Ushauri gani ambao ulishawahi kupewa na Mzazi wako kuhusu mahusiano?

Nimekatazwq kuoa mchaga na mpare hii iko Kwa mama na mama namshukuru Mungu nimeweza kudate na wanawake wawili wakichaga aisee wote nimekutana na Tabia wazazi walizoniambia japo nilikuwa mbishi Kwanza wabinafsi wanapenda Sana Hela hawako hata romantic kiuhalisia Mimi sio mtu wakuzingatia makabila Ila naona kama itabidi nirudi home sweet home Iringa,mbeya,njombe huko ndo kuna wanawake wa kuoa
 
Ushauri wa mzee wako wakipumbavu nimecheka balaa[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Mama alikuwa anatuambia mme wako wa kwanza ni kazi yako. Ukiwa na hela zako huangaishwi na mwanamme
 
Ushauri wa mzee wako wakipumbavu nimecheka balaa[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Ndio. Sasa huo ni ushauri gani unampa mtoto wako? Kama sio kumtengenezea roho ya utelekezaji?
Hio kitu niliikataa kabsa bora nionekane sipo full responsible kuliko kuonekana nimemtelekeza, mtoto anafurahi ata kuona anaita baba ata kama umsaidii sana ila kile kidogo kinampa fajara kuwa na mm nina baba ananipenda na kunipigania.
 
mama yangu huwa ananiambia hivi usijekutegemea kupata mwanaume aliyekamilika hapa dunian kama ni mume wako jali haya awe anakuhudumia chakula,mavazi vizuri,na ukiumwa akutibie bas usije mwacha mume wako kisa mlevi mchepukaji na mengne bali ww kama mwanamke angalia unanafasi gani kwa mungu wako mweleze mungu matatizo ya mume wako jinsi unavyotaka awe na kwa imani ya kweli mungu anaweza mbadilisha mme wako
 
Msalimie Sana Mama mwambie anywe soda ntalipa tukioana

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Ushaur wa mama mkwe wangu ni mzur sana
 
Ungejitahidi ukatafuta hela zako za kula na kujitibia ungepata heshima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…