Ushauri: CHADEMA, Mrudisheni Dkt. Slaa chamani kuongeza morali ya ushindi

Ushauri: CHADEMA, Mrudisheni Dkt. Slaa chamani kuongeza morali ya ushindi

Mwakani uchaguzi na Chadema kama bado ipo ipo tu. Sijui tuisaidiaje Chadema lakini nahisi wanahitaji fikra na uelekeo mpya.
Tanzania hakuna uchaguzi, Bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura.
Rabbon ni Mwananchi wa kawaida, MKULIMA asiye na chama, ila ni Mzalendo wa Nchi yake Tanzania.
Mwambie Dr.Slaa na Mwabukusi waanzishe chama tutawaunga mkono kutokana na wanayosimamia. Usilazimishe arudishwe cdm wakati hakafukuzwa. Milango Iko wazi huko cdm, akitaka arudi, akiona vipi aendelee na utaratibu wake.
 
Baada ya hayo yote uliyoona (observations) bado tu umeweka tumaini kwa CHADEMA? Bado unaamini wananchi wengi wanaitumainia CHADEMA?

Kwa nini usifikirie chama mbadala hata ikibidi Dr Slaa kukianzisha? Kwanza umeshapata maoni yake kuhusu CHADEMA? Ameshasikika na kusomeka akitoa kauli hasi sana kuhusu chama hicho na viongozi wake enzi za awamu ya 5.

Sasa Dr Slaa pamoja na “uzuri” wote unaompamba, unategemea ataweza kufanya kazi na mwenyekiti na viongozi wengine wa CHADEMA kuleta mageuzi ndani ya chama? Unaamini atapewa “blank cheque” afanye anayotaka, anavyotaka?
Ndomana tunawasgauri wabadili uelekeo kurudi katika siasa za kiuanaharakati, na kiuzalendo.

Wasiposikia na kuendelea na urafiki na Mafisadi, move ifuatayo ni kushauri mkt akae pembeni!!
 
Salaam, Shalom!!

Ndugu Mnyika anafanya vizuri, lakini Bado hajafikia viwango vya Dr Slaa, Mnyika anaweza kupewa nafasi nyeti kuelekea uchaguzi huku Dr Slaa akifanikisha njia nyeupe Kwa chama.

ZIFUATAZO, ni sababu kwanini CHADEMA inamuhitaji zaidi Dr Slaa.

1. KUFAIL KWA MARIDHIANO.

Jambo hili Bado Lina maswali mengi ndani na nje ya chama, muda uliopotea kukaa mezani na mahasimu CCM Bado unaleta maswali yasojibika, tukijiuliza, chama kimeachieve nini katika maridhiano Yale, hakuna majibu ya Moja Kwa moja zaidi ya lawama,hivyo kupunguza maswali haya, Leteni ingizo jipya ambalo ni Dr Slaa turudi katika siasa za kiuanaharakati.

2. MIKAKATI THABITI KUELEKEA UCHAGUZI.

Najua mnapanga kushiriki uchaguzi, Dr Slaa Bado ni chaguo zuri. Ubora wake katika mipango thabiti unajulikana.

3. KULETA HAMASA KWA WANANCHI WASIOPENDA UFISADI NA RUSHWA.

Dr Slaa aliondoka akipishana na Lowwassa, na imethibitika kuwa Lowwassa ni Liability Kwa chama, maana amerudia nyumbani kwao, hivyo Dr Slaa alikuwa sahihi kuondoka. majuzi KM ndugu Mnyika amenukuliwa akisema kuwa, pia hakufurahia ujio wa Lowassa chamani, na ndio chanzo Cha ukimya wake wakati Ule, hivyo kurejea kwake Dr Slaa, kutaamsha tumaini jipya.

4. ANAAMINIKA KWA MAKUNDI YOTE.

Dr Slaa ni mtu mwenye misimamo isoyumba, hivyo ujio wake utaleta taswira mpya kuelekea harakati za kupata Tume huru kabla ya Uchaguzi wowote. Vijana watajitokeza tena Kwa wingi mikutanoni sababu aliaminika sana enzi zake.

Kundi kubwa lililohama CHADEMA na lingine kususia siasa baada ya Lowassa mwenye kashfa za ufisadi alipopewa nafasi, litarejea na Dr Slaa ikiwa atarudishwa tena chamani Kwa nafasi ya Katibu MKUU.

5. UANDAAJI WA SERA ZA CHAMA NA ILANI YA UCHAGUZI KWA MIAKA MITANO IJAYO 2025-2030.

Mchango wa Dr Slaa, hata hauhitaji Utafiti, maana alisaidia sana CHADEMA kuwa chama chenye sera thabiti ambazo nyingi ziliibwa na kutumiwa na chama tawala wakati huo 2015.

ANGALIZO: Chama chakavu Hadi sasa hakina KM, So Ingizo la Dr Slaa Kwa wakati huu, lazima utaleta mtikisiko Kwa chama tawala.

Ni hayo Kwa sasa.

Karibuni. 🙏
Bila shaka wako radhi kuwarudisha akina mdee ila si slaa.
 
Tanzania hakuna uchaguzi, Bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura.

Mwambie Dr.Slaa na Mwabukusi waanzishe chama tutawaunga mkono kutokana na wanayosimamia. Usilazimishe arudishwe cdm wakati hakafukuzwa. Milango Iko wazi huko cdm, akitaka arudi, akiona vipi aendelee na utaratibu wake.
CCM Kwa sasa haiwezi ruhusu watu kama Slaa, Mdude na Mwabukusi kuanzisha chama,

Ndomana waliponusa Mbatia anaweza kuwakaribisha, akatumwa 30 kuharibu move.

Siasa zimepoa, hakuna tumaini, tunaowapenda hatuwaamini, sasa Imani inahitajika kuturudisha pale.
 
Bila shaka wako radhi kuwarudisha akina mdee ila si slaa.
Naamini zuio kubwa liko Kwa wakubwa nje ya chama wenye ushirika usio rasmi na viongozi Wachache wa chama.

Hii Si sawa hata kidogo.
 
2025 tukawq na uchaguzi wq rais,madiwani ,wabunge na serikali za mitaa?
Inawezekana kabisa.

Maana u haguzi wa MITAA ni vyema ukasimamiwa na Tume ya Uchaguzi Si Tamisemi.

Malalamiko ni mengi na ukizingatia saiz Kuna shinikizo la kupata Tume huru ya Uchaguzi.
 
Mzee wa miaka 73 tena asiyekuwa na msimamo ana faida gani kwa sasa?
Huyu alisema katiba mpya na mikutano ya hadhara haina umuhimu? Lissu kupigwa risasi ni kawaida?
Ndumilakuwili ni liability kwa chadema
Dr Slaa ni mtu wa misimamo isoyumba.

Hadi Leo, kwake Lowassa ni fisadi, jambo ambalo ukimuuliza Lissu au Mbowe watajiuma meno.
 
Kuhusu kitabu kipya itakuaje hatuandiki tena
Mpango wa kitabu iipya uko pale pale.

Dr Slaa katika Hilo la Katiba mpya amenyooka kabisa,

Kwamba vyama visiingie pressure ya Uchaguzi na kusahau Katiba mpya yenye mengi kuwahusu wananchi.

Kulazimisha uchaguzi bila Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya, liko Giza mbele ambalo tunapambana kuliondoa sasa.
 
Ushauri wa kijinga kabisa.
Maoni Yako yanaheshimiwa.

Ungeeleza pia BUSARA zako zilipo katika kuondoa mkwamo, kuwa njia panda Kwa CHADEMA kuelekea 2025 utatuliweje ingefaa zaidi🙏
 
Mpango wa kitabu iipya uko pale pale.

Dr Slaa katika Hilo la Katiba mpya amenyooka kabisa,

Kwamba vyama visiingie pressure ya Uchaguzi na kusahau Katiba mpya yenye mengi kuwahusu wananchi.

Kulazimisha uchaguzi bila Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya, liko Giza mbele ambalo tunapambana kuliondoa sasa.
Ila naona km kitabu kimepotezewa hivi sioni zile kelele za mwanzo
 
Ila naona km kitabu kimepotezewa hivi sioni zile kelele za mwanzo
Ni sababu ya homa ya Uchaguzi.

Nikwambie ndugu, Bila BUSARA kutumika, kulazimisha uchaguzi kufanyika Kwa Katiba hii, mbeleni Si kuzuri hata kidogo.

Bado naamini kuanzia Sasa Hadi June 2025 tutakuwa tumefanukiwa ktk mengi kuondoa sintofahamu ya kesho ya Taifa letu.
 
Kwahiyo ni heri tuandike kitabu kipya kwanza ,tusiwe na haraka ya Uchaguzi
 
Kwahiyo ni heri tuandike kitabu kipya kwanza ,tusiwe na haraka ya Uchaguzi
Ni Kweli kabisa,

Ikiwa aliyepo atashindwa kulikamilisha Hilo Kwa miaka yake minne na ushehe, ni Bora asipewe muda, akabidhi Kwa wahusika, tukamilishe Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wowote.

Mzee Warioba ameendelea kusisitiza muda unatosha na ni vyema uchaguzi ukafanyika Kwa Tume huru ya Uchaguzi.

Tukiunganisha nguvu, inawezekana kuepuka Shari kamili mbele yetu.
 
Dr Slaa ni mtu wa misimamo isoyumba.

Hadi Leo, kwake Lowassa ni fisadi, jambo ambalo ukimuuliza Lissu au Mbowe watajiuma meno.
Hana msimamo wala, hilo la Lowassa unamuona kama ana msimamo lakini nyuma ya pazia alishiriki kumleta sema kuna vigezo kadhaa Lowassa alishindwana Slaa akajitoa

Kama unafuatilia siasa vizuri na unamfuatilia Slaa vizuri, hana msimamo kama unavyosema

Mfano mdogo tu ni suala la katiba mpya ambapo alisema halina umuhimu wowote labda kwa wanasiasa wanaotafuta vyeo, kingine ni kuhusu mikutano ya hadhara, na kuhusu kesi za kisiasa za kubambikiza
 
Kwahiyo ni heri tuandike kitabu kipya kwanza ,tusiwe na haraka ya Uchaguzi
Na jambo hili la kupata Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi ikishindikana,

Tutaletewa Dikteta mwingine. Na DEMOKRASIA itapotea for all. Na Ule msemo wa kuhamia Burundi utakuwa dhahiri.
 
Back
Top Bottom