LGE2024 Ushauri: CHADEMA ijiondoe kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa

LGE2024 Ushauri: CHADEMA ijiondoe kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Sasa kumbe Wana mbinu elfu kama alivyodai Nape,

Zamani wizi ulikuwa ukifanyika ktk mchakato wa kupiga na kuhesabu kura,

Hivi sasa baada ya kustukiwa, uharibifu unaanzia kwenye mchakato wa kuandikisha wapiga kura, Hadi under 18 wanaandikishwa,

Umefika time sasa wakala wa upinzani anamaliza kuhakikisha idadi jioni akiwa na mwandishi, akiondoka na daftari, nyumbani anaongeza idadi ya watu Hadi 200, hapo jiulize inamaana usiku Kuna uandikishaji huendelea.

Sasa ikiwa mifumo ya HAKI ya Uchaguzi inajaribiwa, na Wana chi kisheria hatutumii silaha kudai mabadiliko, kususia ni jambo muhimu, wabaki na UOVU wao.

Tumwachie Mungu, Yeye ni mwaminifu atawatembelea Kila Mmoja Kwa wakati wake.
Lakini yote haya mkuu 'Rabbon', kwa nini hatujiulizi CHADEMA na hao wengine wameamua kuyakubali; Kwamba CCM ifanye itakavyo yenyewe?
Kweli katika muda mfupi huu yaliyo tokea 2020 CHADEMA watakuwa walikwisha yasahau?

Mimi swali langu ni lile lile: kwa nini CHADEMA kama chama cha siasa hawakuamua kungali mapema kuwaendea wananchi, ambao ndio pekee walio na uwezo wa kuzuia haya yanayo fanywa na CCM sasa hivi?

Hii kazi ya kuwaendea wananchi kule mitaani kwao tokea hiyo 2020 kwa nini ilikuwa ni kazi ngumu zaidi kuliko kuitisha maandamano ambayo polisi walikuwa tayari kuyazima?

Kwani CHADEMA hawana wanachama wao na viongozi wao huko mitaani?
Hawa ndio walio takiwa kufanya kazi toka huko mwanzo kabisa, wakitumia mikakati iliyowekwa na chama nchi nzima. Ofisi za chama tokea makao makuu na kuteremka chini hadi kwenye matawi zingekuwa na jukumu la kuratibu shughuli hiyo ya kuwapa elimu wananchi juu ya haki yao ya kuwachagua viongozi wao na kuweka mipango ya kuzuia ukiukwaji wa taratibu kama hizi unazo zielezea kwenye mada yako.

Kwa nini kazi hiyo ilikuwa ngumu sana hata kujaribu tu kuitekeleza hakukufanyika?
Hili ndilo swali ninalo tafuta jibu lake.
 
Hatupaswi kuilaumu sana CDM, so far Kuna KAZI kubwa wamefanya katika mazingira haya haya magumu.

Wananchi wanachofanya sasa nionavyo ni mwamko wa kutafuta njia mbadala wa kupata viongozi wawatakao, ni suala la muda tu, na vyama vya upinzani vitapata nguvu zaidi wakati chama tawala kikizidi kudhoofika.
 
Hapana..

Ndiyo, CHADEMA huko nyuma chini ya mazingira magumu sana, chini ya ukatiri wa kutisha sana walifanya kazi vizuri sana hata kuwapa waTanzania matumaini juu yao. Hili hakuna anaye lalamika juu yake.

Naomba unionyeshe juhudi na kazi zilizo fanyika tangu Samia aingie madarakani, tuzilinganishe juhudi hizo za chama wakati huu na zile zilizo wahi kufanywa na chama toka enzi za akina Mkapa, na Kikwete, hadi Magufuli.

Hii miaka michache ya Samia imewaduaza kiasi cha kushangaza sana!

Kusema kweli, huu ndio ulikuwa wakati wa CHADEMA kumaliza kazi kwa sababu CCM wapo katika hali mbovu kuliko walivyo wahi kuwa.
 
Pamoja na kuwa kunaweza kuwa na dosari za hapa na pale ila ni dhahiri CHADEMA hawajajianda na huu uchaguzi, ndio maana kila siku ni kutoa matamko na wanajua kabisa wanakwenda kupoteza vibaya huu uchaguzi hivyo muda mwingi wanatafuta sababu za kujitoa. Huwezi kushiriki uchaguzi wakati wananchi hawajui sera zenu. Wao kila wakipewa nafasi majukwaani badala ya kusema watawafanyia nini wananchi wao wanamlamu JPM ambaye kazi zake hadi leo zinaonekana.
You are stupid ,Indeed stupid.

Wewe ni Malaya wa kisiasa ,wewe ni CHAWA akili zako ziko matakoni.
 
Wananchi wanachofanya sasa nionavyo ni mwamko wa kutafuta njia mbadala wa kupata viongozi wawatakao, ni suala la muda tu, na vyama vya upinzani vitapata nguvu zaidi wakati chama tawala kikizidi kudhoofika
Duh. Matumaini haya ni ya ajabu sana!
Labda niseme tu sikuelewa unacho kieleza, mkuu wangu 'Rabbon', katika mistari hii miwili.
 
Hapana..

Ndiyo, CHADEMA huko nyuma chini ya mazingira magumu sana, chini ya ukatiri wa kutisha sana walifanya kazi vizuri sana hata kuwapa waTanzania matumaini juu yao. Hili hakuna anaye lalamika juu yake.

Naomba unionyeshe juhudi na kazi zilizo fanyika tangu Samia aingie madarakani, tuzilinganishe juhudi hizo za chama wakati huu na zile zilizo wahi kufanywa na chama toka enzi za akina Mkapa, na Kikwete, hadi Magufuli.

Hii miaka michache ya Samia imewaduaza kiasi cha kushangaza sana!

Kusema kweli, huu ndio ulikuwa wakati wa CHADEMA kumaliza kazi kwa sababu CCM wapo katika hali mbovu kuliko walivyo wahi kuwa.
Hapo nikiri kuwa,

Mwenyekiti alikosea sana kuingia kwenye maridhiano akiamini Kuna kitu kitabadilika,

Muda ulipotea sana kusubiri embe chini ya mnazi.
 
Duh. Matumaini haya ni ya ajabu sana!
Labda niseme tu sikuelewa unacho kieleza, mkuu wangu 'Rabbon', katika mistari hii miwili.
Nilichomaanisha ni kuwa, wananchi kupuuza Sanduku la kura haimaanishi hawapendi kuchagua viongozi la, wasichopenda ni kutumika kuonyesha Kuna uchaguzi ilhali matakwa na sauti zao haxiheshimiwi,

Sasa wakiamka kudai mabadiliko, vyama vya upinzani vitapata boost ambayo itasaidia kuipoteza CCM once and for all.
 
Salaam, Shalom!!

HOJA ya ushauri hapo juu ni kupuuzwa Kwa mapendekezo muhimu ambayo mliyatoa ikiwemo uchaguzi huo wa Serikali za mitaa kusimamiwa na Tume huru ya Uchaguzi.

Sasa Kwa kuwa yanayoendelea hivi sasa, wanachama wenu wanaendelea kuumizwa na Hila zimeendelea kutawala mchakato wa uchaguzi,

Nichukue nafasi hii kuwasihi kujitoa mapema Ili kuepusha watu wasio na hatia kuumizwa.

NB: Kushiriki uchaguzi ambao mnajua ni batili Kisha kudai kuwa mmeibiwa kura, hiyo ni kuwafanya wananchi kama hawafikiri Sawa sawa!!

Nawasilisha.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Ushauri wa hovyo...

Ijiondoe halafu ili iweje sasa...?

Lazima washiriki na watumie majukwaa ya kampeni kwa wiki nzima kuiwasha moto nchi...

Usiwaze kushinda na kushindwa tu...

Unapaswa kufikiria na kesho itakuwaje....

Hawa hakuna kuwaachia. Ni lazima mapambano yaendelee katikati ya figisufigisu zao...
 
Hadi hapo "watakapo amka".

Kwa sasa hivi mahitaji na matakwa ya CCM yanatimia kwa kuwa lengo ni kuendelea kuwa madarakani.
 
Hivi watanganyika wangesusia harakati za kudai Uhuru ungepatikana? Kila kitu kina faida na hasara zake. Hata kwenye matembezi kuna kujikwaa na kuanguka na kuamka kuendelea na safasi na si kususia safari ukianguka njiani wakati unatembea.
 
Pamoja na kuwa kunaweza kuwa na dosari za hapa na pale ila ni dhahiri CHADEMA hawajajianda na huu uchaguzi, ndio maana kila siku ni kutoa matamko na wanajua kabisa wanakwenda kupoteza vibaya huu uchaguzi hivyo muda mwingi wanatafuta sababu za kujitoa. Huwezi kushiriki uchaguzi wakati wananchi hawajui sera zenu. Wao kila wakipewa nafasi majukwaani badala ya kusema watawafanyia nini wananchi wao wanamlaumu JPM ambaye kazi zake hadi leo zinaonekana.
Kama ushindani ungekuwa ni wa hoja tungeona mazingira ya kweli ya ushindani. Sasa unasema umejipanga lakini unalazimisha kuwa mchezaji na refarii hapo hapo! Ifahamike ccm wanafaidika na mfumo huu wa uchaguzi, na ushahidi wa mfumo huu kuibeba uko wazi.

Wananchi wengi wamesusia huu uchaguzi kwasababu wanajua fika mfumo huu wa uchaguzi hautoi ushindani wa haki, lakini ccm kupitia serekali, wanalazimisha mfumo huu huu ambao wanajua fika utawapa ushindi ndio uendelee kuwepo, wakati hauaminiki na walio wengi. Sasa ukisema cdm wanajua watashindwa, unategemea wataacha kutangazwa kushindwa kwa mfumo huu?
 
Ushauri wa hovyo...

Ijiondoe halafu ili iweje sasa...?

Lazima washiriki na watumie majukwaa ya kampeni kwa wiki nzima kuiwasha moto nchi...

Usiwaze kushinda na kushindwa tu...

Unapaswa kufikiria na kesho itakuwaje....

Hawa hakuna kuwaachia. Ni lazima mapambano yaendelee katikati ya figisufigisu zao...
Ahsante, mkuu 'The Palm Beach'.
Nikiangalia michango yote kwenye mada hii, huu wa kwako ndio umetofautiana na yetu sisi wengine wote ambao tumekata tamaa na kujisalimisha kwa CCM.

Sasa sijui kama CHADEMA kweli wanao moto huo unao wahimiza wauwashe wakati wa Kampeni. Hiyo angalau itakuwa ni kifuta jasho, hata kama si kuzuia ushindi mkubwa wa CCM; lakini wananchi wenyewe watakuwa wamesikia sauti za kuwaunga mkono katika njia zao mbalimbali walizo zitumia kugomea uchafuzi unaofanywa na CCM.

Ni nani ajuae, pengine moto huo utakuwa ndiyo chachu ya kuusambaza nchi nzima na wananchi waweze kufanya kweli wakati wa uchaguzi mkuu wenyewe.

Nikushukuru tena, maanake nami umenipa nafasi tena ya kuwa na matumaini juu ya kuwakabili hawa majini wa CCM.
Sentensi ambayo ninge penda kuitumia: CHADEMA watumie uchafuzi utakaofanywa na CCM kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa, kuwasha moto kuelekea UCHAGUZI MKUU 2025. Wakifanya hivyo, nami nitakuwa na imani na CHADEMA tena.
 
Hapo nikiri kuwa,

Mwenyekiti alikosea sana kuingia kwenye maridhiano akiamini Kuna kitu kitabadilika,

Muda ulipotea sana kusubiri embe chini ya mnazi.
Naomba umsome 'The Palm' hapo chini #69.
Iwapo ilishindikana kwa CHADEMA kwenda mitaani na vitongojini tokea 2020; je itawezekana sasa kuweka matumaini wao na sisi wote tusitaka haya ya CCM kushirikiana nao kuwahimiza wananchi kukataa hujuma 2025?

Mimi nadhani huu ni ujumbe muhimu sasa hivi.
 
Ushauri wa hovyo...

Ijiondoe halafu ili iweje sasa...?

Lazima washiriki na watumie majukwaa ya kampeni kwa wiki nzima kuiwasha moto nchi...

Usiwaze kushinda na kushindwa tu...

Unapaswa kufikiria na kesho itakuwaje....

Hawa hakuna kuwaachia. Ni lazima mapambano yaendelee katikati ya figisufigisu zao...
Tusubiri huo moto.
 
You are stupid ,Indeed stupid.

Wewe ni Malaya wa kisiasa ,wewe ni CHAWA akili zako ziko matakoni.
Halafu ndio unakuta na wewe unategemewa na chama chako. Ni bora ccm waendele kutawala tu ikiwa akili za upinzani ndio hizi.
 
Sasa sijui kama CHADEMA kweli wanao moto huo unao wahimiza wauwashe wakati wa Kampeni.
Hiki ndicho kiini kamili cha wasiwasi wa walio wengi.
Yale maridhiano yalitia doa imani waliyokuwa nayo wananchi kwa CDM.

Ila kama alivyozungumza mdau hapo juu, tusubiri nondo zao wakati wa kampeni.
 
Binafsi ningeshauri vyama vyote viache kushiriki maana kinachoenda kutokea ni Kama yale yale tu
 
Salaam, Shalom!!

HOJA ya ushauri hapo juu ni kupuuzwa Kwa mapendekezo muhimu ambayo mliyatoa ikiwemo uchaguzi huo wa Serikali za mitaa kusimamiwa na Tume huru ya Uchaguzi.

Sasa Kwa kuwa yanayoendelea hivi sasa, wanachama wenu wanaendelea kuumizwa na Hila zimeendelea kutawala mchakato wa uchaguzi,

Nichukue nafasi hii kuwasihi kujitoa mapema Ili kuepusha watu wasio na hatia kuumizwa.

NB: Kushiriki uchaguzi ambao mnajua ni batili Kisha kudai kuwa mmeibiwa kura, hiyo ni kuwafanya wananchi kama hawafikiri Sawa sawa!!

Nawasilisha.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Cjui km watakuelewa ni km wanatekeleza matakwa ya ccm
 
Back
Top Bottom