RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
📖MHADHARA WA 16:
Baada ya kununua kiwanja......
Ukibahatika tena kupata vihela kidogo ni bora kuanza kujenga CHUMBA + SEBULE + CHOO. Kama hela zako ni za msimu au hela za kulenga kwa manati usijenge nyumba kubwa, kwasababu inaweza kukutesa kwenye harakati za kuimaliza. Wabongo wana msemo wao wanasema; "Ujenzi wa nyumba unaanza kutesa wakati wa kuanza matumizi ya lugha ya kiingereza" - Yaani wanamaanisha kuanza harakati za kupaua hadi kumaliza.
Wengi wanateswa sana na ujenzi wa nyumba kubwa unakuta pesa inakatika katikati ya ujenzi, hatimaye jengo linabaki kuwa pagala kwa zaidi ya miaka 5 hadi 10. Ujenzi wa nyumba kubwa unatesa hasa kwa wale wanaotumia mikopo ya benki kwa ajili ya kujenga. Ujenzi wa "kuvuta pumzi" ni mgumu sana kwasababu kila pumzi unayovuta ukiipata inakutana na ada za watoto, ugonjwa, kodi ya nyumba, huduma za ndani, n.k.
Baadhi ya mafundi wa nyumba ambao wanayajua maisha ya kubangaiza huwa wanawashauri watu kuanza kujenga nyumba ya nyuma (CHUMBA + SEBULE + CHOO) - Ni nadra sana kukutana na mafundi watakaokushauri hivyo. Ukizingatia ushauri wao utafanikiwa kuhamia kwako mapema, nyumba ya mbele (nyumba kubwa) utaijenga taratibu ukiwa papo hapo kwako.
RIGHT MARKER,
Dar es salaam,
24/09/2024.