Ni kweli wanawake wanapitia mengi sana kwa sababu zifuatazo:
1.Kwa sisi Waafrika tumeacha mila na desturi zetu za asili na kufuata mkumbo wa mila zisizo zetu.Makabila mengi yameacha na kutupa taratibu,Miiko na desturi zetu.Katika suala la mahusiano ilikuwa ni jambo la thamani sana kwa mwanamke kuolewa akiwa na usichana wake.Lakini kutokana na utandawazi na maendeleo msichana wengi kwa sasa wanaishi maisha ya kwenye mitandao na wanaume nao wameona ongezeko la msichana wazuri kila uchao na kuamua kuwafuja wanawake.Hivyo mawazo yanakuwa kujistarehesha zaidi kuliko kufikiria matokeo yatakuwaje.
2.Kimaumbile mwanamke anapenda zaidi kwa hisia kuliko akili.Atadanganywa sana na kwa kupitia hisia zake anajikuta tayari mambo yameharibika na mwanaume kumkimbia na kutafuta kwingine kwa kujistarehesha.Wanawake badilikeni badala ya kufanya kitu kwa hisia fikiria kwanza ndio uamue kuingia na kuyafanya hayo mapenzi.Msifanye halafu mkafikiria mwishoni.
3.Wanawake wengi hawajiamini.Wengi hawatambui wajibu wao kwa mwanaume.Na mwanaume hawawaelewi wanawake hasa kile kinachoitwa asili ya mwanamke.Mwanamke anapenda kwa hisia na kama mwanaume anapomtokea mwanamke anacheza na hisia zake alimradi ampate na apate alichokitamani.Mwanaume anatamani na hupenda mwishoni.Na hili inategemea yule mwanamke anamhudumia vipi mwanaume kwa kumliwaza,kumshauri na anatumia vipi ulimi wake kumtuliza mwanaume ili afikie kupendwa.Hapa ndipo penye tatizo.Lawama,shutuma na malalamiko ya wanawake dhidi ya mwanaume yanaishia kwenye kukimbiwa.
3.Utakuta katika Jamii mwanamke ni mzuri wa sura,umbile la kuvutia lakini ana historia ya kuwa na boyfriends kadhaa.Na hili linamfanya asiweze kuamua awe na yupi wa kumfaa yeye.Hivyo kisaikolojia anaunda wasiwasi na mashaka yanayopelekea kusahau nafasi yake kwa mwanaume.Hili linazaa matokeo ya kukinai mapenzi,kuwa baridi kwenye mahusiano na mwisho ndio hilo la kukimbiwa na kuachwa na mimba.
Kwa hiyo Tabia ya onjaonja kwa jinsia zote mbili ndio tatizo kubwa.Na huko kuonjana kunafuatiwa na mapenzi ya kuigiza na mwisho wake ni mmojawapo kukimbiwa ama kuachwa.
4.Ushindani katika kupata vitu mbalimbali toka kwa wanaume kunafanya mwanamke kuwa na lundo la wanaume hivyo kuzusha mashaka na wasiwasi kwa yule atakayempata kumfanya chombo cha starehe na kukimbia.Hapa nina maana kwamba mwanaume utampatia mwanamke mzuri wa kuvutia na hatimaye atagundua kwamba mwanamke ana tamaa ya vitu fulani ili aonekane ni matawi ya juu.Kwa hivyo kama mwanaume hajaweza kumtimizia matamanio ya mwanamke,kitakachofuata ni kumtumia mwanamke yule na kumkimbia
Mdogo wangu pole sana, Wanawake tunapitia mengi, never attempt to abort, hii dhambi itakutafuna, Kiache kiumbe cha mungu, Wanaume wengi walaghai, ukimwambia nina Mimba yako hata simu hapokei tena anaanza visingizio kwamba nimesafiri, ni wachache sana utamwambia nina Mimba yako akaonesha uso wa furaha na akaendelea kukujali, wanaume badilikeni jamaniii
Sent using
Jamii Forums mobile app