Ushauri: Awamu Moja Kwa Mbunge inatosha kabisa, wananchi tunahitaji changamoto mpya.

Si ubaguzi huo,

Mbona Urais una ukomo, iweje ubunge usiwe na ukomo?
wabunge wa bunge gani hao ambao hawana ukomo gentleman :pedroP:

na kama unahitaji kuwakomesha, si uungane na wananchi kule jimboni kwanye kura mmnamkomesha huyu msiyo muhitaji na kumuinua yule mnae muhitaji awaongoze, lakini sio kwa chuki na gubu ila kwa kura:BASED:
 
Kwa mawazo Yako, hata nafasi ya ubalozi usingepata, shukuru huishi mtaa ninaoushi.
gentleman,

mambo haya ni kujipanga bana,

na mim niko rada halafu niko chonjo mbaya sana aise..

tatatatatata aise..acha kabisa:pedroP::pedroP:
 
Je bunge lina umuhimu gani kwanini tusitengeneze bunge dogo la Kikanda

Mfano mbunge wa kaskazini ,mbunge wa pwani n.k

Sioni mantiki yakuwa na wabunge wengi ambao hawana uwezo wa kuisaidia nchi.

Then ubunge iwe kazi MTU anaomba na anafanya interview utumishi na awe angalau Ana elimu ya diploma
Unazd kubania ajira za raia. Mi nilipenda wabunge wapatikane kama wagombea huru, wasitokane na chama ili kupunguza au kuondoa wapiga makofi tu bungeni na kusifia mtu. Bajeti nzima imejaa neno Samia kuliko mwananchi.
 
Hawewezi kukuelewa hawa ccm. Kwa mfano nje ya siasa:-
1. Jenista Mhagama, Margret Sitta na mama Salma Kikwete ni walimu wa mwandiko darasa la kwanza.
2. Msukuma na Maganga ni watekaji wa mabasi.
3. Simbachawene na Lusinde ni makondakta wa daladala.
4. Ongezea na wewe
Wabunge wangepatikana kikanda tusingekuwa na wabunge wengi wasio na TIJA.

Wabunge 150 wanetosha kabisa.

Mawaziri wasitokane na wabunge. Mawaziri na Baraza Zima wasizidi 30.

Tungekuwa mbali sana ingawa Bado hatujachelewa!!
 
Yes!! Hata mm ya mawaziri kutokana na wabunge bado inashindwa kuleta tija ya mihimili mitatu ya serikali.
 
Wabunge 150 wanetosha kabisa.
Mm hata hao wabunge 150 nawaona ni wengi. Tulipaswa kuwa na wabunge wawili kila mkoa wa Tanzania bara (mmoja KE na mwingine ME), halafu wabunge 4 toka Zanzibar (2 toka Unguja na 2 toka Pemba).

Mikoa 26 Tanzania bara = wabunge 52 ongeza wabunge 4 wa visiwani, jumla tungekuwa na wabunge 56 tu.
 
Ingekuwa pia sana hii.

Na wabunge wanawake wasiwe viti maalum, wapambane Hasa Kwa uwezo kuwapata.

Nchi ingeokoa sana mapato.
 
Salaam, Shalom!!

Miaka mitano, ni muda unaotosha kabisa kutimiza kusudi na malengo na KAZI ambayo mbunge amepewa na wananchi.

Ikiwa miaka mitano pekee, ya Rais Magufuli, ilitosha kuonyesha matokeo makubwa kuliko waliokaa miaka kumi, iweje mbunge ashindwe kudeliver Kwa miaka mitano?

Kwa kuwa life expectancy imepungua, na wapo wengi wenye ndoto ya kuonyesha makubwa Kwa nafasi ya ubunge, mitano inatosha kabisa.

FAIDA ZA UKOMO WA WABUNGE.

1. RUSHWA ITAPONGUA MAJIMBONI.

Hivi tunavyoongea, wabunge vilaza wanachukua mikopo kwenye MABENKI Ili kupata pesa za kuja kuhonga wananchi maskini, pakiwepo ukomo, wananchi watakuwa salama.

2. WIMBI LA MATAJIRI WAFANYABIASHARA LITAPUNGUA KUUNGIA BUNGENI.

Hawa matajiri wafanyabiashara wenye kutupandishia Bei za mafuta na sukari, watakoma kutuhujumu pakiwa na ukomo wa ubunge.

3. DHARAU ITAPUNGUA KWA WANANCHI.

Hapa wananchi wataichagua Kila baada ya miaka mitano mtu wao Kwa Umakini mkubwa atakaowatumikia.

NB: Mbunge akitaka kuendelea Awamu ya pili, agombee Jimbo lingine.

Ushauri: Wabunge wote Walio bungeni, wapumzishwe, tupate wabunge wapya kabisa, na mchakato wa kuwapata uende mbali zaidi ya upeo na mipaka ya vyama wanavyotoka,

Nawasilisha🙏

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿. Amen
Tuseme uko sawa. Pendekezo lako hili linatekelezwaje? Mhusika au wahusika wenye wajibu wa kuhakikisha linatekelezwa ni akina nani? Kwa mfumo gani? (By what mechanism?).
 
Ni Kwa Kupambana Katiba mpya itokanayo na Rasimu aliyosimamia Judge Warioba.

Tupate Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.
 
Ikiwa ni muumini wa Katiba mpya, nitashangaa ukipingana nami,

Rasimu ya judge Warioba, wananchi wengi walipendekeza ukomo wa wabunge.

Ikiwa anapenda aendelee, akagombee Jimbo lingine.
Walipendekeza pia kura ya kutokuwa na Imani na Mbunge.

Ninachokiona Mimi kwenye ukomo wa Mbunge ni kwamba yeye ni mwakilishi na siyo Mkuu wa nchi ama Serikali kama alivyo Rais.

Ukomo wa rais umewekwa kuzuia mtu kushika Dola kama mali yake binafsi. Lakini uwakilishi hakuna haja ya kuweka ukomo.

Marekani wabunge hawana ukomo ila Rais ana ukomo. Uingereza kwa kuwa Waziri Mkuu si Mkuu wa nchi hakuna ukomo.

Ujerumani Kansela siyo Mkuu wa nchi Kwa ivo hakuna ukomo. Hapa kwetu Rais ni Mkuu wa nchi na ni Mkuu wa Serikali pia.
 
Agency principal ni Kwa wote.

Rais pia ni muwakilishi wa wananchi.

Nchi zilizoendelea sawa, ila huku kwetu, ukomo na kufutwa KAZI wakati wowote akiwa ndani ya uwakilishi ni muhimu sana.
 
Ni Kwa Kupambana Katiba mpya itokanayo na Rasimu aliyosimamia Judge Warioba.

Tupate Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.
Katiba mpya ndiyo iwe na kipengele cha mhula mmoja kwa ubunge? Itapitishwa na watu gani?
 
Salaam, Shalom!!

Miaka mitano, ni muda unaotosha kabisa kutimiza kusudi na malengo na KAZI ambayo mbunge amepewa na wananchi.

Ikiwa miaka mitano pekee, ya Rais Magufuli, ilitosha kuonyesha matokeo makubwa kuliko waliokaa miaka kumi, iweje mbunge ashindwe kudeliver Kwa miaka mitano?

Kwa kuwa life expectancy imepungua, na wapo wengi wenye ndoto ya kuonyesha makubwa Kwa nafasi ya ubunge, mitano inatosha kabisa.

FAIDA ZA UKOMO WA WABUNGE.

1. RUSHWA ITAPONGUA MAJIMBONI.

Hivi tunavyoongea, wabunge vilaza wanachukua mikopo kwenye MABENKI Ili kupata pesa za kuja kuhonga wananchi maskini, pakiwepo ukomo, wananchi watakuwa salama.

2. WIMBI LA MATAJIRI WAFANYABIASHARA LITAPUNGUA KUUNGIA BUNGENI.

Hawa matajiri wafanyabiashara wenye kutupandishia Bei za mafuta na sukari, watakoma kutuhujumu pakiwa na ukomo wa ubunge.

3. DHARAU ITAPUNGUA KWA WANANCHI.

Hapa wananchi wataichagua Kila baada ya miaka mitano mtu wao Kwa Umakini mkubwa atakaowatumikia.

NB: Mbunge akitaka kuendelea Awamu ya pili, agombee Jimbo lingine.

Ushauri: Wabunge wote Walio bungeni, wapumzishwe, tupate wabunge wapya kabisa, na mchakato wa kuwapata uende mbali zaidi ya upeo na mipaka ya vyama wanavyotoka,

Nawasilisha🙏

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿. Amen
Kweli kabisa tofauti na ilivyo Sasa Kuna vijana Wana miaka 20+ wamemkuta Jenista Mhagama ni mbunge hii siyo sawa.
Pia mambo ya ufalme yakome yaani unakuta familia Fulani wako kwenye kazi Fulani tuu Ina maana hakuna Watanzania wengine?
 
Sasa kama Jana Mh Tabasamu na Musuk wanajitoa ufahamu kiasi kile,

Mbona miaka 5 ni mingi sana kuwapo bungeni?
 
Back
Top Bottom