Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watakuwa wanalingana au kazidiwa miaka 7Wewe una umri gani
Usiamini watu kihivyooooMiaka 47, na wewe ulituambia una 23 [emoji28][emoji28][emoji28] ina maana ni mzazi kabisa huyu[emoji28][emoji119]
Mkuu unanitoa machozi.....usimtaje mama yangu pls. Na kqa mdomo wake baada ya kuona nimeanza kaz aliniambia huyu mwanaume hakufai atakusumbua sana. Achana naeNimeshindwa kwa uliyopitia,
Ila sikio la kufa halisikii dawa, Seems wewe ni sikio la kufa, hutasikia utakachoambiwa hapa,
Kutokumsikiliza mamayako akiwa hai minkosa kubwa, then kurudi nyuma akiwa amekufa plus jitihada alizofanya ili kukuondolea hilo janga,
Basi kwa kuomba tubushauri huu, unamkosea mama yako na hustahili hata kupewa ushauri.
Nakadori Kafa kaoza, hivyo ninashauri Kama ifuatavyo.Wapendwa nawasalimu.
Leo Nakadori mimi nimekuja nikiwa mdogo sana... sio yule mliyemzoea siku zote...naomba kwa nia njema tu mnishauri. Ni ndefu ila naomba msome tu kwakuwa ni story ya kweli kabisa ya maisha yangu....
Nina ex wangu niliyeanza mishe za mapenzi nae 2017 kwa jina ni J ...mwanaume niliyempenda sana hadi kuamua kwamba huyu ndiye mwanaume wa maisha yangu...na hivyo nilikubali alipe mahari....! Mama yangu hakupenda niwe nae.... ila kwakuwa alinipenda sana hakuweza kwenda kinyume na nikipendacho (RIP mama yangu mpenzi).
J pia alinipenda kiasi cha kuamua hata kupigana na wanaume wengine waliokuwa wananizonga.
Kweli alinijali mnoooo mnooo na dah nilikuwa najiskia muda wote kuwa nae karibu. Na J hakuwa bahili hata... yani kila nilichotaka alinipatia.... na nilizidi kupendeza na vile najipenda ndo nikazidi...
Basi maisha ya mahusiano yakanoga kweli hadi waliokuwa wanatuona pamoja na ndugu zake wakawa wanashangaa kwamba kweli J kapata kiboko yake...na mimi bila hiyana nilijiachia kweli kweli madeko kama yote...kifupi tu wapo tuliowafurahisha na wapo tulio wakera.
Lakini pia wapo waliokuwa wanashangaa kwamba yani huyu dada kwa umri wake na elimu yake yote na anavyonata ndo ameangukia kwa huyu J? Dah kweli uchawi upo. Walisema hivi kwa vile kwanza J alikuwa mtu mzima kwangu (almost 47 years by then), lakini pia alitoboa maisha kupitia biashara (ni form four leaver ) hivyo alikuwa na elimu ndogo , pia alikuwa hajijali I mean alikuwa mchafu (hakuwa na mwanamke permanent yani alikuwa ni wale pesa mkononi anakula tunda then anasonga kwa mwingine so hakukuwa na wa kumjali). Binafsi kwa kuwa nilimpenda nilimbadilisha...akawa msafi hasa, akatulia... na kweli watu walishangaa.
Ilipofika 2019 mwishoni mambo yalibadilika... J akaanza kugomba gomba nikimuuliza baadha ya vitu...akawa tena hataki tufwatane (tulikuwa tunaongozana anapoenda kwa ishu za bizness zake na huko huko tunainjoy sana), alikuwa ananipatia password ya simu yake lakini ikafika mahali anabadili... ugomvi kila siku yakawa ndo maisha yetu.
Siku moja aliaga anenda kwa ndugu yake (thou haikuwa hivyo...mara nyingi alikuwa anatumia hii nafasi kwenda kufanya yake) akiwa huko hakutaka mawasiliano .... text hakuwa anajibu... sasa aliporudi nikawa nina hasira kiasi nikamuuliza we J ulikuwa wapi hata simu hupokei? Akajibu '" kwani wewe hutaki niende kwa ndugu zangu .... usinipangie...". Basi nikiwa na hasira tukaingia ndani huku nikilalamika kwamba nampenda sana tena ni mkubwa sana kwangu, nampikia vizuri namfulia amependeza na nimembadilisha sana lakini ananifanyia hivyo... basi akanikwida (kweli nilipokwidwa koo nikawa nimemshika kwa nguvu shingoni karibu na sikio...ghafla akaishiwa nguvu akadondoka chini akawa kama haongei na hana nguvu. Me nkaita rafiki zetu walikuwa na boda nikamkalisha katikati me nkakaa nyuma ili kumpatia ballace then tukamuwahisha hospital. Njia nzima me naongea peke yangu tu maana nlijua napata kesi ya kuua kama ya lulu...Tukiwa njian akapata fahamu..... tulipofika hospitali akaambiwa presha ilipanda. Tulipatiwa matibabu then tukarudi home... nikawa naomba msamaha kwamba me sikujua kilichotokea na sikuwa na nia ya kumuumiza. Tukasameheana lakini maisha hayakuwa na amani. Kuna kipindi J aliniambia G naomba usinipende please... akiwa na maana mapenzi yangu kwake yalizidi sana hadi yakawa kero kwake 😭. Niliumia mnoo ila kumuacha J ilikuwa mtihani. Sikuweza.
Kero zikawa nyingi... akawa anatembea na wadada live live... na wao wakawa wananikomoa wanajiachia wanamkumbatia mbele yangu bila aibu maana kipindi najibebisha nao waliumia sana hadi wakawa wanamuuliza ina maana hukutuona sisi hadi ukaenda hukooo (wakataja mji) kumchukua huyu... we haya tu. Kwahiyo iliwafurahisha sana me kupitia niliyokuwa napitia.
J alikuwa ananitamkia kabisa kwamba me kwake nimefika sina pa kwenda... nikawa naumiaaaa hadi nikapata tatizo la moyo.
Maisha yalienda niliyopitia ikawa siri yangu.....hata mama yangu hakujua ninachopitia lakini ndugu zangu walikataa kabisa kumkubali huyu J.
Kuna kipindi mapema 2020 J alifiwa na baba yake mzazi mazishi yakawa kijijini kwao huko mngeta morogoro (huku me sikuwahi kufika). Wakat anapewa taarifa za msiba alikuwa safari hivyo akanitaarifu. Nikawa najiandaa kwenda kumzika ba mkwe ila J akawa kama anakwepa me kwenda. Akaniambia we tulia tu huna haja ya kwenda ...biashara zako zitayumba.
Nikawazaaa moyoni nikasema me siwezi kutokwenda. Yani ba mkwe amefariki kila mtu anajua halafu me nisiende ....hapana. Basi nikaenda salon nikajiandaa kwenye saa 9 hivi nkaenda stend kutafuta usafiri wa kuunga unga. Nikaambiwa niende njia panda ya himo. Kweli nikabahatisha coster ya dar kupitia chalinze...safari ikaanza saa 12 jioni by saa 7 usiku nikashuka chalinze. Nikapanda IT hadi moro Town asubuhi nikaanza safari ya kwenda mugheta. Usiku wake Wakati niko mombo nilimjulisha J kwamba niko njiani lakini wakati nipo moro nilipopiga simu wala hakupokea na mwisho ilizimwa kabisa.
Kwenye mazungumzo ya nyuma J alishawah nitajia kijiji alichokuwa anaishi mama yake... hivyo haikuwa kazi kufika hapo kijijini. Nilipofika nikauliza msiba wa baba mmoja hivi nikamtaja jina...
Wakawa wanasema misiba hapo kijijini ilikuwa kama 4 hivi na jina nililotaja hawalijui. Wakasema labda nipitie hyo misiba huenda nikawapata. Nikachukua boda Sasa kazi ikawa ya kupita kwenye makaburi kuangalia jina la marehemu kwenye msalaba..... na nyumba za wafiwa ....wapi hatukuona jina wala hatukuipata hiyo familia ya akina J.
Basi nikiwa nimekata tamaa sana nikiwaza nirudi tu mjini then kesho yake niondoke kabisa moro... nikakumbuka kwamba J alishaniambia shule ambayo mwanae wa kike K alikuwa anasoma lakini alikuwa amemaliza shule mwaka uliopita...nikajipa moyo kwamba kutakuwa na rafiki zake ambao hata walikuwa wanaishi jirani watakuwa wanamjua. Basi shule haikuwa karibu sana lakini nikaelewana na boda akanipelaka....
Tulifika shuleni lakini ilikuwa kipindi cha likizo hivyo ni form two na four waliokuwepo hapo shuleni. Nilikuta pia waalimu wamekaa nje kwwnye dawati wako busy na laptop na makaratasi.
Ni kama vile walikuwa wanajaza taarifa flan kwenye pc. Baada ya Salam Nilimkamata mwalimu mmoja hivi ambaye alionekana social na kijana nikamuuliza kuhusu yule binti wa J na kwamba alimaliza hapo mwaka jana. Nkamwambia nimekuja msibani ila namba ya babake ambaye ni mume wangu haipatikani. Hivyo naomba nipate japo rafiki wa K ili nifike msibani. Kuna madame pembeni akasikia akaropoka kwamba je kama nataka kumfanyia baya huyo dogo... wao hawawezi nisaidia. Nikamuomba yule ticha wa kiume kwamba alinganishe namba ninayopiga na ya kwenye mafaili. Na kweli kuchek kwenye kumbukumbu namba ya J ndo Iliandikwa kwenye faili la K. Yule ticha wa kiume akasema nakusaidia kama kuna baya basi utajua mwenyewe.
Wanafunzi kama 4 wakaitwa wakaulizwa kuhusu K na wakaulizwa anayepajua kwao.... akapatikana mmoja akamuelekeza mwalimu. Mwalimu akanambia niweke mafuta anipeleke kwa pikipiki yake. Nikampa af 10 haoo akanipeleka. Tulipofika nikakuta kweli kuna msiba ila nikasimama kwa mbali nikaita kijana mmoja nikamuuliza hapa ndo kwenye msiba wa Mzee flani ambaye mtoto wake ni baba flani anaishi mahali flani...yule kijana akajibu ndio ni hapa. Nikajikuta nimemwambia naomba niitie J na mke wake sisi ni marafiki zake tumekuja kumuona....(nilisema mke wake makusudi kwakuwa tayar nlishapata mashaka kwamba kuna nini hadi azime simu muda wote ule wakat me niko barabarani? Na kwann hakutaka nije msibani) yule kaka akaenda.
Kumbuka muda wote huo J Amezima simu yake...
Basi J akawa ameitwa akaja na mdada flani ambaye me namjua ni binam yake...nkajiuliza hivi J ndo kumbe amemuoa na huyu?.... alistuka sana kuniona. Me nikamuuliza kumbe na huku umeoa ndo maana hukutaka nije eeh
Wakanibeba pembeni na wakati wote huo yule ticha anaangalia tu movie. Nikamwambia aniambie ukweli la sivyo naenda kukinukisha msibani kwa alivyonitesa usiku kucha au nimuaibishe...maana angekuwa hana mke kule yule kijana angenambia kwamba mkewe hayupo (yule kijana nlikuja kujua kwamba alikuwa mdogo wake J kwa mama mwingine na walijuana baada ya msiba wa baba yao).
Basi J akaniambia ni kweli nina mke mwingine tena wa ndoa.... anaishi arusha (ndani ndani huko kwenye mto maarufu) Ni mwalimu. Ila me nlishamuacha kwakuwa hazai (na kweli kipindi cha mapenzi yetu sikuwah kusikia hata simu ya mke akilalamika au kusalimia. Akaomba msamaha. Akadai hakuniambia kwakuwa angeniambia basi ningemkataa na nisingemkubali. Me nikamwambia ukitaka nikusamehe umuite huyo mwanamke wako mbele yangu nijue kama mlishaachana na pia uka file talaka. J akakubali. Yule ticha alikuja akatuaga na akatusihi tumaliZe kwa amani. Akanambia yani dada kumbe ulikuwa unakuja kufumania halaf hujanambia...je mngeuana na huyo mke mwenzako ningejisikiaje...nkamuomba msahama nkamtoa wekundu wawili akanipatia namba akasepa.
Me hapo hata msibani sijafika (thou walishazika jana yake) Tuko busy na kesi na watu hawajui kwamba j ana msala. Basi bwana J akaniambia twende nje kidogo ya eneo la pale kwao akaja na yule binam yake pamoja na mama /mdada hivi mweupe wa mpauko (yani ule weupe usiovutia). Nikatambulishwa kwamba yule ndo mke wa J basi yule mama akasema yeye ashaachana na J na hivyo anatutakia kila la heri. Me nkajisikia amani kuchaguliwa mbele ya mke mwenza....halaf me mdogo na napendeza wakat yy amepauka.... alichonizidi labda urefu tu. Kifupi nikajiona me ndo mimi maana bwana ashatubu mbele ya mkewe kwamba hapa ndo kigoma. ila sasa nikawa nshapata tena ganzi la kudanganywa na kutokuambiwa ukweli tangu mwanzo...
Yakaisha nikaenda msibani nikamuona ma mkwe nkampatia Pole (wekundu kadhaa) nikakaa kaa pale hadi usiku.
Ile siku J hakutaka nilale msibani badala yake alinipeleka center kulikuwa na Lodge akasema kwao kugumu sana sitaweza kulala hivyo nilale pale halafu kesho yake atakuja kuniandaa niende stend niondoke (imagine ratiba napangiwa wakati me ni mke maana mahari nilishalipiwa...)me sikubisha kesho yake nilianza safari. Njiani niliwaza sana kumuacha J sababu ya kutokuniambia kama aliwahi oa maana nilishamuuliza kama ana mke akakataa....Ila nikajiona kabisa siwezi kumuacha ntaumia sana. J alipomaliza msiba alirudi na maisha yakaendelea lakini bado mambo yalikuwa magumu hakuna maelewano.
Ilifika mahali hata akawa halali nyumbani anarudi tu asubuhi anabadili nguo then anaondoka. Nikilalamika ananiambia kwamba me sina uvumilivu...nitulie hapo maana nakula nashiba hakuna kitu ninakosa. Nikaanza kuchakaa kwa mawazo...mvuto wote ukapotea. Nilishasahau kama nimesoma hata kazi wala sikuwaza kuitafuta... na biashara nilishashindwa sababu ya stress nikala mtaji wote na haukuwa mdogo (na huu mtaji wa biashara alinipatia mama yangu). ...mtaani nikawa gumzo kwamba J ameniweza.
Mama yangu aligundua kwamba sina amani...ikabidi tu nimueleze. Mama akaniambia kwamba me bado mdogo niachane na huyo mzee ni focus kwenye maisha yangu maana maradh mengi. Mama alikuwa anaongea lakini me nlikuwa nalia tu ma nilijua J aiwezi muacha.
Mama alisimama na mimi muda wote akinitia moyo na kuna kipindi akaja kunisalimia so akaaga anaenda msalimia rafiki yake anayeishi mkoa flani akaniomba vyeti vyangu akapeleka kwa mtoto wa huyo rafiki yake ili wanisaidie ajira (nadhan alifanya hivi ili nibadili mazingira niweze kuwa mbali na J). Hatimaye nikapata ajira baada ya miezi 5 tangu mama apeleke vyeti. Nilimuaga J kwamba kuna kaz ya uchaguzi nimepata mkoa flani hivyo sitakuwepo kwa muda wa miezi 3 kumbe me ndo nshapata kazi hvyoo .
Kwakuwa nilikuwa mbali na J Mdogo mdogo niliweza msahau J japo haikuwa rahisi....akawa anajiongelesha mwenyewe eti anani miss sana na amekumbuka vitu flan flan (alivitaja) me nikamwambia we kukurudia labda nife nifufuke. Bas nikawa tu napewa story zake za mahangaiko... japo wale waleta story walijua bado tuko pamoja ni kazi tu zimetuweka mbali. Yapo mengi magumu nilipitia nimefanya kuyaruka ili kulinda privacy ya baadh ya watu.... lakini pia hata ya kwangu.
Sasa mwaka huu nilienda mkoa anaoish J kwa ishu zangu tu.... nikakutana na marafiki zetu na rafiki zangu pia.... wakawa wanasifia nimependeza na J akiniona lazima atubu....me nkawaambia wala sina muda nae. Kweli kwa siku nliokuwepo pale tukawa nimekutana na J (hyo siku nlivaa gauni fupi sana alaf nkawa natembea kwa kunata hasaaaa kifupi nilirudi kuwa yule G wa kipindi tunaanza mahusiano au zaidi) akaanza kuomba msahama na akatia huruma sana. Eti nikumbuke yale tuliyofanya pamoja ikiwemo sweet moments...lakini pia anadai eti mimi ndo namuwezea (sijui ni fix au) na kwamba yeye ni mwanadamu anakosea....na bla bla kibao.
Bado akaendelea kuomba msamaha ila me dah kila nikiwaza moyo umegoma...
Kweli kuna muda nakuwa mpweke namkumbuka lakini ghafla nayakumbuka aliyonifanyia na hapo hapo najiskia vibaya...
Naombeni mnishauri....
Hivi huyu kweli ni mtu wa kurudiana naye? Au mimi ndo nina over react?
Katika umri wake bado tu anafanya mambo ya ajabu badala ya kutulia.
Au ni kweli ametulia?
Unamuwezea kwa kipi?kama kweli una muwezea kwa nini alikusaliti tena ukiwa nae kingine huyo Mwanaume ana tabia tatu kwanza Mhuni,ana dharau pia si Mkweli kwako uchaguzi ni wako je utaweza kuvumilia kama utaamua kurudiana nae ni kwambie ukweli best huyo hawezi kamwe kubadilika.lakini pia anadai eti mimi ndo namuwezea (sijui ni fix au) na kwamba yeye ni mwanadamu anakosea....na bla bla kibao.
Hahah huu moyo huu acha kabisaNisaidie anitoke kabisaaa
Kweli sihitaji kurudi kule
Nimepitia mengi
Haha me by then nlijua kwakuwa mtu mzima angetulia na mwanzoni alitilia kweli.Nakadori Kafa kaoza, hivyo ninashauri Kama ifuatavyo.
1.Ni yapi malengo yenu wewe na mstaafu mtarajiwa?Kama ni kula "Gudi taimu " uko mahali sahihi Kama ni ndoa refer case ya Mengi na Jackie.
Vinginevyo sikiliza moyo wako. Hili suala liwafikie wanaume under 40 amekosekana rijali anayejali mpaka uende kwa 53? JF hii ni fursa Ahsanteni
Asante sana kwa ushauri wakoKwanza muombe sana mungu,zidisha kutoa sadaka na ufunge kwa imani...amini mungu yupo na anakupenda sana...
Hilo ni jambazi halikufai,hizo ndio tabia zake halisi hawez badirika..kumpa nafasi tena ni kukaribisha uadui kati yenu na mwisho wake utakua mbaya..
Kuendelea kumsogeza ni Eiza umuue au akuue..
Achana na jambazi hilo.
Thread ifungwe mkuu Nakadori huu ushauri ulaminate kabisa usije ukapigwa na kitu kizito baadae 😁. Nakadori, sijui umri wako, but take it from me, kuna raha ya kwenda mbele na kuanza mambo mapya, kuacha utoto, na kujenga familia......
Msahau, and trust me, I may be his age, kuna kitu kinaitwa mutual understanding, watu wazima kwa mtoto hufuata huo mwili wako tu......
Watu wa umri wetu tunapenda sana kukutana na watu similar kwa majadiliano ya ki umri na ki mtazamo, utatumika kama chombo cha starehe.
Achana NAYE
Samahani wewe ni kaka au ni dada?Nimevumilia kusoma yote, nasikitika sana maana wewe unaweza kuwa Dada yangu.
Unawezaje kutupa future prospect ya kuwa na familia yako ya Furaha na kurudiana na mtu kama huyu?
Hemu be respectful to your Mother and allow her to enjoy huko aliko kwa kutorejea kwenye hicho kifungo cha mateso.
1. Hajakutafuta, wewe umeenda mkoa alipo yeye?
2. Umefuata nini kwa rafiki zake? Una shida wewe.
3. Marafiki zake wakakwambia akikuona atatubu.....
Ni shida sana ukijiona wewe ni mrembo sana na ukapewa bichwa, utaharibu future kizembe...
Hujanijibu kwenye malengo 😀😀huyu J anatumia tunguli au?Haha me by then nlijua kwakuwa mtu mzima angetulia na mwanzoni alitilia kweli.
Ila alipofungulia koki wee nkachoka.
Ukweli nilimpenda na ndo maana niliruhusu mahari na tukaishi pamoja na tangu tuachane seriously sio mda mrefu sana