Ushauri: CHADEMA, Mrudisheni Dkt. Slaa chamani kuongeza morali ya ushindi

Mwakani uchaguzi na Chadema kama bado ipo ipo tu. Sijui tuisaidiaje Chadema lakini nahisi wanahitaji fikra na uelekeo mpya.
 
Kiukweli,Chadema bila MTU Kama Dr. Slaa mwenye kuuchukia ufisada kamwe hakiwezi na hakitaweza na hakitwezeshwa na wananchi kuingia madarakani Hata wakiambiwa waunde Tume ya Uchaguzi na kuusimamia Kwa katiba yoyote wanaodhani kuwa ni Bora.

Kwanza Chini ya Mbowe Chadema Haina Tofauti na CCM ya Mafisadi.
Mbowe ni MTU Wa aina ya Mafisadi wote walioko Afrika.

Hatuwezi kuichagua Chadema inayoongozwa na bepari huku ikiwa na makada maskini na wananchi wanyonge NDIO wapiga kura!
Kuichagua Chadema yenye serΓ‘ na mlengo Wa Kibepari chini ya Mbowe Rafiki Wa majizi na Mafisadi walioko CCM wakati nchi imejaa Majizi ni kupeleka Nchi mnadani.

Chadema isahau kabisa kuingia madarakani Kwa serΓ‘ zake za kuwategemea Wazungu kuja kuiba rasilimali za Nchi eti ni wawekezaji.
Bandari imeuzwa , Mbowe akalamba Asali ya Waarabu akampinga Dr Slaa na Mwabukusi Sasa tunaona Mpaka Maeneo nyeti yanachukuliwa na Wageni .Watahamisha Mpaka Kambi za Majeshi ya Bukinafaso.

Mbowe anailazimisha Chadema Kucha kutwa watumie muda mwingi kumponda na kumsema Hayati Magufuli. Jambo linalowapandisha hasira Wananchi.
 

1. Hapana ndugu. Taabu yangu na wengi ni kuweka hisia zao kuwa ni uthibitisho.

2. Humo wakiendeleza ramli chonganishi zisizokuwa na mashiko.

3. Kulikoni kutodhani hichi unachowahisi wengine pasipokuwa ushahidi, kinaweza elekezwa kwako hivyo hivyo?
 
CCM haitaweza kuangushwa kwa maneno bila kuchapana na kuuana na hatimaye kupata katiba mpya na tume huru.

CCM ipo na itaendelea kuwepo. Yaani hata rais Samia akipigiwa kura na mwanaye Abdul tu, bado atatangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais.
Ndomana nimependekeza ujio wa Dr Slaa, chama kirudi katika siasa za kiuanaharakati.

Hii biashara ya kwenda kuishtaki CCM marekani na ubelgiji Kila uchwao hailipi,

Chama kirudi Kwa wananchi.

Pia ingekuwa ni Rahisi tu Kwa CCM kushinda uchaguzi, wasingeanza mapema compaign, uchaguzi ni habari ingine kabisa.
 
Nimeedit, ni Ilani ya 2025-2030 thanks πŸ™.

Pia tuwekee records sawa, Dr Slaa, hakuwahi kurudi CCM.

Ni kama tu Marehemu Anna Mugwira.
 
1. Hapana ndugu. Taabu yangu na wengi ni kuweka hisia zao kuwa ni uthibitisho.

2. Humo wakiendeleza ramli chonganishi zisizokuwa na mashiko.

3. Kulikoni kutodhani hichi unachowahisi wengine pasipokuwa ushahidi, kinaweza elekezwa kwako hivyo hivyo?
1 & 2. Wanasema mtu mwenye utimamu wa akili hawezi kata tawi alilokalia. Kauli aliyoitoa kwenye angalizo lake ndio imenipa Mimi dhana niliyonayo juu yake. Na hata hivyo, sikusema kwamba hisia zangu ni sahihi, ndio maana nilitumia neno "dhana"

3. Ushahidi ulioibua dhana yangu, ni wa kifact zaidi, na nimeelezea hapo juu. Na pia endapo akitokea mtu akaelekeza kwangu, awe na kilichomsukuma kusema atakachosema.
 
Kama saccos Yao Ile na kina Mdude na wale wengine wenye njaa Wameshindwa kupata kiki kwenye dp World ndio itakuwa huko kwa walamba asali?
Wameshindwa kivipi wakati wananchi wengi wako upande wao including makada wa CCM?

DP world ndo imeondoa kabisa possibility ya aliyepo kugombea tena.
 
Mkuu mrudishe ww maana hakufukuzwa cdm.
Nimekishauri chama kimrudishe.

Hivi mwamko wa CHADEMA majukwaani Kwa sasa unauonaje ukilinganisha na 2015 kurudi nyuma?
 

Sawa:

 
Kipimo chako juu ya ili ni kipi?
Kutuaminisha umma kuwa Serikali ya Rais Samia ni wasikivu, kwamba wanaweza kuaminika na kubadilika na kutenda HAKI ,

Mkt anaweza KURUDIA maneno Yale saiz?
 
Msimamo Gani unao uzungumzia wewe wakati aliunga juhudi kipindi Cha jiwe

Uzuri hakufukuzwa na mtu anaona aibu kurudi

Wenye CCM wamerudi rasmi Sasa hawamtaki na CDM hawamtaki mwanasiasa mwenye tabia za kimalaya malaya
Dr Slaa hakurudi CCM,

Mbona Hilo liko wazi?

Lowassa ndiye aliyerudi CCM.

So Dr Slaa alikuwa sahihi kujitenga na Fisadi, Mnyika pia amerejea kusema Juzi, hakuunga mkono ujio wa Lowassa, na ndo sababu ya ukimya wake Kwa kipindi chote kile.
 
Umekosa vyakuandika sasa umeanza kuandika ujinga.
 
Hata Dume la Mbuzi likizeeka zizini huwa tunalitoa bahna πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
Akili ya Dr Slaa Iko murua kabisa.

Siasa Si kambi ya Jeshi kwamba inahitajika kubeba viroba vya mawe.
 
Umekosa vyakuandika sasa umeanza kuandika ujinga.
Kuishauri CHADEMA kumrudisha Dr Slaa Ili kurudi katika siasa za kiuanaharakati ni Ujinga?

Basi huo ni Ujinga wenye TIJA.
 
Kutuaminisha umma kuwa Serikali ya Rais Samia ni wasikivu, kwamba wanaweza kuaminika na kubadilika na kutenda HAKI ,

Mkt anaweza KURUDIA maneno Yale saiz?
Alikuwa anatoa mrejesho kwa wananchi juu ya walichokubaliana.

Pengine hayo aliyoyasema ndio ambayo walikubaliana kwenye vikao vyao. Kutotekelezwa kwake, pengine watawala wameamua kuyakiuka. Nadhani hapo kinachotakiwa ni yeye kuulizwa, mbona hatuoni utekelezaji?. Kisha ndio tujue shida ipo kwake aliyetupa mrejesho au kwao aliokubaliana nao?
 
Akili ya Dr Slaa Iko murua kabisa.

Siasa Si kambi ya Jeshi kwamba inahitajika kubeba viroba vya mawe.
Sawa nakukubalia sija kataa ila huoni kwamba hatutakuwa tumetenda haki kwa wengine kunyanyuka na kikendeleza chama. nafikiri Afrika tuanze kunyanyuka kuacha kutegemea wale wale kila uchao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…