Ushauri: Anataka kuacha kazi Serikalini sababu ya maslahi madogo

Ajilipue tuu lakini ajue kitaa kigumu sana! Afanye maamuzi sahihi asije akaja kujuta maana majuto ni mjukuu
 
Avumilie kwa muda tu akishaa thibitishwa kazini aende achukue mzigo afanye mambo yake
 
Umeelezea madaktari na ualimu, halafu ukaelezea ualimu. Ualimu sawa , ila madaktari wana nafuu, na si kweli kazi zote serikalini hazina malipo mazuri, zipo kada wanalipwa vizuri sana.
Mwambie huyo bwana kama anataka kuacha ahakikishe ana chanzo kingine , else atarudi square one hali itakuwa mbaya zaidi
 
una wazo kama langu..jambo la msingi ni kujipanga huku ukiwa unaangalia unapotaka kwenda...mfano anzisha ofc Yako ukiona imekaa sawa unaweza kufanya maamuzi lakini kama bado usifanye maamuzi ya kuacha kwanza
 
Sasa huko bush watu wamaana ndio hao, walimu, manesi, polisi, mtendaji kata, halmashauri ndo vibosile kabisa 😹😹😹
Sasa huko bush watu wamaana ndio hao, walimu, manesi, polisi, mtendaji kata, halmashauri ndo vibosile kabisa 😹😹😹
Kuna dada humu nilisikia analalamika ana bahati mbaya ya kutongozwa na wanaume below standard kumbe mchawi location.

Inasikitisha kwakweli, kuna kabinti mtaani kamepangiwa huko Kibondo Kigoma na ameshazalishwa tayari.

Halafu kinachobowa ni bora mtu wa kuanzisha naye familia lakini wengi wanazaa tu yani wanaume wanakuwa hawana future plan nao.
 
Yeye aendelee na hiyo kazi huko huko na akamate fursa ya kuuza huduma ambazo hazipatikani huko. Akiacha kazi atakuwa mzigo kwa ndugu, rafiki, na jamaa. Aache kazi akishapata kazi nyingine.
 
Mi pia aisee☹️🤣🤣
Nakumbukaga starehe ya weekend 🤣🤣🤣

Alikuwepo mtumishi babu mmoja ndo anakaribia kustaafu, basi kila weekend anapiga simu babuu jiandae nakuijia, ananipitia ananibeba kwenye baiskeli tunaenda mnadani bia na nyama jioni ananirudisha kwangu huu ndo mtoko wa maana 😹😹😹

Kuna kero kijijini ila raha zake ni za ukweli
 
Jamii itakuwa na mawazo mgando. Kinachomshinda huyu mwalim anaishi kwa kujilinganisha na aliosoma nao au watu wake wa karibu. Anaona amechelewa.
 
Kubebwa na baiskeli Tena!?🤭🤣🤣...mie niliponea chupuchup kuzabwa vibao na nyani ...nilikuwa na kibustani bondeni Cha figiri na Chainiz........kufika kule nakuta wamevamia kishamba Cha jirani yangu lilikuwa na njegere...si nikajifanya kuwafukuza bhana!....Weee,vikanionesha ishara ya "Utakula makofii!" Nilivyokimbia hata sielewi nilifikaje home peku🙌
 
Usiache kazi kwasababu ya maslai duni. Ila acha kama upo na mchongo mzuri kuliko hiyo kazi.

Hata hivo, Kazi inaweza kua ni assets ya wewe kupata mkopo na kufanya hizo biashara, kama kweli ni mfanya biashara, mambo ya kichanganya unasepa
 
Sa usafiri wa huko nini tena ndugu, ni mwendo wa baiskeli....tena wananishawishi namie nijifunze, kimoyomoyo najisemea tu mmh na utu uzima huu nije nivunje kiungo najifunza baiskeli akaaaah!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…