PostGE2025 Ushahidi wa mauaji kwa watu wasiohusika na maandamano

PostGE2025 Ushahidi wa mauaji kwa watu wasiohusika na maandamano

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Unazijua sifa za kujiunga na jeshi la polisi? Hata ukiwa na D mbili form 4 hawakuchukui. Wanataka wenye D moja na F zote. Halafu unategemea wawe na akili ya kujiongeza? Yale hata maroboti yana unafuu. Yakiambiwa mkikuta watu wamekusanyika tandika risasi basi yanabeba amri hivyo hivyo. Hata kama ni familia mmekusanyika mnakula linawanyuka tu risasi. Mtu mwenye D moja si ni sawa tu na mtu mwenye utindio wa ubongo? 😳😳😳😳😳
😂😂😂😂
 
Awali ya yote napenda kuweka wazi kuwa sishabikii maandamano wala mauaji ya raia wasiokuwa na hatia. Niliyoshuhudia au kusimuliwa na watu kuhusu maauji ya baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025 yanahuzunisha sana na yamenifanya niamini kuwa jeshi la polisi Tanzania linafanya kazi kitutusa sana.

Nimeanzisha uzi huu ili tupeane updates kuhusu kilochojiri kwenye maeneo yetu ili kuthibitisha ukiukwaji wa maadili uliofanywa na jeshi la polisi kwa raia wasiokuwa na hatia. Katika eneo nililopo watu wengi sana waliouliwa hawakuwa na hatia na wala hawakuhusika kwenye maandamano. Pamoja na kuzimwa kwa huduma ya internet na wananchi kuzuiliwa kufanya shughuli zao za kiuchumi, ni dhahairi wananchi mmeshuhudia mauaji holela katika maeneo yenu ambayo yangeweza kuepukika ikiwa polisi wangetumia busara na weledi.

Matukio ya kipuuzi na yasiyokuwa na chembe ya utu ambayo nimeshuhudia au kusimuliwa na wananchi wakati nikichukua takwimu za mauaji ni mengi lakini naomba niweke haya machache kwa kuwa mengi yanafanana na haya.

1. Polisi waliingia kwenye kituo cha watoto wanaojifunza mpira (football academy) wakati watoto hao wakijifunza kwa vitendo mambo ya mpira kwenye runinga, wakawaua watoto 7 kwa risasi papo hapo.

2. Katika tukio lingine, polisi waliokuwa wakirandaranda huku na huku walifika kwenye baa moja na kuwakuta watu wakinywa pombe. Wakamuita mzee mmoja akatoka nje kabla hajafika mbali wakampiga risasi kifuani akafia palepale.

3. Polisi waliwakuta vijana dukani wakiwa kwenye foleni ya kununua bidhaa, wakawaamrisha walale chini kifudifudi bila kujitikisha. Wakawapiga risasi za kisogoni wote kisha wakapakia maiti kwenye gari wakaondoka nazo.

4. Polisi walivamia genge la mama ntilie mmoja, wakawatawanya raia waliokuwa wakila chakula kwa kuwarushia risasi za moto. Risasi ikampata mama ntilie ikampasua kichwa akafia palepale.

5. Polisi walipita mtaani wakawakuta wanafamilia wameketi nje ya nyumba yao wanajipatia chakula cha jioni, wakwarushia risasi mfululizo na kufanikiwa kumuua baba wa familia na mtoto wake mmoja papo hapo.

Kwa mifano hiyo michache ni wazi kuwa polisi wa Tanzania hawana weledi kabisa wa kikazi. Hata kama walipewa maagizo ya kuua raia kwa risasi za moto, hakukuwa na haja ya kuwaua raia wasiokuwa na hatia kwa kuwapiga risasi ovyo. Kwa takwimu hizi za kusimuliwa na kushuhudia mwenyewe, ni dhahiri wananchi wengi waliouawa hawakuwa kwenye maandamano na wala walikuwa hawafanyi vurugu yoyote. Fikiria watu wako kwenye shughuli zao lakini wanauliwa bila sababu za msingi.

Tumekuwa tukishuhudia kwingineko duniani polisi wakituliza maandamano lakini siokwa staili hii ya polisi wa Tanzania. Inasikitisha sana. Hizi roho za wananchi wasiokuwa na hatia zilizozimwa na polisi haziwezi kupita bure.

Je, eneo ulilopo kuna tukio gani la mauaji ya ovyo uliloshuhudia? Tunataka tukusanye matukio ya kutosha ili watetea haki za binadamu na ICC wazitumie kama reference ya kuichukulia hatua serikali ya Tanzania kwa mauaji haya ya halaiki.
Taarifa yako imejaa propaganda tupu. Wewe hangaika na Kagame huko kwenu Rwanda.
 
Kila nikiwafikiria wale wa banda la mpira akili yangu inaenda mbali sana, nakumbuka siku hiyo hiyo nami na wanangu tulikuwa banda la mpira, tukaforce tutizame game, huku arsenal na burnley, kule man u na Nottingham forest! Kibaya zaidi mashabiki wa man u wakawa wanapiga kelele kiasi nikawaambia wanangu mmepagawa ama!! Akiwemo na mdogo wangu wa kiume

Hawa waliouawa naona ndio kama sisi siku ile.
Dogo alipoiona tu hii ya mwanza, fasta akaja kunionesha, akikumbuka siku ile tunatizamq mpira na jinsi nilivyowakoromea mule waache usenge.

Mungu apumzishe roho za ndugu zetu, na kukatishwa kwao uhai wao na iwe sababu ya kuwatia peponi!!

mola wangu, najua HUKUMU nzito ni siku ya kiama nayo ndio siku ya malipo kwa yooote, kwa wale waliodhulumu roho za wenzao, ila nakuomba mola wangu uwape adhabu hapa duniani na kesho akhera uwape hukumu yao nzito. Wadhalilishe hapa duniani.. kila chozi la mfiwa na huzuni ya walioondokew iwe laana juu ya hawa wauaji na waliopanga mauaji
Kwani umesharudi TZ mkuu?
 
Huu utawala usipofikishwa ICC kwa uhalifu dhidi ya binadamu tutakuwa hatuna tofauti na wanyama
Ujinga mwingine ni kusubiri ICC watatue matatizo yenu. Je walishayatatua ya wapi... Somalia, libya, palestina au???? Kulishana upuuzi tu
 
Wakati hayo yote yanatokea Muliro na Wambura na makamanda wa Polisi wamejificha kambini Lugalo na familia zao wakilindwa na JW
Inasikitisha sana. Next time tutaanza nao.
 
Ujinga mwingine ni kusubiri ICC watatue matatizo yenu. Je walishayatatua ya wapi... Somalia, libya, palestina au???? Kulishana upuuzi tu
Wewe unashauri nini kifanyike mkuu?
 
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mianzini kata ya makurumla jimbo la ubungo kwa tiketi ya ccm mr njele,wamemzika ijumaa iliyopita,alikula shaba ya shingo akiwa amesimama pale shule ya msingi ya mianzini mburahati
Walitusaliti hao watanzania wenzao wakajua watakuwa salama..!!
Ndiomana tunawaambia unafki ni kitu kibaya, hapo alitoka ili ashuhudie tunavyouliwa matokeo yake kala chuma yeye familia yao 😹
 
Wewe unashauri nini kifanyike mkuu?
Kutegemea demage control kutoka mataifa ya kigeni ni kujidanganya na kujitengenezea mazingira ya kutawaliwa kuliko livyo sasa....

Unadhani ni wangapi wamekufa mwaka huu kwa machafuko ya kisiasa... Yani Mmarekani aitoe CCM madarakani na anamikataba ya gesi Mtwara😂 na possibly kama Jeshi lulitachukua washaona kilichotokea kwa Mfaransa kule Bukinabe.

Kuliingiza jeshi mkenge kutawala Tanzania ni kujadili upuuzi na wakijidanganya kufanya hivyo wataona maana halisi ya CCM NA MIFUMO YAKE NCHINI..... Namaanisha Hivi ilipaswa kuiparalaiz CCM kwa mpango wa muda mrefu kwanza ndipo lifuate suala la maandamano.

Na kwasababu imeshafanyika attemp ccm inarudi kujipanga upya 2030 upinzani utashangazwa.

Aidha, Kama nchi imefahamika shida ilikua wapi na wapi tuliteleza ni muda wa kujijenga upya.

Ila........

Lazima kila upande ukiri kukosea na wananchi wawe tayari kupokea matokeo ilivyo sasa kuna upande mmoja unajiona uko sahihi sana kwa kila kilichotokea na ni kwa sababu hawajui undani wa mipango iliyokuwepo.

Serikali lazima ifanye reforms za haraka kwa baadhi ya maeneo kulingana na demand na impact ionekane ndani ya muda mfupi.
 
Roho za marehemu wote zisitulie Hadi zilipe kisasi cha yale waliyofanyiwa ya uonevu. Damu zao zikawalilie waliokatisha uhai wao wasiwe na Amani. Sizani kama raisi aliwatuma wakaue watu wasio na hatia wala wazo la luandamana majumbani mwao.
May their souls never settle until the revenge is paid
 
Kutegemea demage control kutoka mataifa ya kigeni ni kujidanganya na kujitengenezea mazingira ya kutawaliwa kuliko livyo sasa....

Unadhani ni wangapi wamekufa mwaka huu kwa machafuko ya kisiasa... Yani Mmarekani aitoe CCM madarakani na anamikataba ya gesi Mtwara😂 na possibly kama Jeshi lulitachukua washaona kilichotokea kwa Mfaransa kule Bukinabe.

Kuliingiza jeshi mkenge kutawala Tanzania ni kujadili upuuzi na wakijidanganya kufanya hivyo wataona maana halisi ya CCM NA MIFUMO YAKE NCHINI..... Namaanisha Hivi ilipaswa kuiparalaiz CCM kwa mpango wa muda mrefu kwanza ndipo lifuate suala la maandamano.

Na kwasababu imeshafanyika attemp ccm inarudi kujipanga upya 2030 upinzani utashangazwa.

Aidha, Kama nchi imefahamika shida ilikua wapi na wapi tuliteleza ni muda wa kujijenga upya.

Ila........

Lazima kila upande ukiri kukosea na wananchi wawe tayari kupokea matokeo ilivyo sasa kuna upande mmoja unajiona uko sahihi sana kwa kila kilichotokea na ni kwa sababu hawajui undani wa mipango iliyokuwepo.

Serikali lazima ifanye reforms za haraka kwa baadhi ya maeneo kulingana na demand na impact ionekane ndani ya muda mfupi.
Kuisubiri serikali ifanye reforms zinazowanufaisha wananchi ni sawa na kusubiri meli uwanja wa ndege. Kumbuka kuwa haki haiombwi bali hupokonywa hata ikibidi kwa kumwaga damu.

Kusema kuwa CCM itajipanga 2030 wakati roho za maelfu ya watanzania zimepotea ni kujidanganya. Hakuna kitu kinachoweza kuwasahaulisha watanzania kuhusu haya mauaji haya ya kimbari.

Hiki walichofanya CCM ni sawa na kutega bomu. Siku likilipuka hakuna atakayebaki salama.
 
Walimpiga coz alituchamba waandamanaji [emoji81][emoji81]
Polisi wengi walifanya hivyo ili kumponza boss wao achafuke zaidi, kuna mambo kuyaelewa ni ngumu km huna jicho la kuona mbali..!!
Hapa sijakuelewa mkuu, ukiachana na Sharif kada wa CCM kuna raia kibao ambao sio makada wa CCM na wala hawakuwa katika maandamano lakini wameuliwa pasipo na sababu zozote. Tena ni wengi mno
 
Kuisubiri serikali ifanye reforms zinazowanufaisha wananchi ni sawa na kusubiri meli uwanja wa ndege. Kumbuka kuwa haki haiombwi bali hupokonywa hata ikibidi kwa kumwaga damu.

Kusema kuwa CCM itajipanga 2030 wakati roho za maelfu ya watanzania zimepotea ni kujidanganya. Hakuna kitu kinachoweza kuwasahaulisha watanzania kuhusu haya mauaji haya ya kimbari.

Hiki walichofanya CCM ni sawa na kutega bomu. Siku likilipuka hakuna atakayebaki salama.
Vipi kwenu huko Rwanda mauaji ya kimbari bado mnayakumbuka? Mbona Kagame bado anatawala wakati wanasema ndie alisababisha mauaji hayo?
 
Back
Top Bottom