PostGE2025 Ushahidi wa mauaji kwa watu wasiohusika na maandamano

PostGE2025 Ushahidi wa mauaji kwa watu wasiohusika na maandamano

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Am
Kila nikiwafikiria wale wa banda la mpira akili yangu inaenda mbali sana, nakumbuka siku hiyo hiyo nami na wanangu tulikuwa banda la mpira, tukaforce tutizame game, huku arsenal na burnley, kule man u na Nottingham forest! Kibaya zaidi mashabiki wa man u wakawa wanapiga kelele kiasi nikawaambia wanangu mmepagawa ama!! Akiwemo na mdogo wangu wa kiume

Hawa waliouawa naona ndio kama sisi siku ile.
Dogo alipoiona tu hii ya mwanza, fasta akaja kunionesha, akikumbuka siku ile tunatizamq mpira na jinsi nilivyowakoromea mule waache usenge.

Mungu apumzishe roho za ndugu zetu, na kukatishwa kwao uhai wao na iwe sababu ya kuwatia peponi!!

mola wangu, najua HUKUMU nzito ni siku ya kiama nayo ndio siku ya malipo kwa yooote, kwa wale waliodhulumu roho za wenzao, ila nakuomba mola wangu uwape adhabu hapa duniani na kesho akhera uwape hukumu yao nzito. Wadhalilishe hapa duniani.. kila chozi la mfiwa na huzuni ya walioondokew iwe laana juu ya hawa wauaji na waliopanga mauaji
Amiyn Allahumma Amyn
 
Hivi watawala wanajisikiaje wanapokaa madarakani kwa sababu ya kumwaga damu za raia? Hiyo amani ya roho na akili wanaitoa wapi? Inawezekana kabisa mtu askishakuwa mtawala anakuwa na roho ya shetani. Kwa hiyo, hawa watawala tunapaswa kuwakemea na kuwalaani zaidi ya tunavyokemea mapepo. Na ukiona kiongozi yeyote wa dini kama Mwamposa anawashabikia watawala, ntu huyo muogope zaidi ya ukoma.
Correct
 
Kijana wangu ambaye niliamua kujitolea kumsaidia baada ya maisha kuwa magumu, nilimlipia ufundi, akawa Fundi wa milango na madirisha ya Aluminum, amenipigia simu juzi kuwa amepigwa risasi na askari mguuni huku room mate wake akiaga dunia baada ya ku-bleed sana kuanzia saa nne hadi saa kumi walivyopata matibabu Mbagala. Audio ninayo nimemrekodi.....nimeumia sana sana
Pole sana; hatutaikiwi tena nchi hii kwaani inawenyewe. Wanyonge tutamalizwa.
 
Awali ya yote napenda kuweka wazi kuwa sishabikii maandamano wala mauaji ya raia wasiokuwa na hatia. Niliyoshuhudia au kusimuliwa na watu kuhusu maauji ya baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025 yanahuzunisha sana na yamenifanya niamini kuwa jeshi la polisi Tanzania linafanya kazi kitutusa sana.

Nimeanzisha uzi huu ili tupeane updates kuhusu kilochojiri kwenye maeneo yetu ili kuthibitisha ukiukwaji wa maadili uliofanywa na jeshi la polisi kwa raia wasiokuwa na hatia. Katika eneo nililopo watu wengi sana waliouliwa hawakuwa na hatia na wala hawakuhusika kwenye maandamano. Pamoja na kuzimwa kwa huduma ya internet na wananchi kuzuiliwa kufanya shughuli zao za kiuchumi, ni dhahairi wananchi mmeshuhudia mauaji holela katika maeneo yenu ambayo yangeweza kuepukika ikiwa polisi wangetumia busara na weledi.

Matukio ya kipuuzi na yasiyokuwa na chembe ya utu ambayo nimeshuhudia au kusimuliwa na wananchi wakati nikichukua takwimu za mauaji ni mengi lakini naomba niweke haya machache kwa kuwa mengi yanafanana na haya.

1. Polisi waliingia kwenye kituo cha watoto wanaojifunza mpira (football academy) wakati watoto hao wakijifunza kwa vitendo mambo ya mpira kwenye runinga, wakawaua watoto 7 kwa risasi papo hapo.

2. Katika tukio lingine, polisi waliokuwa wakirandaranda huku na huku walifika kwenye baa moja na kuwakuta watu wakinywa pombe. Wakamuita mzee mmoja akatoka nje kabla hajafika mbali wakampiga risasi kifuani akafia palepale.

3. Polisi waliwakuta vijana dukani wakiwa kwenye foleni ya kununua bidhaa, wakawaamrisha walale chini kifudifudi bila kujitikisha. Wakawapiga risasi za kisogoni wote kisha wakapakia maiti kwenye gari wakaondoka nazo.

4. Polisi walivamia genge la mama ntilie mmoja, wakawatawanya raia waliokuwa wakila chakula kwa kuwarushia risasi za moto. Risasi ikampata mama ntilie ikampasua kichwa akafia palepale.

5. Polisi walipita mtaani wakawakuta wanafamilia wameketi nje ya nyumba yao wanajipatia chakula cha jioni, wakwarushia risasi mfululizo na kufanikiwa kumuua baba wa familia na mtoto wake mmoja papo hapo.

Kwa mifano hiyo michache ni wazi kuwa polisi wa Tanzania hawana weledi kabisa wa kikazi. Hata kama walipewa maagizo ya kuua raia kwa risasi za moto, hakukuwa na haja ya kuwaua raia wasiokuwa na hatia kwa kuwapiga risasi ovyo. Kwa takwimu hizi za kusimuliwa na kushuhudia mwenyewe, ni dhahiri wananchi wengi waliouawa hawakuwa kwenye maandamano na wala walikuwa hawafanyi vurugu yoyote. Fikiria watu wako kwenye shughuli zao lakini wanauliwa bila sababu za msingi.

Tumekuwa tukishuhudia kwingineko duniani polisi wakituliza maandamano lakini siokwa staili hii ya polisi wa Tanzania. Inasikitisha sana. Hizi roho za wananchi wasiokuwa na hatia zilizozimwa na polisi haziwezi kupita bure.

Je, eneo ulilopo kuna tukio gani la mauaji ya ovyo uliloshuhudia? Tunataka tukusanye matukio ya kutosha ili watetea haki za binadamu na ICC wazitumie kama reference ya kuichukulia hatua serikali ya Tanzania kwa mauaji haya ya halaiki.
Mkuu, itapendeza ukiweka na eneo tukio husika lilipotokea ili kuweka kumbukumbu sawa.
 
Mkuu 'tpaul' (mleta mada), kisha thibitisha kuwa hao alnao wazungumzia yeye walikuwa wamevaa mavazi rasmi ya kipolisi. Kwa upande huo ni rahisi kidogo kujuwa wapi pa kuanzia; kwani akina Jumanne Mulilo italazimu wajibu maswali.
Lakini pia kuna matokeo ya mauaji ya waTanzania yaliyo wahusisha watu ambao hawakuwa na alama yoyote ya kidola, wakihusika kwenye mauaji. Picha zao zimo humu humu JF, kwenye uzi ulioletwa na mkuu 'waufukweni'. Hawa nao italazimu kujuwa walikuwa wakifanya mauaji kwa amri ya nani.
Yote haya yanapaswa kujibiwa na wenye dhamana ya ulinzi wa watu na mali zao.

Sisi kama wananchi hatuna chombo cha uchunguzi. Kwa waliokuwa na uniform na wasio na uniform anayepaswa kuwa accountable anajulikana.

Wananchi hatuna silaha za kivita, watu hawa wasio na uniform wana silaha za kivita ni akina nani? Tukumbuke weeks/a month back Mange kimambi alitoa taarifa juu ya kuingizwa kontena lenye silaha ambalo halinasibishwi na Majeshi yetu(taarifa kama hii ilipuuzwaje)

Katika mlolongo wote huu wa kuwa accountable anajulikana narudia.
 
Kulingana na mtiririko wa habari, kwa mtazamo mbona ni kama kuna watu ama kundi lilikua na kisasi kifuani, walikua wakisubiri nafasi ya dhahabu siku moja itokee waweze kulipa? Ukiachana either amri ilitolewa lakini ni kama wameenda zaidi, na imekua kama kulipa KISASI. Embu tufikiri kwa kina, inawezekana hili jambo likawa limebeba mengi ndani yake.
Good observation.

Mpaka nachelea kusema waliotoa maagizo ya kutuliza maandamano “hawakukusudia hili”

Lakini hadi pale watakowajibika ndipo watajikosha na hili, Until then hili ni la kwao.

Ukiwa msomaji mzuri wa comments mtandaoni, Kuna watu wanazungumzia kuwa “zoeeni hiki ndicho alichofanya Hayati Mkapa (RIP) Pemba mwaka ule.. (Sina hakika na ukweli wa kinachoongelewa katika hizo comments na sijafunua vitabu vya historia kuhusu hili. )

Kauli iliyonukuliwa ya hayati Mkapa kwenye hotuba ya Rais Samia ilikuwa bahati mbaya?
 
Samia Suluhu Hassan damu hizi haziatakuacha salama hata kidogo usijetafuta mchawi.
Unfortunately kuna watu wataangushiwa huu mzigo.

Tuendelee Kuweka records sawasawa, mfululizo wa matukio ya utekaji kwa miaka minne, Kauli ya kiongozi mkuu juu ya utekaji na mauaji, kauli za jeshi la polisi, kutokumuwajibisha mtekaji hata mmoja… kejeli kwa waliotekwa na kulaumu victims… Waliotekwa walitekwa na waliokemea utekaji walitekwa.

Wana kesi ya kujibu.
 
Awali ya yote napenda kuweka wazi kuwa sishabikii maandamano wala mauaji ya raia wasiokuwa na hatia. Niliyoshuhudia au kusimuliwa na watu kuhusu maauji ya baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025 yanahuzunisha sana na yamenifanya niamini kuwa jeshi la polisi Tanzania linafanya kazi kitutusa sana.

Nimeanzisha uzi huu ili tupeane updates kuhusu kilochojiri kwenye maeneo yetu ili kuthibitisha ukiukwaji wa maadili uliofanywa na jeshi la polisi kwa raia wasiokuwa na hatia. Katika eneo nililopo watu wengi sana waliouliwa hawakuwa na hatia na wala hawakuhusika kwenye maandamano. Pamoja na kuzimwa kwa huduma ya internet na wananchi kuzuiliwa kufanya shughuli zao za kiuchumi, ni dhahairi wananchi mmeshuhudia mauaji holela katika maeneo yenu ambayo yangeweza kuepukika ikiwa polisi wangetumia busara na weledi.

Matukio ya kipuuzi na yasiyokuwa na chembe ya utu ambayo nimeshuhudia au kusimuliwa na wananchi wakati nikichukua takwimu za mauaji ni mengi lakini naomba niweke haya machache kwa kuwa mengi yanafanana na haya.

1. Polisi waliingia kwenye kituo cha watoto wanaojifunza mpira (football academy) wakati watoto hao wakijifunza kwa vitendo mambo ya mpira kwenye runinga, wakawaua watoto 7 kwa risasi papo hapo.

2. Katika tukio lingine, polisi waliokuwa wakirandaranda huku na huku walifika kwenye baa moja na kuwakuta watu wakinywa pombe. Wakamuita mzee mmoja akatoka nje kabla hajafika mbali wakampiga risasi kifuani akafia palepale.

3. Polisi waliwakuta vijana dukani wakiwa kwenye foleni ya kununua bidhaa, wakawaamrisha walale chini kifudifudi bila kujitikisha. Wakawapiga risasi za kisogoni wote kisha wakapakia maiti kwenye gari wakaondoka nazo.

4. Polisi walivamia genge la mama ntilie mmoja, wakawatawanya raia waliokuwa wakila chakula kwa kuwarushia risasi za moto. Risasi ikampata mama ntilie ikampasua kichwa akafia palepale.

5. Polisi walipita mtaani wakawakuta wanafamilia wameketi nje ya nyumba yao wanajipatia chakula cha jioni, wakwarushia risasi mfululizo na kufanikiwa kumuua baba wa familia na mtoto wake mmoja papo hapo.

Kwa mifano hiyo michache ni wazi kuwa polisi wa Tanzania hawana weledi kabisa wa kikazi. Hata kama walipewa maagizo ya kuua raia kwa risasi za moto, hakukuwa na haja ya kuwaua raia wasiokuwa na hatia kwa kuwapiga risasi ovyo. Kwa takwimu hizi za kusimuliwa na kushuhudia mwenyewe, ni dhahiri wananchi wengi waliouawa hawakuwa kwenye maandamano na wala walikuwa hawafanyi vurugu yoyote. Fikiria watu wako kwenye shughuli zao lakini wanauliwa bila sababu za msingi.

Tumekuwa tukishuhudia kwingineko duniani polisi wakituliza maandamano lakini siokwa staili hii ya polisi wa Tanzania. Inasikitisha sana. Hizi roho za wananchi wasiokuwa na hatia zilizozimwa na polisi haziwezi kupita bure.

Je, eneo ulilopo kuna tukio gani la mauaji ya ovyo uliloshuhudia? Tunataka tukusanye matukio ya kutosha ili watetea haki za binadamu na ICC wazitumie kama reference ya kuichukulia hatua serikali ya Tanzania kwa mauaji haya ya halaiki.
Kwanza nikwambie katika umbwaji wa binadamu katika ulimwengu wa kiroho kuna maana kubwa sana,binadamu siyo sawa na mnyama,hao waliofanya hivyo tayali huko waliko wameshaanza kupata matatizo kutokana roho za watu waliowauwa,
Mfano mfupi siyo kila kichaa kalogwa,wengine ni sababu ya kufanyia mambo yao gizani kama kuuwa wanajikuta mwishowe wanachanganyikiwa
 
Nawachukia polisi vibaya mno.
Nilikataa nafasi ya kujiunga jeshi la polisi, ilikuwa nimetafutiwa na dada yangu mwenye unasaba na RPC fulani mwanamke miaka hiyo nimehitimu kidato couldha 6.
Lakini naomba niseme huu uliyoweka hapa ni ubongo kuhusu sifa za kujiunga na jeshi la polisi.
Nilikuwa na classmates wa chuo kikuu wenye GPA kubwa sana walijiunga na jeshinla polisi. Hivyo ingekuwa kweli usemayo wasingepata hiyo nafasi.
Hao ni wasomi wachache wanaokuja kupata vyeo vikubwa kama akina Mafwele na akina Muliro. Na hawa ni commanding officers.

Mimi naongelea utitiri wa haya maroboti ya huku chini yanayotumwa kwenda kupiga watu risasi hata kama ni familia mmekusanyika mnakula au watoto wamekusanyika ndani wanaangalia katuni.
 
Kuna picha nyingine zinazo onyesha watu waliovaa t-shirts wakiwa na bunduki wakiwasaka watu wa kuwaua, ndio maana nikauliza swali hilo.

Sasa kwa upande huo wa askari walioshiriki mauaji, hilo ni rahisi kwa sababu pa kuanzia pako wazi, ni kwa akina Jumanne Mulilo.
Hebu tupia humu tuzione mkuu.
 
Kulingana na mtiririko wa habari, kwa mtazamo mbona ni kama kuna watu ama kundi lilikua na kisasi kifuani, walikua wakisubiri nafasi ya dhahabu siku moja itokee waweze kulipa? Ukiachana either amri ilitolewa lakini ni kama wameenda zaidi, na imekua kama kulipa KISASI. Embu tufikiri kwa kina, inawezekana hili jambo likawa limebeba mengi ndani yake.
Sidhani kama kulikuwa na kitu kama hicho mkuu. Ni ushenzi tu wa polisi katika matumizi ua ovyo ya silaha
 
Hata kama walipewa maagizo ya kuua polisi walivuka mipaka na kwa hili Gen Z hawatasemehe na nichelee kusema maandamano yajayo watu watatua polisi there will be no mercy.Hizo video za vijana waliouawa kwenye banda la mpira,waliouawa nje ya nyumba zao zimechochea chuki kubwa mno.Tanzania itaingia kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe
 
Wakati hayo yote yanatokea Muliro na Wambura na makamanda wa Polisi wamejificha kambini Lugalo na familia zao wakilindwa na JW
 
Good observation.

Mpaka nachelea kusema waliotoa maagizo ya kutuliza maandamano “hawakukusudia hili”

Lakini hadi pale watakowajibika ndipo watajikosha na hili, Until then hili ni la kwao.

Ukiwa msomaji mzuri wa comments mtandaoni, Kuna watu wanazungumzia kuwa “zoeeni hiki ndicho alichofanya Hayati Mkapa (RIP) Pemba mwaka ule.. (Sina hakika na ukweli wa kinachoongelewa katika hizo comments na sijafunua vitabu vya historia kuhusu hili. )

Kauli iliyonukuliwa ya hayati Mkapa kwenye hotuba ya Rais Samia ilikuwa bahati mbaya?
Naam, kuna mengi endapo utatazama jambo hili katika angle tofauti. Japo sijasikiliza hiyo hotuba, unaweza quote hiyo kauli aliyowahi sema Mkapa ambayo imekua refered?
 
Back
Top Bottom