Ushauri gani ambao ulishawahi kupewa na Mzazi wako kuhusu mahusiano?

Ushauri gani ambao ulishawahi kupewa na Mzazi wako kuhusu mahusiano?

heartbeats

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2014
Posts
6,736
Reaction score
10,669
Wakuu,

Binafsi mimi wazazi wangu wote walishanipa ushauri japo ilikuwa kiutani Ila meseji ili delivery

Kwa wakati tofauti, Father alishawahi nishauri mambo machache kuhusu mahusiano/wanawake

1. Katika kabila letu LA kaskazini kule kuna watu wa mahala fulani kaniambia nisioe huko hata kwa kushikiwa bunduki

2. Aliniambia mwanamke asiweze kukariri ratiba zangu hasa za kurudi na kutoka muda anaofikiria hautoki we unatoka muda anaofikiria unatoka wewe utoki. Kama nitachelewa sana nimtarifu mapema.

3. Kama nitakuwa mlevi basi nisimkere Ila nitumie pombe zangu kumchekesha na kumbebisha

5. Nisikubali kupelekeshwa na mwanamke pia nisiwe sirias wakati wote

Kwa wakati tofauti mama alinipa ushauri kadha
1. Msichana wangu awe mzuri kuanzia sura na roho yaani awee na hofu ya Mungu

2. Alinikataza kumpelekea single mama

3. Alishawahi niuliza kwanini niliachana na Ex wangu na alikuwa anavigezo alivyovitaka

4. Alinishawishi nijiweke smart hata tukienda kanisani atatumia muda mwingi kuniweka smart kuliko yeye

5. Mama atanambia kwa fulani sio kwa kuoa wanatabia hizi na hizi

Funguka nawe...
 
Aliniambia.....
Akili ni mali lakini tena akaniambia Akili nyingi huondoa maarifa.....😜
Hakika ukisomea sana kitu ukakielewa saaana mwishowe unahisi sio vile tofauti na ivo , ndo maana unakuta wasomi wazima wanafanya things za kiwaki,kama kupindisha sheria,kusain mikataba utopolo n.k
 
Bi mkubwa: hajawai nipa ushauri wowote wa maana zaid ya kunisema tu.

Mzee: aliniambia achana nao tafta maisha kwanza kama ni wako atakutafta tu siku moja atakuja(hapo baada ya kupata mtoto ) huu niliona ni ushauri wa kipumbavu sana maana ata ayo maisha aliyosema nitafte bado sijayaona.
 
Bi mkubwa baada ya kusikia tetesi kua natembea na shosti yake alinikanya sana kua sio vizuri kutembea na watu wazima, ni bora nitafute binti wa rika langu,
ila mimi sasa na hao mabinti wa rika langu ni kama Urusi na Ukraine.
 
Back
Top Bottom