Ushauri:Baada ya mwanaume kunipa mimba ananikwepa sana, eti niitoe

Ushauri:Baada ya mwanaume kunipa mimba ananikwepa sana, eti niitoe

Ndugu zangu poleni na majukumu, Kwa kifupi nimekuwa na Mwanaume kama Boyfriend, tumependana sana, Baada ya kuhisi nina mimba yake kaanza chenga, anasema au tuitoe, Sijawahi kutoa Mimba na sifikirii kitu kama hicho maishani mwangu, Mwili wangu siyo Sehemu ya kufanya mauaji.

Naomba ushauri wenu

Una miaka mingapi??labda tuanzie hapo kwanza alafu tutajuwa namna ya kuku shauri....
 
Ni kweli wanawake wanapitia mengi sana kwa sababu zifuatazo:
1.Kwa sisi Waafrika tumeacha mila na desturi zetu za asili na kufuata mkumbo wa mila zisizo zetu.Makabila mengi yameacha na kutupa taratibu,Miiko na desturi zetu.Katika suala la mahusiano ilikuwa ni jambo la thamani sana kwa mwanamke kuolewa akiwa na usichana wake.Lakini kutokana na utandawazi na maendeleo msichana wengi kwa sasa wanaishi maisha ya kwenye mitandao na wanaume nao wameona ongezeko la msichana wazuri kila uchao na kuamua kuwafuja wanawake.Hivyo mawazo yanakuwa kujistarehesha zaidi kuliko kufikiria matokeo yatakuwaje.

2.Kimaumbile mwanamke anapenda zaidi kwa hisia kuliko akili.Atadanganywa sana na kwa kupitia hisia zake anajikuta tayari mambo yameharibika na mwanaume kumkimbia na kutafuta kwingine kwa kujistarehesha.Wanawake badilikeni badala ya kufanya kitu kwa hisia fikiria kwanza ndio uamue kuingia na kuyafanya hayo mapenzi.Msifanye halafu mkafikiria mwishoni.

3.Wanawake wengi hawajiamini.Wengi hawatambui wajibu wao kwa mwanaume.Na mwanaume hawawaelewi wanawake hasa kile kinachoitwa asili ya mwanamke.Mwanamke anapenda kwa hisia na kama mwanaume anapomtokea mwanamke anacheza na hisia zake alimradi ampate na apate alichokitamani.Mwanaume anatamani na hupenda mwishoni.Na hili inategemea yule mwanamke anamhudumia vipi mwanaume kwa kumliwaza,kumshauri na anatumia vipi ulimi wake kumtuliza mwanaume ili afikie kupendwa.Hapa ndipo penye tatizo.Lawama,shutuma na malalamiko ya wanawake dhidi ya mwanaume yanaishia kwenye kukimbiwa.

3.Utakuta katika Jamii mwanamke ni mzuri wa sura,umbile la kuvutia lakini ana historia ya kuwa na boyfriends kadhaa.Na hili linamfanya asiweze kuamua awe na yupi wa kumfaa yeye.Hivyo kisaikolojia anaunda wasiwasi na mashaka yanayopelekea kusahau nafasi yake kwa mwanaume.Hili linazaa matokeo ya kukinai mapenzi,kuwa baridi kwenye mahusiano na mwisho ndio hilo la kukimbiwa na kuachwa na mimba.

Kwa hiyo Tabia ya onjaonja kwa jinsia zote mbili ndio tatizo kubwa.Na huko kuonjana kunafuatiwa na mapenzi ya kuigiza na mwisho wake ni mmojawapo kukimbiwa ama kuachwa.

4.Ushindani katika kupata vitu mbalimbali toka kwa wanaume kunafanya mwanamke kuwa na lundo la wanaume hivyo kuzusha mashaka na wasiwasi kwa yule atakayempata kumfanya chombo cha starehe na kukimbia.Hapa nina maana kwamba mwanaume utampatia mwanamke mzuri wa kuvutia na hatimaye atagundua kwamba mwanamke ana tamaa ya vitu fulani ili aonekane ni matawi ya juu.Kwa hivyo kama mwanaume hajaweza kumtimizia matamanio ya mwanamke,kitakachofuata ni kumtumia mwanamke yule na kumkimbia
Mdogo wangu pole sana, Wanawake tunapitia mengi, never attempt to abort, hii dhambi itakutafuna, Kiache kiumbe cha mungu, Wanaume wengi walaghai, ukimwambia nina Mimba yako hata simu hapokei tena anaanza visingizio kwamba nimesafiri, ni wachache sana utamwambia nina Mimba yako akaonesha uso wa furaha na akaendelea kukujali, wanaume badilikeni jamaniii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Dada na hongera pia kwa kuwa mama mtalajiwa.Hyo jamaa anawza kuwa anakupenda Tena Sana lkin changamoto za kimaisha zinaweza kuwa ndo tatzo .Manake hata yeye maisha yake mwenye yanampa tabu kuyaendasha.Ushauli wangu Kama ni kweli umjamzito na umeamua kuzaa ivo jipange vzr kuzikabili changamoto za kulea mtoto.Mimi Sina uwezo lakini Kama utakua na uhitaji ukishajifungua naahidi Kila mwezi kukusaidia kwa ntakachojaliwa .Hyo Hali ilimtokea dadangu najua maumivu aloptia lakin Kama ndugu tulimhudumia na maisha yakaendelea.Pole sn na hayo ndo maisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Somo kubwa ambalo wanawake wengi wanaoamua kuzaa kabla ya ndoa wanalifanya.
Usiwe tayari kuzaa kama wewe binafsi huna uwezo wa kumudu matunzo ya mtoto hili pia hata kwa wana ndoa linawahusu.

Huyu ameamua kukuzingua Je ingekuwaje kama angefariki? Au kutoweka?
Jukumu la mtoto ni la wazazi wote wawili lakini dhamana ya mtoto anayo mama ,Mwanao hana nafasi ya kuchagua baba na Mungu amekupa dhamana hiyo wewe ni vizuri kuitumia kwa makini.
Mimi si muumini wa abortions ! Hii dhambi ilinishinda mara nyingi hutumia condoms au vidonge na ni njia ambazo ni salama.

Ushauri wangu ni huu You are never late to do the right thing jenga mazingira ya kumtumza mtoto wako wewe si wa kwanza na hautakuwa wa mwisho gangamala pambana kwaajili ya mtoto wako na wakati ukifika utaona matunda yake .



Sent from my iPhone using JamiiForums
Mjomba kasaidie kulea
 
hivi inafikaje mpaka unabeba mimba kwa mwanaume ambae hajakuoa? matatizo merngine ni kujitaftia tu. 80% ya wanaume watakuruka baada ya kupata ujauzito na bado munaendelea kubeba
 
Back
Top Bottom