USHAURI: Halima Mdee na wenzake wafukuzwe CHADEMA

USHAURI: Halima Mdee na wenzake wafukuzwe CHADEMA

Nimeona Halima Mdee na kundi lake wakila kiapo kwa spika wa bunge kama wabunge wa viti maalumu CHADEMA, kama kweli wamerubuniwa na CCM na hatimaye kula kiapo bila kuwa na lidhaa ya chama wafukuzwe unachama Mara mmoja.

Hii itasaidia kujenga nidhamu ndani ya chama. Ni bora kujenga chama upya kuliko kuwa na watu wasio na nidhamu ndani ya chama. Ifahamike kuwa chama hiki ni mali ya wanachama na si watu wachache. Kuna watu tumepoteza kazi serikalini kwa sababu ya kukipigania chama.

Narudia kama wamekengeuka na kula kiapo bila ridha ya chama ,basi wafukuzwe wote Mara moja bila kujali jina la MTU.
Wakifukuzwa uniiteeeeee.
Achana na tumbo wewe.
 
Habari wakuu,
Kutokana na Duru za siasa zinavyoendelea nchini Tanzania, Hasa kwa upande wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Huenda Wabunge wa Viti Maalum kutoka Chadema Ambao Wameenda Bungeni Dodoma leo kwa ajili ya kuapishwa kuwa Wabunge wa Viti maalum, WAKAFUKUZWA ndani ya chama.

Hili Ni nalisema kwamba huenda isifike 2024 Viongozi wakuu wa Chama wakafanya maamuzi magumu. Na Hili linaweza Kuwapa credentials CHADEMA lkn kusiwe na faida ktk suala la ruzuku. Yaan itapungua kuliko wangekuwepo hawa kina Mdee na Wenzake.
Anawafukuza nani wakati wana baraka za mbowe?
 
Yaani niache posho ya gari zuri,malazi na mafao 100% uhakika huku wengine wanalilia mafao, si ni upumbavu.Hongera sana Kamanda Mdee.
 
Kuna uwezekano hata wakifukuzwa uanachama ndugai akawalinda waendelee kihudhuria bungeni, ref yule mbunge alievuliwa ubunge lakini ndugai alimkingia kifua na aliendelea kuhudhuria bunge
Hawa ni wabunge wa Ndugai siyo wa chade
Bora ndugai awalinde hizo ni nafasi za wanawake kwanini wanaume watumie mfumo dume kuwanyanyasa wanawake
Kwanini wasipewe wanna CCM wenzako?
 
Hata Halima Mdee!! Loh, kweli usimwamini mtu kwa 100%.

CHADEMA lazima isimamie inachoKiamini. Bila ya kujali kama CCM itaendelea kuvunja katiba na kuamua kuendelea kuwaweka Bungeni wanachama hawa waliokisaliti chama au vinginenvyo, ni lazima hatua madhubuti zichukuliwe. Wasaliti hawa wote wafukuzwe uanachama mara moja. Wakaongeze nguvu ya UWT.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kitu itakuwa na baraka ya chama,Mnyika anawachota akili tu kuwazuga.

Jinsi Mdee alivyo mtiifu kwa Mbowe, huo ubavu wa kuenda kinyume na mkondo wa maji hana.

Yawezekana Mbeligiji ndo kaingizwa mkenge hapa.
 
Back
Top Bottom