USHAURI CHADEMA: Mdude Nyagali amemkosea adabu Rais Samia, mtakeni amwombe radhi

Hakuna watu wasio na adabu wala staha kama baadhi ya wanaCCM.

Rais Magufuli alikuwa na kauli za hovyo ambazo Mdude hafikii hata 50%.

Heri James ana mdomo mchafu, na kauli za kuhatarisha usalama, kwa kiasi ambacho Mdude hafikii hata 10%.

Bashiru na kauli zake za CCM itatumia dola kushinda, ni kauli za kipuuzi, hovyo, na za kuhatarisha usalama wa nchi.

Polepole ana kauli za kijinga kama zile za sisi tunatumia V8, unaijua V8 wewe, ni kauli za kijinga, za kuudhi na kuwadharau masikini walipa kodi.

Kabudi ana kauli za hovyo, mpaka kumwita Magufuli Mungu. Hivi sisi ambao tunajua Mungu halinganishwi na chochote, mnajua tulikereka kiasi gani?

Kangi Lugola kumwita Magufuli ni sawa na Yesu, ni kauli za kukufuru imani za watu.

Mwanri kusema kuwa Mungu anatakiwa kumshukuru Magufuli, ni kauli ya kipuuzi, na ya kuudhi kwa wanaomwabudu Mungu.

Mdude alitumia kauli kali kwa mtu ambaye hakustahili lakini bado kauli yake ni nyepesi sana ukilinganisha na kauli nyingi za hovyo za baadhi ya wanaCCM, tena ni za viongozi wakubwa kwenye chama na Serikali.
 
Ni kosa kubwa kulinganisha vitu visivyo fanana. Kuna baya na kuna baya zaidi.

Sasa mkiwa mnashindwa kutofautisha mambo hata haki zenu ni muhali kuzijua.
 
Ongezea na yule mwanaharakati huru Musiba. Amewahi kuwatukana akina mzee Warioba kwamba wameeka wanasubiri kujifia wasitubaribie nchi.
 
Ni kosa kubwa kulinganisha vitu visivyo fanana. Kuna baya na kuna baya zaidi.

Sasa mkiwa mnashindwa kutofautisha mambo hata haki zenu ni muhali kuzijua.
Kwangu mimi, mtu anayesema kuwa, tulishindwa kummaliza kwa risasi, safari hii akija, tutammaliza kwa kumchoma sindano, ni kauli ya hatari zaidi kuliko anayesema ayamnyoa Rais kwa wembe.
 
Ongezea na yule mwanaharakati huru Musiba. Amewahi kuwatukana akina mzee Warioba kwamba wameeka wanasubiri kujifia wasitubaribie nchi.
Sahihi kabisa.
 
Mdude size yake apewe U-DC tu,kijana mchapa kazi.
Hamtaki,pelekeni matako huko.
 
Kwangu mimi, mtu anayesema kuwa, tulishindwa kummaliza kwa risasi, safari hii akija, tutammaliza kwa kumchoma sindano, ni kauli ya hatari zaidi kuliko anayesema ayamnyoa Rais kwa wembe.
Swali la msingi huyo ni nani na ana mwambia nani ?

Lazima mjue kutofautisha mambo na kuyapima. Athari inayoletwa na mtawala huwezi kulinganisha na mtu mmoja mmoja.

Lakini kauli hiyo ina mdhuru nani ? Jamii au mtu mmoja ?

Duniani kumepita viongozi au watawala waouvu pengine mpaka leo hakuna mfano,na watu walifaulu na kuwashinda watawala hao kwa njia bora zaidi na si hizi zenu za kihuni na utovu wa adabu.
 
Kwangu mimi, mtu anayesema kuwa, tulishindwa kummaliza kwa risasi, safari hii akija, tutammaliza kwa kumchoma sindano, ni kauli ya hatari zaidi kuliko anayesema ayamnyoa Rais kwa wembe.
Naomba uniambie jambo moja alichokisema Mdude ni sahihi au si sahihi ?
 
Nonsense & baseless discourse.

Kwa heshima na taadhima, viijana wa CCM mnatia aibu sana mnapoibua mambo madogo ambayo hayana madhara yoyote katika jamii kana kwamba hamna ubongo katika vichwa vyenu. Huenda hii ni kwa sababu hamna hata exposure yoyote.

Aidha, mnashindwa kupambana na mambo ya msingi kama ukosefu wa ajira, Suala la afya na ubora wa elimu bali mnajadili minor issues kama ya MDUDE vs SAMIA SULUHU HASSAN ambazo hazina madhara yoyote katika jamii.

Kadhalika, napenda kuwafahamisha kwamba alichokifanya Mdude ni jambo la kawaida sana kwa sababu zile ni tambo za kisiasa tu nothing more. Kwa ambao tulipata nafasi ya kukaa nje ya Tanzania tunaelewa sana. Hata kwa nchi ambazo wanajitambua na zenye maendeleo makubwa ya demokrasia mfano Marekani utakuta Rais anakosolewa na hata kutukanwa but people don't care.

Ila ukifanya hivyo hapa Tanzania watu wanakuona wa ajabu sana. Mfano mwingine ni hapa Nchini Kenya ambapo Rais aliambiambiwa anavuta bangi ila hakumchukulia hatua za kisheria yule aliyemwambia hivyo.

Nitumie nafasi hii kuwakumbusha kuwa Rais ni cheo tu kama vyeo vingine. Rais siyo Mungu kwamba asikosolewe. She is even not perfect. Kwanini asikosolewe na kuambiwa ukweli pale anapovunja katiba?

Mwisho, tatizo la watanzania wengi ni ukosefu wa exposure, education( mmesoma ila hamjaelimika) na ndiyo maana mnapenda kujadili minor issues kuliko vitu vya msingi, uwezo wenu wa kuchanganua mambo ni mdogo sana.

To be honestly fair, I didn't expect this to be discussed on in here. We have to discuss on intricate issues for instance, social amenities but not this. Kindly let's be smart.
 
So what's your point...Cariha?

Alichokifanya Mdude katika siasa zile ni tambo za kisiasa tu but nothing more au kwa vile katumia lugha anbayo Watanzania hatutaki kuisikia? How many times mwendazake alikuwa anawaita watendaji wake kwamba wapumbavu, wajinga?

Unakumbuka yule DED aliyemwambia mwananchi kwamba kalisha tako chini? Yule ni CDM au CCM?

Unakumbuka Makonda alivyomdhalilisha mzee Waryoba? Je ni mwana CDM yule?
 
"Mtoto akisema,basi ujue amesikia kwa baba au mama". Ukiuelewa huu msemo,utakuwa umepevuka kisiasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusi kubwa sana unatakaje kumnyoa mama mtu mzima anayeweza kukuzaa akicheza rede. Wewe waweza mwambia hvo mamako mzazi. Mdude Hana adabu tangu hata enzi za Jiwe bwana
Unajua maana ya tusi?

Kumnyoa mtu ni tusi?

Kumnyoa maana yake watapambana na Rais kwa hali na mali kutetea katiba isivunjwe na Rais ila siyo kumnyoa kama ulivyoelewa.

Nawaombeni vijana muache hisia za ajabu hakuna tusi pale.
 
Unajua maana ya tusi?

Kumnyoa mtu ni tusi?

Kumnyoa maana yake watapambana na Rais kwa hali na mali kutetea katiba isivunjwe na Rais ila siyo kumnyoa kama ulivyoelewa.

Nawaombeni vijana muache hisia za ajabu hakuna tusi pale.
Unatetea upuuzi!! Tunahangaika tu kuwashauri inavyoonyesha matusi ni agenda kuu ya chama chenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…