Pre GE2025 Ushauri: Abdul aende mahakamani kumshtaki Lissu ili kujisafisha na tuhuma za RUSHWA zinazoelekezwa kwake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Odemba, StarTV: "Mh. Tundu Lissu, wewe ni mwanasheria. Tuhuma zako zinapaswa kuwa na ushahidi. Kuna hata footage ya CCTV camera ingalau..?"

Tundu Lissu: ".......Wala!, hakuna CCTV camera nyumbani kwangu. Ndiyo, Mimi ni mwanasheria. Na katika sheria ya ushahidi inasema ushahidi bora ni ule wa shahidi kuona mwenyewe au kusikia au kunusa mwenyewe. Mimi mwenyewe niliona na kusikia yote haya..."

✍️Mpaka hapo huyo Abdul asifikiri kabisa kuwa hakuwa recorded kwa sauti au kwa picha...!

✍️Msidanganyike, kwa Tundu kuna vichukua picha na sauti vya kutosha. Akirogwa tu kuingia huko mahakamani, atalambishwa mchanga asubuhi tu...!

##Mwisho nakupa homework. Tazama body language ya TL wakati anapojibu swali hilo utaelewa ni kwanini huyo jamaa ni very tricky...
 
Ila Lissu kiboko, pamoja na kuchangiwa ml 5 pale furahisha lakini Bado hanyamazi.

Ama Kweli, Lisuu hajawahi kunyamazishwa!!
Kingine ni hiki, huyo Abdul ukiacha kuwa ni mtoto wa Rais lakini uwezo wake kichwani ni mdogo sana, siyo Intelijenti, amerekodiwa kwenye matukio mengi ya hovyo sana, ni kama hana mwongozo wowote.

Ni bahati yake kwamba Mama yake ni Rais, ila huko mbele ataanikwa kwenye kila uchafu wake
 
Muacheni Abdul aende mahakamani yote yakajulikane huko.
 
Anaweza kuzitumia mahakama kumsafisha Kwa kudai fidia kama Ile ya Manji dhidi ya Mengi!!
Kwa vyovyote vile Lisu atakuwa ana ushahidi mzuri wa kuithibitishia mahakama kuwa Abdul alifika nyumbani kwake.
 
Kwanini Lissu naye asiende kumshtaki Abdul kwa kutoa rushwa?
 
Kwa vyovyote vile Lisu atakuwa ana ushahidi mzuri wa kuithibitishia mahakama kuwa Abdul alifika nyumbani kwake.
Sasa kufika nyumbani Si ushahidi wa RUSHWA, yaezakuwa alikuja kujadili mambo ya Simba na Yanga.

Cc: johnthebaptist
 
Kwanini Lissu naye asiende kumshtaki Abdul kwa kutoa rushwa?
Hiyo ni KAZI ya TAKUKURU.

By the way RUSHWA ilikataliwa, hivyo mtuhumiwa alirudi na pesa nyumbani.
 
Ataweza maswali ya Kibatala au ndio tumbo la kuhara litaabza kama la Yule polisi?
 
amshitaki kwa kosa gani? kwamba alimpa lissu hela akakataa?
 
Amtaje kwa majina yake yote Matatu. Bila hivyo, mahakamani atamruka!!!
Lissu mjanja mjanja sana kwenye mambo haya ya Sheria.

Bora Abdul akaebtu kimya, maana Kwanza Abdulnwapo wengi Nchi hii,

Hata Yule Nondo wa ACT ni Abdul pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…