweli? Hao ni wadhibiti uchafu. Maafisa wa serikali walitumwa hiyo shule wakaishia kubugia chai hawakutimiza wajibu wao. Nenda kasome sasa ripoti waliyoandika, utachoka km siyo kuzimia. Hakuna afisa wa serikali mwenye mtoto anayesoma shule ya serikali siku hizi, ni kwa kuwa wenyewe wanajua sababu. Sasa nani wa kusaidia shule za serikali hasa za misingi? Maana huku ndiko msingi unakojengwa, inajulikana nyumba yenye msingi mbovu lazima iwe mbovu. Ndugu mleta maada Mungu akubariki ulete vielelezo zaidi. Mwl. Mkuu badala achukue hatua anaenda kunyanyasa watoto wa watu, anaenda kutishia watu tena asiowahamu, ni aibu na fedheha. Inawezekanaje mtu mdogo km yule anapumbaza majitu mazima na elimu zao? Kuna namna.
 
Ndugu mkurugenzi napenda kukutaarifu kama mtanzania mzalendo na mwenye wivu mkubwa na ubora wa elimu yetu niliandika kupitia mtandao huu wa Jamii Forums juu ya matendo yasiyofaa yanayofanyika ktk shule ya msingi Kimandafu iliyoko ndani ya halmashauri ya wilaya ya Meru unayoiongoza hivi sasa. Najua kwa uhakika kuwa serikali yetu sikivu imefanya makubwa kufuatilia taarifa tajwa. Ila cha kusikitisha wadhibiti ubora waliotumwa na ofisi yako kwenda kufanya ukaguzi kuhakiki ukweli wa tuhuma zile waliishia kunywa chai na pengine kupewa takrima, kwa ufupi wali-collude na mtuhumiwa(mwl. Mkuu). Nayasema haya kwani afisa wa serikali aliyefunzwa na kuaminiwa lazima ajue mbinu za kufanya uchunguzi na ukaguzi, haiwezekani utoe taarifa juu ya ujio wako na nini unachokifuatilia. Kiukweli mwalimu mkuu aliwandaa wanafunzi wake namna ya kuwajibu wale wadhibiti ubora, ile ni aibu na fedheha kubwa. Kwanza umetumwa kuchunguza tuhuma inawezekanaje na unapewa chain a takrima zingine? Je kwa maana hiyo ingekuwaje kama na polisi wangekuwa wanafanya uchunguzi kwa style ile? Ofisa ametokea Usa River yaliko makao makuu ya Halmashauri umbali wa kilomita isiyofika 10 amejisikia njaa saa ngapi na ametumia usafiri wa serikali. Ni aibu!

Jambo la pili mwalimu mkuu aliitisha kikao cha wazazi mnamo tarehe 05.06.2025, kikao kilichohudhuriwa na baadhi ya maafisa kutoka ofisini kwako. Ajenda ya kikao kile kilikuwa kujadili maendeleo ya shule. Kikao kilitakiwa kuanza saa 2 asubuhi, bahati mbaya mwalimu mkuu na mwenyekiti wa kamati ya shule waliitumia kikao kile kwa maslahi yao binafsi. Kikao kilijaa uzushi, uwongo, vitisho, upandikizaji wa chuki, uenezi wa chuki hasa kwa kushambulia familia moja anayoihisi mwalimu mkuu kuwa ndio walioandika taarifa zile ktk huu mtandao. Mimi ni mtanzania nisiyependa uzembe, uonevu, unyanyasaji na dhuluma dhidi ya haki za wanafunzi wa shule ile. Nimekuwa nikiandika post mbalimbali kuhusu changamoto mbalimbali ndani ya nchi yetu. Ikiwa Rais wa nchi anaandikwa kila siku saa zingine kwa uwongo, uzushi lakini Rais hajawahi kumtafuta mchawi. Yule mwalimu mkuu anakosa sifa ya msingi ya kuwa kiongozi, ukiambiwa uko uchi busara ni kuchutama siyo kupambana na aliyekupata taarifa. Kwanini alinde walimu wazembe.

Inavyoonekana ni mtu amekaa kile kituo pengine kwa muda mrefu unaokaribia miaka 20, ndio maana yuko karibu sana na viongozi wa kijiji na kata na wanamtetea kwa mambo waiyoyajua, mtendaji wa kata alicheza ngoma asiyoijua, kuna mzee moja kwa vyovyote vile atakuwa alinunuliwa kwa jinsi alivyokuwa anatukana na kutishia kuwa watamloga anayeandika mambo ya shule, mara tutamlaani, sasa sijui hiyo laana wanamwomba Mungu watakayemchonga wao au huyu mungu tunayemjua sisi. Kwa ufupi Yule mwalimu mkuu alitumia kile kikao cha wazazi kutafuta huruma ya wazazi, kuwapotosha, kuwapumbaza, kuwadanganya, kupandika na kueneza chuki baina ya wananchi jambo ambalo ni hatari sana. Kwa kuwa yeye ana jukwaa la kuzungumza yaani anaweza kuwaita wazazi na kuwatumia kujisafisha, sisi watanzania wa kawaida hatuna jukwaa lingine zaidi ya jukwaa km hili la Jamii Forums kwa hiyo asitutishie, asitishie wasiohusika.

Msingi wa uzi wangu wa kwanza ulikuwa ni wanafunzi wa madarasa ya juu kama la sita na la saba kusahihisha mitihani ya wanafunzi wa madarasa ya chini na vilevile wanafunzi wa darasa la saba kusahihishiana mitihani wenyewe kwa wenyewe km inavyoonekana ktk mtihani wa English darasa la VII 2024. Ni kwamba kinachomsumbua yeye ni ushamba tu, habari zinazoandikwa humu nyingi zina ushahidi, hakutakiwa kupanic, kutishia na kuwanyanyasa baadhi ya wanafunzi anaohisi wazazi wao wanahusika. Hata ni kweli watoto wanahusika nini? Unaendaje kuwasimanga, kuwaonea, kuwanyanyasa malaika wasio na hatia. Je kwake yeye itakuwa sahihi kuhukumiwa makosa ya babake? Yule mama ni katili lisilo na punje ya huruma.

Kwa yaliyojadiliwa katika kile kikao cha wazazi kipi cha uwongo:

  1. Mitihani haisahihishwi na wanafunzi? Nitakuambatanishia baadhi ya vielelezo vya awali
  2. Je hajawaondoa wanafunzi wawili waliokuwa wanafanya usafi ktk ofisi yake? Yeye mwenyewe alikiri mbele ya kikao cha wazazi na kusema kuwa baba wa moja wa watoto ndio mimi, jambo linalohitaji ushahidi usioacha shaka
  3. Je watoto halishwi makukuru(makande yasiyokobolewa)?. Ingawa jambo la ajabu aliwasuka watu waliojiita wazazi kuwa wao wanapenda watoto wao kula makukuru na ugali wa dona na maharage km mbpga, hii ni ajabu sana na iko wazi wale watu walihongwa, hakuna mzazi angependa kuona mtoto wake akila chakula kibaya. Ni kwasababu tu Yule mwl. Mkuu ni katili hana upendo wala huruma kwa watoto wadogo. Mbona shule zenye wanafunzi zaidi ya 1300 ndani ya kata ille ile ya Maji ya Chai wanalishwa vizuri? Wazazi walipumbazwa na kupotoshwa
  4. Je wanafunzi hawalipii kila mtihani? Yalithibitishwa kwenye kikao cha wazazi
  5. Je unga wa lishe na choroko hakugawana na walimu wenzake? Hata ktk hili nitaleta ushahidi au kafuatilie shule za jirani ndani ya kata hiyo hiyo ya Maji ya Chai.
Vifuatavyo ni viambatanisho vya vielelezo vya awali kuhusu wanafunzi kusahihishiana mitihani:

  1. Baadhi ya mitihani ya English std VII, mwaka 2024
  2. Sehemu ya mtihani wa utimilifu wa Sayansi na Teknolojia, Mei 2024
    Majibu yaliyojazwa na mwanafunzi yametokana na habari iliyoandikwa, je kwa mujibu wa habari husika majibu aliyoyajaza mwanafunzi siyo sahihi? Tukisema kumejaa uchafu tunakosea, tuna wadhibiti ubora au wadhibiti uchafu?
  3. Sehemu ya mtihani wa utimilifu wa maarifa ya Jamii, Mei 2024
    Sehemu C
    Swali 3(i) usahihishaji ni wa kihuni umefanywa na mwanafunzi na iko wazi, ndio tunavyochezea elimu yetu?
  4. Mtihani wa muhula wa wa I wa Hisabati, Mei 2025
    3(c) KDS cha 18 na 30 siyo 90?. Kwanini mwanafunzi kakoseshwa maksi? Hii siyo dhuluma?
    5(e) Je kipeuo cha pili cha 361 siyo 19? Kwanini kakoseshwa? Je ni mwalimu kweli aliyesahihisha huu mtihani?
Hii ni baadhi ya vielelezo vya kuanzia nitaambatanisha vingine kila ninapoona inafaa.
Kama mtumishi wa umma uliyeaminiwa na mh. Rais kushughulikia na kuatatua kero za wananchi natumai utalishughulikia jambo hili ili haki itendeke na ionekane ikitendeka. Ahsante!

Huyo mwalimu wako aache vitisho alimtumia mtendaji wa kata ya Maji ya Chai kutishia wazazi ktk kikao cha wazazi cha tarehe 05.06.2025 kuwa atawashughulikia wanaotuma habari kwenye mitandao, Mtendaji wa kata anahusika vipi na utendaji wa kila siku wa shule? Kwanini anacheza ngoma asiyoijua na isiyomhusu? Vitisho, matusi yanafanyika mbele ya maafisa wako, ni kusema kwamba walibariki vitendo vile visivyo vya kimaadili? Sisi tutaendelea kutumia mitandao ya kijamii yeye aendelee kuwatumia viongozi wa serikali, kamati ya shule na vikao vya wazazi kama jukwaa lake kujitetea, kututishia ila hatashinda. Nitaendelea kukutumia vielelezo vingine kwa njia nitakayoona inafaa ikiwa ni pamoja nah ii ninayoitumia sasa.
Kama kuna mtu atabisha kuwa hiyo mitihani siyo ya shule ya msingi Kimandafu, nitakuletea hard copies original ofisini kwako.

Pia soma
  1. Wanafunzi kusahihishiana mitihani shule ya msingi Kimandafu
  2. Meru: Hii tabia ya wanafunzi kusahihisha mitihani ya wanafunzi wenzao ndio competence-based education?
Hivi Kwanini walimu mna chuki sana?
 
Walimu pendaneni, chuki hazitawasaidia chochote.
 
Ni suala la haki ya watoto wetu hakuna chuki hapo, walimu wa shule za serikali wamekuwa hawajali, wazembe, wavivu, mbaya zaidi kiongozi wao ambaye ni mwl. Mkuu anatetea uchafu, wadhibiti ubora wamegeuka wadhibiti uchafu, wanaweza kuhongwa ht kwa chai, je hatima ya elimu ya wanetu ni nini? Shule binafsi hawawezi ht kujaribu kufanya huo upuuzi. Mwanafunzi amepata majibu anakoseshwa, je nani atamrekebisha mtoto km huyo, wanawachanganya watoto, wamewadhulumu haki zao za msingi kwamba wamepunjwa maksi, mitihani inasahihishwa kihuni. Badala mwaliku mkuu asafishe nyumba yake anataka kutapatapa kutafuta mchawi anaenda kuwanyanyasa na kuwakatili watoto ambao anahisi mzazi wao ndio ameanika huo uchafu mitandaoni. Anataka kushindana na mitandao? Ataweza? Ndio anajiharibia zaidi. Mbaya zaidi anatumia kamati ya shule, mwenyekiti wa kamati hushinda shuleni, ana vipindi? Ni kwamba mwl. Mkuu hana uwezo wa kuongoza
 
Labda ungefafanua zaidi kuhusu;

Mosi, Shule inawanafunzi wangapi na Walimu wangapi?

Je Kuna uwiano kati ya idadi ya Wanafunzi na Walimu wa masomo kwenye shule hiyo??

Kama hakuna uwiano wa idadi ya Walimu na Wanafunzi hapo shida inaanzia hapo .

Unakuta Mwalimu anafundisha masomo mawili, idadi ya somo la kiswahili Wanafunzi 300 na somo la hesabu Wanafunzi 300 Jumla huyu Mwalimu anapaswa atahini Mitihani 600 yenye maswali 1-25 au 50 n.k.

Huyu Mwalimu ni wazi hawezi kumaliza kwa siku mbili wala tatu.

Hivyo njia anayoifanya ni maswali ya kuchagua Wanafunzi kubadilishana maswali na kuweka alama ya kosa au pata.

Yale ya kujieleza ndo Mwalimu husika husahihisha.

Ila kama hawana upingufu wa Walimu na wanawapa Wanafunzi basi Kuna shida.

Kumbuka Kuna shule Moja niliwahi kuisikia ilikuwa na Mwalimu mmoja tu shule nzima. Alikuwa akifundisha anasaidiana na kiranja Mkuu wa shule.

Kwahiyo kuhusu Wanafunzi kusahihishana ni Katika Mazingira kama hayo.

Sasa ungechunguza idadi ya Walimu na Wanafunzi kama zinawiana ndipo utoe dukuduku lako.

Kuhusu Wanafunzi kukoseshwa hili siyo kwasababu Wanafunzi kusahihishana wenyewe kwa wenyewe ndo maana wamekoseshwa hapana.

Hata angesahihisha Mwalimu Bado angeweza kuwakosesha.

Ndiyo maana hata Baraza la Mitihani la Taifa matokeo yakitoka watu hukata rufaa na wakikata matokeo Yao hubadilika kama awali alipata divisheni 3 atapanda na kupata div 1 au 2!

Hii maana yake Nini? Hii maana yake mtahiniwa Kuna maswali alikoseshwa.

Hata ngazi ya shule ,Mwalimu anaweza akasahihisha mwenyewe na Bado akamkosesha mwanafunzi na mwanafunzi huyo akipewa mtihani akirudi kwa Mwalimu wake kulalamika husahihishiwa upya na maks huongezeka.

Hii maana yake alimkosesha hapo awali.

Hivyo hakuna MWANADAMU aliyekamilika.

Hivyo kukoseshwa kwa Wanafunzi hakuwezi kuwa ushahidi wa kuwa Wanafunzi wanasahihishiana kwani hata Walimu nao hufanya mistake hiyo hiyo.

KIKUBWA tuendelee kuisadia serikali iajili Walimu wengi zaidi. Wastani Mwalimu mmoja afundishe Wanafunzi 45.

Je shule yako inawastani huo? Yaani Kila Mwalimu anawanafunzi 45??

Kama ni zaidi ya hapo ,Ujue shida inaanzia hapo.
 
Ni suala la haki ya watoto wetu hakuna chuki hapo, walimu wa shule za serikali wamekuwa hawajali, wazembe, wavivu, mbaya zaidi kiongozi wao ambaye ni mwl. Mkuu anatetea uchafu, wadhibiti ubora wamegeuka wadhibiti uchafu, wanaweza kuhongwa ht kwa chai, je hatima ya elimu ya wanetu ni nini? Shule binafsi hawawezi ht kujaribu kufanya huo upuuzi. Mwanafunzi amepata majibu anakoseshwa, je nani atamrekebisha mtoto km huyo, wanawachanganya watoto, wamewadhulumu haki zao za msingi kwamba wamepunjwa maksi, mitihani inasahihishwa kihuni. Badala mwaliku mkuu asafishe nyumba yake anataka kutapatapa kutafuta mchawi anaenda kuwanyanyasa na kuwakatili watoto ambao anahisi mzazi wao ndio ameanika huo uchafu mitandaoni. Anataka kushindana na mitandao? Ataweza? Ndio anajiharibia zaidi. Mbaya zaidi anatumia kamati ya shule, mwenyekiti wa kamati hushinda shuleni, ana vipindi? Ni kwamba mwl. Mkuu hana uwezo wa kuongoza
Suala la chai ni la kawaida kabisa na haliwezi kuathili utendaji .

Kudhibiti ubora ni vioo vya Walimu.

Wanapokuja hukaa na Walimu na kuwapa maelekezo ya mambo ambayo wameyaona hayapo sawa

Kama walifika maana yake wameacha ripoti kwa Mkuu huyo wa shule na wamemuagiza ashughulikie.

Huongea na wazazi,Wanafunzi,viongozi wa eneo Hilo.

Kwahiyo sidhani kama wanaweza kufumbia jambo.
 
Back
Top Bottom