PostGE2025 Ushahidi wa mauaji kwa watu wasiohusika na maandamano

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mianzini kata ya makurumla jimbo la ubungo kwa tiketi ya ccm mr njele,wamemzika ijumaa iliyopita,alikula shaba ya shingo akiwa amesimama pale shule ya msingi ya mianzini mburahati
Hii ni mbaya sana katika taifa linalojinasibu kutii utawala wa sheria na utu wa raia
 
Upolisi ni kazi yalaana. Kuwa tu na cheo cha upolisi ni laana kubwa.
 
1. Polisi waliingia kwenye kituo cha watoto wanaojifunza mpira (football academy) wakati watoto hao wakijifunza kwa vitendo mambo ya mpira kwenye runinga, wakawaua watoto 7 kwa risasi papo hapo.
Umetumia mara nyingi sana kwenye mada yako neno hili "polisi".

Naomba tu kujuwa uhakika wako kuwa hawa kweli walikuwa ni polisi. Walikuwa kwenye nguo zao za kikazi zinazofahamika?

Hapa naomba ujue tu kuwa sina sababu hata moja ya kutetea jeshi la polisi la Tanzania.; kwani maovu yao yanajulikana hata kabla ya hili la kuua waTanzania 'indiscriminately', kama ulivyo eleza hapa.
 
Polisi wote waliohusika na mauji walikuwa in uniforms. Hakukuwa na polisi aliyevaa kiraia mkuu.
 
Huu utawala usipofikishwa ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu tutakuwa hatuna tofauti na wanyama
Hizi taasisi za nje, kama zilivyo hizi tulizo nazo sasa hapa hapa hazina maana sana katika maisha wa watu.

Ni bora, iwapo kama tutafanikiwa wenyewe kujinasua kwenye janga hili; tutengeneze utaratibu wa kuwashughulikia watu waovu kama hawa.
Huko ICC itakuwa ni kama wapo likizo tu, hata kama watapatikana na hatia.
Kwani Idd Amin kuishi kwake Saud, si ni kama alikuwa yupo jela ya nje tu!
 
ebu tujiulize kwann wanachukua mait , zingatien hili swal , mnaeza lijib kiutan utan ila hapa ndo chanz cha yote
 
swali lako ni nyet sn likijibiwa ndipo ukwel utajulikana nan mhusika
 
Kuna dogo mmoja miaka kama 27...
Katoka maeneo ya Kisongo Arusha...mpaka majengo siku ya Ijumaa...kachoka vibaya...
Kafika kwa Dada yake ..akanywa maji kwa kiu ...
Ilikuwa saa 3 usiku dogo akamwambia Dada yake Nina njaa na sioni msosi...
Dada akamwambia ufanye fasta..Toka nje..Kuna nenda duka flani gonga kwa nje atakufungulia nunua mkate, pia nunua na sabuni.
Kwa kuwa sio mbali dogo katoka ndani katembea ...mpaka kwenye Lami ...akavuka akagonga duka...
Akafumguliwa dirisha kapewa mkate na sabuni..dogo anarudi ana vuka Lami..gari ya Polisi hii hapa...kapigwa risasi 3 za kifua..
Polisi wakaendelea na safari zao...
Amezikwa juzi
 
Walimuua mwenyekiti wa CCM aliyetiki. Walikuwa hawachagui mkuu. Yeyote wanayemuona mtaani anakula shaba
Kuna picha nyingine zinazo onyesha watu waliovaa t-shirts wakiwa na bunduki wakiwasaka watu wa kuwaua, ndio maana nikauliza swali hilo.

Sasa kwa upande huo wa askari walioshiriki mauaji, hilo ni rahisi kwa sababu pa kuanzia pako wazi, ni kwa akina Jumanne Mulilo.
 
swali lako ni nyet sn likijibiwa ndipo ukwel utajulikana nan mhusika
Mkuu 'tpaul' (mleta mada), kisha thibitisha kuwa hao alnao wazungumzia yeye walikuwa wamevaa mavazi rasmi ya kipolisi. Kwa upande huo ni rahisi kidogo kujuwa wapi pa kuanzia; kwani akina Jumanne Mulilo italazimu wajibu maswali.
Lakini pia kuna matokeo ya mauaji ya waTanzania yaliyo wahusisha watu ambao hawakuwa na alama yoyote ya kidola, wakihusika kwenye mauaji. Picha zao zimo humu humu JF, kwenye uzi ulioletwa na mkuu 'waufukweni'. Hawa nao italazimu kujuwa walikuwa wakifanya mauaji kwa amri ya nani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…