Ushauri gani ambao ulishawahi kupewa na Mzazi wako kuhusu mahusiano?

Bi mkubwa baada ya kusikia tetesi kua natembea na shosti yake alinikanya sana kua sio vizuri kutembea na watu wazima, ni bora nitafute binti wa rika langu,
ila mimi sasa na hao mabinti wa rika langu ni kama Urusi na Ukraine.
Ushaoa au bado?!![emoji1][emoji2]yule hausigel alikuharibu sana

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Bi mkubwa baada ya kusikia tetesi kua natembea na shosti yake alinikanya sana kua sio vizuri kutembea na watu wazima, ni bora nitafute binti wa rika langu,
ila mimi sasa na hao mabinti wa rika langu ni kama Urusi na Ukraine.
Naelewa mkuu wanazingua sana awa mabinti, wakubwa ndio fresh.
 
Bi harusi Mkubwa aliwahi niambia usije ukasumbuka na mwanamke unaempenda afu unaona kabisa anazingua, bora uoe yule anaekupenda kwa dhati kuliko unaempenda wewe. Huyu anaekupenda unaweza kujifunza kumpenda.
ushaur mrua sana huu
 
Mama huyo.."mwanangu hivi unajua upendo ni uvumilivu"...nikageuka nikamuangalia nikaishia kucheka ..aliongea Hilo baada ya kumuuliza kitu kuhusu Baba.. 😂😂ila ile siku aliongea kwa kumaanisha khaaa!!
 
Baba aliwahi niambia;
Kama nina mahusiano na msichana ambaye ameenda kusoma chuo cha mbali basi niamini nimeshapoteza.
Anaamini kuwa msichana atakuwa na wewe kwa sababu unampa comfort na kufufill mahitaji yake kwa wakati na sehemu husika...anapoenda sehemu nyingine , kuna watu watafanya hivyo! Atakusahau, ladies are too easy to forget.
 
Mama yangu Ni daktari, huwaga ananishauri nitumie Kinga wakati nashiriki ngono na wanawake ili nisije nikaukwaa kimasihara

Pia ananipaga CDs kila baada ya muda fulani

Abarikiwe Sana mamangu.
 
Baba alinionya nisiwe na mazoea ya kumtembelea mke wangu kazini kwani naweza kumkuta kapakatwa ama kushikwa shikwa hovyo na wanaume wengine kwani wenzetu wanapenda kutaniwa wakati wote na kutongozwa pia. Pia nisije kuwa na mahusiano na wanawake wa Kichagga, Kipare, wa Tanga, Wagogo, Wanyaturu, Wanyiramba na Waha pamoja na Wafipa. Akaongezea kwa kusema, ukija kuoa usiombe mchango wa mtu yeyote, jiandae wewe mwenyewe na sisi wazazi tutakuongezea kama ukipungukiwa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…