Ushauri: CHADEMA, Mrudisheni Dkt. Slaa chamani kuongeza morali ya ushindi

Mwakani uchaguzi na Chadema kama bado ipo ipo tu. Sijui tuisaidiaje Chadema lakini nahisi wanahitaji fikra na uelekeo mpya.
Tanzania hakuna uchaguzi, Bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura.
Rabbon ni Mwananchi wa kawaida, MKULIMA asiye na chama, ila ni Mzalendo wa Nchi yake Tanzania.
Mwambie Dr.Slaa na Mwabukusi waanzishe chama tutawaunga mkono kutokana na wanayosimamia. Usilazimishe arudishwe cdm wakati hakafukuzwa. Milango Iko wazi huko cdm, akitaka arudi, akiona vipi aendelee na utaratibu wake.
 
Ndomana tunawasgauri wabadili uelekeo kurudi katika siasa za kiuanaharakati, na kiuzalendo.

Wasiposikia na kuendelea na urafiki na Mafisadi, move ifuatayo ni kushauri mkt akae pembeni!!
 
Bila shaka wako radhi kuwarudisha akina mdee ila si slaa.
 
CCM Kwa sasa haiwezi ruhusu watu kama Slaa, Mdude na Mwabukusi kuanzisha chama,

Ndomana waliponusa Mbatia anaweza kuwakaribisha, akatumwa 30 kuharibu move.

Siasa zimepoa, hakuna tumaini, tunaowapenda hatuwaamini, sasa Imani inahitajika kuturudisha pale.
 
Bila shaka wako radhi kuwarudisha akina mdee ila si slaa.
Naamini zuio kubwa liko Kwa wakubwa nje ya chama wenye ushirika usio rasmi na viongozi Wachache wa chama.

Hii Si sawa hata kidogo.
 
Kuna Kila dalili uchaguzi wa MITAA kupelekwa 2025,

Kapu limekaushwa na wizi, pia marejesho ya mikopo na riba ni makubwa sana.
2025 tukawq na uchaguzi wq rais,madiwani ,wabunge na serikali za mitaa?
 
2025 tukawq na uchaguzi wq rais,madiwani ,wabunge na serikali za mitaa?
Inawezekana kabisa.

Maana u haguzi wa MITAA ni vyema ukasimamiwa na Tume ya Uchaguzi Si Tamisemi.

Malalamiko ni mengi na ukizingatia saiz Kuna shinikizo la kupata Tume huru ya Uchaguzi.
 
Mzee wa miaka 73 tena asiyekuwa na msimamo ana faida gani kwa sasa?
Huyu alisema katiba mpya na mikutano ya hadhara haina umuhimu? Lissu kupigwa risasi ni kawaida?
Ndumilakuwili ni liability kwa chadema
Dr Slaa ni mtu wa misimamo isoyumba.

Hadi Leo, kwake Lowassa ni fisadi, jambo ambalo ukimuuliza Lissu au Mbowe watajiuma meno.
 
Kuhusu kitabu kipya itakuaje hatuandiki tena
Mpango wa kitabu iipya uko pale pale.

Dr Slaa katika Hilo la Katiba mpya amenyooka kabisa,

Kwamba vyama visiingie pressure ya Uchaguzi na kusahau Katiba mpya yenye mengi kuwahusu wananchi.

Kulazimisha uchaguzi bila Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya, liko Giza mbele ambalo tunapambana kuliondoa sasa.
 
Ushauri wa kijinga kabisa.
Maoni Yako yanaheshimiwa.

Ungeeleza pia BUSARA zako zilipo katika kuondoa mkwamo, kuwa njia panda Kwa CHADEMA kuelekea 2025 utatuliweje ingefaa zaidi🙏
 
Ila naona km kitabu kimepotezewa hivi sioni zile kelele za mwanzo
 
Ila naona km kitabu kimepotezewa hivi sioni zile kelele za mwanzo
Ni sababu ya homa ya Uchaguzi.

Nikwambie ndugu, Bila BUSARA kutumika, kulazimisha uchaguzi kufanyika Kwa Katiba hii, mbeleni Si kuzuri hata kidogo.

Bado naamini kuanzia Sasa Hadi June 2025 tutakuwa tumefanukiwa ktk mengi kuondoa sintofahamu ya kesho ya Taifa letu.
 
Kwahiyo ni heri tuandike kitabu kipya kwanza ,tusiwe na haraka ya Uchaguzi
 
Kwahiyo ni heri tuandike kitabu kipya kwanza ,tusiwe na haraka ya Uchaguzi
Ni Kweli kabisa,

Ikiwa aliyepo atashindwa kulikamilisha Hilo Kwa miaka yake minne na ushehe, ni Bora asipewe muda, akabidhi Kwa wahusika, tukamilishe Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wowote.

Mzee Warioba ameendelea kusisitiza muda unatosha na ni vyema uchaguzi ukafanyika Kwa Tume huru ya Uchaguzi.

Tukiunganisha nguvu, inawezekana kuepuka Shari kamili mbele yetu.
 
Dr Slaa ni mtu wa misimamo isoyumba.

Hadi Leo, kwake Lowassa ni fisadi, jambo ambalo ukimuuliza Lissu au Mbowe watajiuma meno.
Hana msimamo wala, hilo la Lowassa unamuona kama ana msimamo lakini nyuma ya pazia alishiriki kumleta sema kuna vigezo kadhaa Lowassa alishindwana Slaa akajitoa


Kama unafuatilia siasa vizuri na unamfuatilia Slaa vizuri, hana msimamo kama unavyosema

Mfano mdogo tu ni suala la katiba mpya ambapo alisema halina umuhimu wowote labda kwa wanasiasa wanaotafuta vyeo, kingine ni kuhusu mikutano ya hadhara, na kuhusu kesi za kisiasa za kubambikiza
 
Kwahiyo ni heri tuandike kitabu kipya kwanza ,tusiwe na haraka ya Uchaguzi
Na jambo hili la kupata Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi ikishindikana,

Tutaletewa Dikteta mwingine. Na DEMOKRASIA itapotea for all. Na Ule msemo wa kuhamia Burundi utakuwa dhahiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…