PostGE2025 Ushahidi wa mauaji kwa watu wasiohusika na maandamano

PostGE2025 Ushahidi wa mauaji kwa watu wasiohusika na maandamano

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Awali ya yote napenda kuweka wazi kuwa sishabikii maandamano wala mauaji ya raia wasiokuwa na hatia. Niliyoshuhudia au kusimuliwa na watu kuhusu maauji ya baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025 yanahuzunisha sana na yamenifanya niamini kuwa jeshi la polisi Tanzania linafanya kazi kitutusa sana.

Nimeanzisha uzi huu ili tupeane updates kuhusu kilochojiri kwenye maeneo yetu ili kuthibitisha ukiukwaji wa maadili uliofanywa na jeshi la polisi kwa raia wasiokuwa na hatia. Katika eneo nililopo watu wengi sana waliouliwa hawakuwa na hatia na wala hawakuhusika kwenye maandamano. Pamoja na kuzimwa kwa huduma ya internet na wananchi kuzuiliwa kufanya shughuli zao za kiuchumi, ni dhahairi wananchi mmeshuhudia mauaji holela katika maeneo yenu ambayo yangeweza kuepukika ikiwa polisi wangetumia busara na weledi.

Matukio ya kipuuzi na yasiyokuwa na chembe ya utu ambayo nimeshuhudia au kusimuliwa na wananchi wakati nikichukua takwimu za mauaji ni mengi lakini naomba niweke haya machache kwa kuwa mengi yanafanana na haya.

1. Polisi waliingia kwenye kituo cha watoto wanaojifunza mpira (football academy) wakati watoto hao wakijifunza kwa vitendo mambo ya mpira kwenye runinga, wakawaua watoto 7 kwa risasi papo hapo.

2. Katika tukio lingine, polisi waliokuwa wakirandaranda huku na huku walifika kwenye baa moja na kuwakuta watu wakinywa pombe. Wakamuita mzee mmoja akatoka nje kabla hajafika mbali wakampiga risasi kifuani akafia palepale.

3. Polisi waliwakuta vijana dukani wakiwa kwenye foleni ya kununua bidhaa, wakawaamrisha walale chini kifudifudi bila kujitikisha. Wakawapiga risasi za kisogoni wote kisha wakapakia maiti kwenye gari wakaondoka nazo.

4. Polisi walivamia genge la mama ntilie mmoja, wakawatawanya raia waliokuwa wakila chakula kwa kuwarushia risasi za moto. Risasi ikampata mama ntilie ikampasua kichwa akafia palepale.

5. Polisi walipita mtaani wakawakuta wanafamilia wameketi nje ya nyumba yao wanajipatia chakula cha jioni, wakwarushia risasi mfululizo na kufanikiwa kumuua baba wa familia na mtoto wake mmoja papo hapo.

Kwa mifano hiyo michache ni wazi kuwa polisi wa Tanzania hawana weledi kabisa wa kikazi. Hata kama walipewa maagizo ya kuua raia kwa risasi za moto, hakukuwa na haja ya kuwaua raia wasiokuwa na hatia kwa kuwapiga risasi ovyo. Kwa takwimu hizi za kusimuliwa na kushuhudia mwenyewe, ni dhahiri wananchi wengi waliouawa hawakuwa kwenye maandamano na wala walikuwa hawafanyi vurugu yoyote. Fikiria watu wako kwenye shughuli zao lakini wanauliwa bila sababu za msingi.

Tumekuwa tukishuhudia kwingineko duniani polisi wakituliza maandamano lakini siokwa staili hii ya polisi wa Tanzania. Inasikitisha sana. Hizi roho za wananchi wasiokuwa na hatia zilizozimwa na polisi haziwezi kupita bure.

Je, eneo ulilopo kuna tukio gani la mauaji ya ovyo uliloshuhudia? Tunataka tukusanye matukio ya kutosha ili watetea haki za binadamu na ICC wazitumie kama reference ya kuichukulia hatua serikali ya Tanzania kwa mauaji haya ya halaiki.
Saddam aliuawa kwa kuua watu 148 tu. Na aliuawa kwa makosa aliyofanya miaka 24 nyuma

Saddam was sentenced to death by hanging, after being convicted of crimes against humanity by the Iraqi Special Tribunal for the Dujail massacre—the killing of 148 Iraqi Shi'ites in the town of Dujail, in 1982, in retaliation against an attempt on his life.
 
Walitusaliti hao watanzania wenzao wakajua watakuwa salama..!!
Ndiomana tunawaambia unafki ni kitu kibaya, hapo alitoka ili ashuhudie tunavyouliwa matokeo yake kala chuma yeye familia yao 😹
Ni huzuni kwa kweli
 
Jumla ya Watanganyika waliouwawa ili Samia aendelee kuitawala Tanganyika ni zaidi ya 10,000.
 
Hivi nyie kwa akili zenu mnafikiri polisi walipiga kwa bahati mbaya 😹😹

Kuna people zilifatwa mpk ndani, km huyo Sharif majini aliondoka katiki 🤣
Jamaa saiz anatafuna bikira zake tu huko firidaus
 
Watupe taarifa siku ya arobaini yake tukafinye cha mtume..!!

Wali wa wanafki unanoga sana!!
Nitajitolea kupika siku hiyo wali ujae mafuta uwe mtamu. 😹
Huo wali wa kwenye 40 za hao jamaa usile

Sikushaul kabisa
 
K
Umetumia mara nyingi sana kwenye mada yako neno hili "polisi".

Naomba tu kujuwa uhakika wako kuwa hawa kweli walikuwa ni polisi. Walikuwa kwenye nguo zao za kikazi zinazofahamika?

Hapa naomba ujue tu kuwa sina sababu hata moja ya kutetea jeshi la polisi la Tanzania.; kwani maovu yao yanajulikana hata kabla ya hili la kuua waTanzania 'indiscriminately', kama ulivyo eleza hapa.
Kwani silaha walibeba wananchi au policcm?
 
Tukumbuke weeks/a month back Mange kimambi alitoa taarifa juu ya kuingizwa kontena lenye silaha ambalo halinasibishwi na Majeshi yetu(taarifa kama hii ilipuuzwaje)
Na ndiyo sababu akina Hamza Johari, hata kabla hawajavuta hewa baada ya uteuzi, jambo la kwanza ni kumfikiria Mange.
Maana yake ni kwamba Mange katoa siri za ndani zinazowakosesha utulivu wa akili..
Hawa wote ni lazima wawajibishwe kwa maovu waliyo wafanyia waTanzania.
 
Hebu tupia humu tuzione mkuu.
Mada hii hapa, iliyowekwa na mkuu 'Waufukweni': "Picha, Sura za wanaodaiwa ni askari walioshiriki kuua maelfu ya watanzania". Ni mada ya juzi tu, ni rahisi kuipata chini ya jina la 'Waufukweni'.
Sidhani kama kulikuwa na kitu kama hicho mkuu. Ni ushenzi tu wa polisi katika matumizi ua ovyo ya silaha
Anayosema, mkuu 'r2ga usiyabeze (dismiss) bila kuyapa fikra zaidi..
Mara nyingi pamekuwepo na mauaji yanayotokana na uchaguzi haramu huko visiwani, hasa Pemba. Hali hiyo inaweza kuwa pia ni kichocheo cha kufanya hivyo hivyo huku Tanganyika. It may be far fetched, but not too easily dismissed.
 
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mianzini kata ya makurumla jimbo la ubungo kwa tiketi ya ccm mr njele,wamemzika ijumaa iliyopita,alikula shaba ya shingo akiwa amesimama pale shule ya msingi ya mianzini mburahati
Sasa mburahati si ni mbali na Barabara kuu? Watu waliandamanaje mitaani?
 
Mada hii hapa, iliyowekwa na mkuu 'Waufukweni': "Picha, Sura za wanaodaiwa ni askari walioshiriki kuua maelfu ya watanzania". Ni mada ya juzi tu, ni rahisi kuipata chini ya jina la 'Waufukweni'.

Anayosema, mkuu 'r2ga usiyabeze (dismiss) bila kuyapa fikra zaidi..
Mara nyingi pamekuwepo na mauaji yanayotokana na uchaguzi haramu huko visiwani, hasa Pemba. Hali hiyo inaweza kuwa pia ni kichocheo cha kufanya hivyo hivyo huku Tanganyika. It may be far fetched, but not too easily dismissed.
Sure ni Kama vile walikua na kisasi waliisubili hii nafasi kwa muda mrefu sana
 
Saddam aliuawa kwa kuua watu 148 tu. Na aliuawa kwa makosa aliyofanya miaka 24 nyuma

Saddam was sentenced to death by hanging, after being convicted of crimes against humanity by the Iraqi Special Tribunal for the Dujail massacre—the killing of 148 Iraqi Shi'ites in the town of Dujail, in 1982, in retaliation against an attempt on his life.
Kwanini huyu yeye asiuawe. Hii dunia haina usawa.
 
Sio kuwatuma wawakilishi wenu bungeni wafikishe hayo matakwa.
Hao wawakilishi hawakuchaguliwa na watu kwa kuwa hakukuwa na uchaguzi. Wawakilishi wanajiwakilisha wenyewe na familia zao. Hawakuwakilishi wewe na familia yako mkuu.
 
Hivi hakuna wazee wenye busara kweli , wakemee vikali haya yaliyotokea kila mtu yupo kimya kulinda ugali wake ,

Hichi kilichotokea hata Makaburu wanatushangaa,sisi ndiyo tulikuwa tunalaani vikali vitendo vya makaburu dhidi ya watu weusi lakini angalia leo hii nini tunafanya.

Waliohusika wanapaswa kuwajibishwa haraka sana tusioneane aibu.
wangesikiliza ushauri wa mzee warioba na kuufanyia kazi yote haya yasingetokea waliamini kwenye kiburi na ubinafsi
 
Back
Top Bottom