Lakini yote haya mkuu 'Rabbon', kwa nini hatujiulizi CHADEMA na hao wengine wameamua kuyakubali; Kwamba CCM ifanye itakavyo yenyewe?Sasa kumbe Wana mbinu elfu kama alivyodai Nape,
Zamani wizi ulikuwa ukifanyika ktk mchakato wa kupiga na kuhesabu kura,
Hivi sasa baada ya kustukiwa, uharibifu unaanzia kwenye mchakato wa kuandikisha wapiga kura, Hadi under 18 wanaandikishwa,
Umefika time sasa wakala wa upinzani anamaliza kuhakikisha idadi jioni akiwa na mwandishi, akiondoka na daftari, nyumbani anaongeza idadi ya watu Hadi 200, hapo jiulize inamaana usiku Kuna uandikishaji huendelea.
Sasa ikiwa mifumo ya HAKI ya Uchaguzi inajaribiwa, na Wana chi kisheria hatutumii silaha kudai mabadiliko, kususia ni jambo muhimu, wabaki na UOVU wao.
Tumwachie Mungu, Yeye ni mwaminifu atawatembelea Kila Mmoja Kwa wakati wake.
Kweli katika muda mfupi huu yaliyo tokea 2020 CHADEMA watakuwa walikwisha yasahau?
Mimi swali langu ni lile lile: kwa nini CHADEMA kama chama cha siasa hawakuamua kungali mapema kuwaendea wananchi, ambao ndio pekee walio na uwezo wa kuzuia haya yanayo fanywa na CCM sasa hivi?
Hii kazi ya kuwaendea wananchi kule mitaani kwao tokea hiyo 2020 kwa nini ilikuwa ni kazi ngumu zaidi kuliko kuitisha maandamano ambayo polisi walikuwa tayari kuyazima?
Kwani CHADEMA hawana wanachama wao na viongozi wao huko mitaani?
Hawa ndio walio takiwa kufanya kazi toka huko mwanzo kabisa, wakitumia mikakati iliyowekwa na chama nchi nzima. Ofisi za chama tokea makao makuu na kuteremka chini hadi kwenye matawi zingekuwa na jukumu la kuratibu shughuli hiyo ya kuwapa elimu wananchi juu ya haki yao ya kuwachagua viongozi wao na kuweka mipango ya kuzuia ukiukwaji wa taratibu kama hizi unazo zielezea kwenye mada yako.
Kwa nini kazi hiyo ilikuwa ngumu sana hata kujaribu tu kuitekeleza hakukufanyika?
Hili ndilo swali ninalo tafuta jibu lake.