Ushauri: Anza hata na chumba na sebule. Nyumba kubwa inatesa

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
📖MHADHARA WA 16:
Baada ya kununua kiwanja......
Ukibahatika tena kupata vihela kidogo ni bora kuanza kujenga CHUMBA + SEBULE + CHOO. Kama hela zako ni za msimu au hela za kulenga kwa manati usijenge nyumba kubwa, kwasababu inaweza kukutesa kwenye harakati za kuimaliza. Wabongo wana msemo wao wanasema; "Ujenzi wa nyumba unaanza kutesa wakati wa kuanza matumizi ya lugha ya kiingereza" - Yaani wanamaanisha kuanza harakati za kupaua hadi kumaliza.

Wengi wanateswa sana na ujenzi wa nyumba kubwa unakuta pesa inakatika katikati ya ujenzi, hatimaye jengo linabaki kuwa pagala kwa zaidi ya miaka 5 hadi 10. Ujenzi wa nyumba kubwa unatesa hasa kwa wale wanaotumia mikopo ya benki kwa ajili ya kujenga. Ujenzi wa "kuvuta pumzi" ni mgumu sana kwasababu kila pumzi unayovuta ukiipata inakutana na ada za watoto, ugonjwa, kodi ya nyumba, huduma za ndani, n.k.

Baadhi ya mafundi wa nyumba ambao wanayajua maisha ya kubangaiza huwa wanawashauri watu kuanza kujenga nyumba ya nyuma (CHUMBA + SEBULE + CHOO) - Ni nadra sana kukutana na mafundi watakaokushauri hivyo. Ukizingatia ushauri wao utafanikiwa kuhamia kwako mapema, nyumba ya mbele (nyumba kubwa) utaijenga taratibu ukiwa papo hapo kwako.

RIGHT MARKER,
Dar es salaam,
24/09/2024.
 
Chumba sebule choo inaweza kukucost kiasi gani hadi kuhamia?
 
Kwa Gharama ya kawaida 8m mpaka 9 Kijumba kizuri tu.
Na kwa Gharama ya Juu, ukikiremba sana kijumba 15m.
Chumba cha kulala 10Fut kwa 11Fut Choo 4Fut kwa 5Fut Sebre ile 11Fut kwa 11Fut.
Hata usipo usipo weka tailils utahamia kwa sakafu tu ya kawaida
Note: Bati nunua za Migongo midogo 30G.
usichukue Bati za Migongo mpana, Zina washinda mafundi wengia Nyumba inawai kuvuja.
 
Bahati mbaya mtu akisema ajenge hiyo ya uwani kwanza then aje kujenga nyumba ya ndoto zake mpaka anakuja kuzeeka atakachokuwa amefanikiwa ni kununua tofali anazipanga nje kwake zikinyeshewa mvua na kubadilika rangi lakini hakuna cha kuanza ujenzi tena wala nini.

Hili lieleweke tu kwamba kila mtu atamiliki alichopangiwa wewe anza ujenzi kama ni nyumba kubwa au ndogo utakapoishia ni hapo hapo muhimu anza ujenzi lakini kama unapumua na bado unapambana utaishi kwenye nyumba uliyoitaka.
 
Kuwai kujenga nako tatizo akili inalala sana nakumbuka nilijenga nikiwa na miaka 25 kilichofuata mambo yalikuwa magumu kushika m1 ilikuwa kaz nilipofika30 nikauza nyumb yenyewe nikaenda kupanga na kununua eneo pemben ya mji kwa bei cheep kwaajil ya kufugia so baada ya mwaka nikajikuta uchumi umekua na nimenunua viwanja vya kutosha na kujenga nyumb ya ndoto yangu lakin ndugu waliniambia umeuza nyumb unaenda kupoteana
 
Motivation speaker hamkosekani kila sehemu mpo

Eti baada ya mwaka uchumi ukaimarika........ 🤣😂
 
Ushauri mzuri Sana huu.Mjumba Mkubwa ulinitesa Sana maana ulichukua Miaka 7 Kuukamilisha,huku nikiwa nishakopa.Yaani unakopa,Nyumba haiishi na Pesa zimekata,na bado unapanga.Lakini yote Kwa yote ili usipoteze mwelekeo Kama kiwanja Kikubwa angalau anza na Nyumba ndogo ambayo bàdaye itakuwa servant quarter au utaipangisha Kwa familia changa.Weka dermacation ya kutosha ili Kupunguza mwingiliano na Mpangaji.Na mbeleni ukiwa mzee unarudi kukaa nyumba ndogo alafu ile kubwa utaipangisha.Hesabu rahisi maana ukiwa mzee utabaki na mkeo au mumeo,watoto wakishamaliza Chuo wanaondoka.Siku hizi watoto wako radhi wakae geto lakini wawe huru.
 
Kwa Gharama ya kawaida 8m mpaka 9 Kijumba kizuri tu.
Na kwa Gharama ya Juu, ukikiremba sana kijumba 15m.
Chumba cha kulala 10Fut kwa 11Fut Choo 4Fut kwa 5Fut Sebre ile 11Fut kwa 11Fut.
Hata usipo usipo weka tailils utahamia kwa sakafu tu ya kawaida
Note: Bati nunua za Migongo midogo 30G.
usichukue Bati za Migongo mpana, Zina washinda mafundi wengia Nyumba inawai kuvuja.
Thanks
 
📖MHADHARA WA 16:
Baada ya kununua kiwanja......
Ukibahatika tena kupata vihela kidogo ni bora kuanza kujenga CHUMBA + SEBULE + CHOO. Kama hela zako ni za msimu au hela za kulenga kwa manati usijenge nyumba kubwa, kwasababu inaweza kukutesa kwenye harakati za kuimaliza. Wabongo wana msemo wao wanasema; "Ujenzi wa nyumba unaanza kutesa wakati wa kuanza matumizi ya lugha ya kiingereza" - Yaani wanamaanisha kuanza harakati za kupaua hadi kumaliza.

Wengi wanateswa sana na ujenzi wa nyumba kubwa unakuta pesa inakatika katikati ya ujenzi, hatimaye jengo linabaki kuwa pagala kwa zaidi ya miaka 5 hadi 10. Ujenzi wa nyumba kubwa unatesa hasa kwa wale wanaotumia mikopo ya benki kwa ajili ya kujenga. Ujenzi wa "kuvuta pumzi" ni mgumu sana kwasababu kila pumzi unayovuta ukiipata inakutana na ada za watoto, ugonjwa, kodi ya nyumba, huduma za ndani, n.k.

Baadhi ya mafundi wa nyumba ambao wanayajua maisha ya kubangaiza huwa wanawashauri watu kuanza kujenga nyumba ya nyuma (CHUMBA + SEBULE + CHOO) - Ni nadra sana kukutana na mafundi watakaokushauri hivyo. Ukizingatia ushauri wao utafanikiwa kuhamia kwako mapema, nyumba ya mbele (nyumba kubwa) utaijenga taratibu ukiwa papo hapo kwako.

RIGHT MARKER,
Dar es salaam,
24/09/2024.
Sahihi
 
Kwa Gharama ya kawaida 8m mpaka 9 Kijumba kizuri tu.
Na kwa Gharama ya Juu, ukikiremba sana kijumba 15m.
Chumba cha kulala 10Fut kwa 11Fut Choo 4Fut kwa 5Fut Sebre ile 11Fut kwa 11Fut.
Hata usipo usipo weka tailils utahamia kwa sakafu tu ya kawaida
Note: Bati nunua za Migongo midogo 30G.
usichukue Bati za Migongo mpana, Zina washinda mafundi wengia Nyumba inawai kuvuja.
Ukifuata hizi hesabu za humu unaweza usianze hata msingi kwa woga

Mkuu chumba na sebure mil15? Maeneo gani huko wenye gharama kubwa hivyo
 
Mzee wangu alipingana na hiyo dhana,nyumba yake ya ujanani ni kubwa sana la kiume,ukianza na chumba na sebule,utafiamo humo,hutajenga kubwa
Bahati mbaya mtu akisema ajenge hiyo ya uwani kwanza then aje kujenga nyumba ya ndoto zake mpaka anakuja kuzeeka atakachokuwa amefanikiwa ni kununua tofali anazipanga nje kwake zikinyeshewa mvua na kubadilika rangi lakini hakuna cha kuanza ujenzi tena wala nini.

Hili lieleweke tu kwamba kila mtu atamiliki alichopangiwa wewe anza ujenzi kama ni nyumba kubwa au ndogo utakapoishia ni hapo hapo muhimu anza ujenzi lakini kama unapumua na bado unapambana utaishi kwenye nyumba uliyoitaka.
Mnaandika kama ni kanuni. Inategemea malengo ya mtu na kipato chake.
 
Ukifuata hizi hesabu za humu unaweza usianze hata msingi kwa woga

Mkuu chumba na sebure mil15? Maeneo gani huko wenye gharama kubwa hivyo
Kasema 8-9m ukikiremba sana ndio 15m. Ni kweli ukinogewa kuweka vitu vya gharama unaweza kutumia gharama kubwa kujenga hadi watu wakakushangaa. Kumbuka chumba na sebule mtu anaweka na jiko pia sio chumba na sebule kama police post.
 
Back
Top Bottom