MJENGA
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 884
- 850
Clip hii inayomuoneesha Mdude Nyagali akiapa kutumia wembe kumnyoa Rais Mama Samia Suluhu Hassan (sijui ni kwa namna gani) inaonesha kiwango cha juu cha ukosefu wa adabu wa mhusika kwa mamlaka za nchi na watu waliomzidi umri.
Kauli ya Mdude kwa Rais si tu ni ya kishenzi isiyopaswa kuvumiliwa hata na wanachadema wenyewe, bali inatoa taswira mbaya kwa chama chake, kwa nchi na kwa Rais ambaye amejipambanua kujenga demokrasia ya kistaarabu isiyokwamisha ustawi wa nchi yetu.
Ninafahamu Mbowe ni mtu mstaarabu anayejua mipaka ya demokrasia. Mbowe angekuwa kama Mdude nchi hii ingeshavurugika hivyo ninamshauri amtake Mdude amuombe radhi Rais Samia. Huo ndio itakuwa kipimo cha ukomavu wa siasa kwa chadema.