Ushauri: Je, ajenge nyumba au aweke pesa fixed deposit CRDB kwa riba ya 7%?

Ushauri: Je, ajenge nyumba au aweke pesa fixed deposit CRDB kwa riba ya 7%?

Watu hawana huruma na wastaafu uwapa michongo ya pesa wanaishia kufa kwa pressure.
Ukistaafu idea nyingi sana unaletewa na ndugu.
Pana mstaafu alipata milion 250.
Shemeji yake akamwambia tufate pikipiki china ukileta kwa jumla pesa ipo,akampa pesa shemeji yake akalala nazo Kona China hadi wa Leo hata Kama alirudi nchini kimya kimya Siri yake.
Pana mstaafu aliambiwa trekta zinalipa akapigiwa hesabu na motivator akaingia dukani akachukua trekta mbili mpya kwa milion 90 Leo zipo juu ya mawe zinaliwa na kitu, amekosa pesa za kununua spea, mwingine aliambiwa daladala zinalipa akazinunua akaishia kushinda stand anahesabu tripu Kila ikipita.
Ukistaafu achana na biashara,nunua bond,au weka fixed nje ya nchi mfano Canada, USA au zile stable country ule gawio Kila baada ya mda umeshindwa sana Jenga chumba sebule chumba sebule gombana na wapangaji maisha yasonge.
Kisha tafuta shamba mikoani acha familia mjini weka kasikilize sauti za ndege tu porini unalima kilimo kisicho Cha biashara ili kufanya mazoezi tu utafika miaka 100,pia kaa mbali kabisa na Hawa mitume na manabii watakufilisi.
Pana mama yupo kitandani mwaka Sasa anaumwa aliambiwa biashara Fulani inalipa alikuwa na nyumba zake 4 alijinyima akiwa kazini kujenga,akaingia bank akazikopea milion 200 baada ya mda biashara ikawa hasara bank wanataka Hela zao.
Bora upoteze pesa ujanani una nguvu kuliko kupoteza uzee zikienda zimeenda.
 
Mama yangu kastaafu utumishi.kapewa.mafao milioni 100.anataka ushauri ajenge.nyumba yakupangisha au aweke fixed deposit bank ambayo kwa urahisi itampa kama laki saba kila mwezi.

Ushauri please

Binafsi, Nakushauri awekeze UTT especilly Bond Fund au Liquid fund, kwa 100 ambayo anayo atakuwa anapata walau 1,000,000 kila mwezi (Ambayo anauwezo wa kuitoa ndani ya siku kumi tu tofauti na fixed deposit za bank ukitoa unakuwa umevunja mkataba while UTT unaweza kuitoa hela yote wakati wowote ndani ya siku kumu.....actualy ni siku mbili hivi ..mimi huwa napata fedha yangu ndani ya siku mbili tokea nifanye repurchase),Pili Bank ile riba unapata wanakata witholding tax ya 10% wakati UTT au Bond ya BOT hawakati kodi ya Zuio.

Baada ya kuwekeza UTT-Bond fund, kama yupo interested na vibiashara vidogovidogo ama kujenga nyumba anaweza kwenda bank akakopa akaweka vipande vyake vya UTT kama bond/Collateral na zile coupon /faida anazopata zikatumika kulipa mkopo wake, say,rejesho la kila mwezi 700,000 anakuwa anabakiwa na 300,000. Hii 300,000 akichanganya ka pension zake za kila mwezi ataishi vizuri tu, Mungu akimjalia vibiashara navyo vikafanya vema atapata faida.

Kwa mpangilio huo niliokushauri,pesa yake yote itabakia 100M, muda wote bila kupungua na life likaenda vema.

For more Advise ,kwenye eneo la Personal finance PM with consultation fees
 
Inategemea yupo maeneo gani, lakini kama yupo maeneo ya mjini kitumia 80M anapata nyumba mbili standard kabisa ambazo kodi yake kwa mwaka haipungui 4M

Na hii sio biashara bali ni uwekezaji maana wastaafu wengi biashara huwa zinawashinda.
 
Kwa umri wake, kujenga nyumba kwa 80M kisha upate 4M kwa mwezi si uamuzi wa busara, aweke UTT, apate 1M kila mwezi
 
Umenikumbusha jamaa mmoja mjeda alistaafu bado ana nguvu watoto ndio wanaanza sekondari si akanunua fuso mbili. Napoongea hapa hata nyumba ya kuishi kashindwa kumaliza madirisha kaweka maboksi madirishani. Fuso zote aliuza kwa hasara

Sasa hivi watoto wanasoma kwa shida sana na mmoja alimaliza anaendesha bodaboda
Wazee wetu Huwa wanachemka sana,
Umri huo,kama Sina akili ya kufanya chochote,Bora pesa yote niipige pasu,niwape watoto,vijana wa siku Hz,akili zinachaji,
 
Mama yangu kastaafu utumishi.kapewa.mafao milioni 100.anataka ushauri ajenge.nyumba yakupangisha au aweke fixed deposit bank ambayo kwa urahisi itampa kama laki saba kila mwezi.

Ushauri please
Aache ujinga. Aende UTT (*150*82#) apate riba ya zaidi ya 10%, aweke bond fund au liquid fund, au aziweke faida fund (*152*00#). Akiweka hiyo fixed deposit atakuwa jinga maana wenzake watapeleka huko UTT watapata 10% wanamgawia 7% na kibaya kabisa wao watapata interest ambayo ni compounded.
 
Ukisha staafu hata ujitunze viipi mwusho wa siku mali ni kwa ajili ya utakao waacha duniani. Hao wanaomwambia atunze hela ale kidogo kidogo wanamdanganya. Hela haitunziki ili iliwe kidogokidogo. Baada ya miezi 6 tu tutarudi hapa kwenye account zikiwa zimebaki chavhe sana.

Ndugu, wanao, marafiki na matatizo wakijua umetunza hela kila siku wanagonga hodi mlangoni kwako kukushawishi hili na lile na ni ngumu kuwakatalia wote. Unaweza kuwakatalia ndugu ukaangukia kwa wanao. Unawakatalia wanao unaangukia kwenye matatizo

Wote walio jaribu kuweka nenda kavute statement yao uone kama walikaa na hizo hela kwa miaka 2 na zaidi.

Niko hapa
Mtu mwenye mafao ya 100m anapata pension kila mwezi kama 1.5m. Pesa hii inamtosha kwa matumizi yake ya mwezi.
Akiweka hiyo pesa 100m utt liquid fund kwa miaka 2 atavuta Tshs 24m kama riba.
Ataweza kutumia pesa hiyo 24m kujenga nyumba hiyo ya kupangisha ...na pesa yake 100m ikiwa iko utt intact inaendelea kuvuna riba.
 
Binafsi, Nakushauri awekeze UTT especilly Bond Fund au Liquid fund, kwa 100 ambayo anayo atakuwa anapata walau 1,000,000 kila mwezi (Ambayo anauwezo wa kuitoa ndani ya siku kumi tu tofauti na fixed deposit za bank ukitoa unakuwa umevunja mkataba while UTT unaweza kuitoa hela yote wakati wowote ndani ya siku kumu.....actualy ni siku mbili hivi ..mimi huwa napata fedha yangu ndani ya siku mbili tokea nifanye repurchase),Pili Bank ile riba unapata wanakata witholding tax ya 10% wakati UTT au Bond ya BOT hawakati kodi ya Zuio.

Baada ya kuwekeza UTT-Bond fund, kama yupo interested na vibiashara vidogovidogo ama kujenga nyumba anaweza kwenda bank akakopa akaweka vipande vyake vya UTT kama bond/Collateral na zile coupon /faida anazopata zikatumika kulipa mkopo wake, say,rejesho la kila mwezi 700,000 anakuwa anabakiwa na 300,000. Hii 300,000 akichanganya ka pension zake za kila mwezi ataishi vizuri tu, Mungu akimjalia vibiashara navyo vikafanya vema atapata faida.

Kwa mpangilio huo niliokushauri,pesa yake yote itabakia 100M, muda wote bila kupungua na life likaenda vema.

For more Advise ,kwenye eneo la Personal finance PM with consultation fees
Mkuu natamani ungemwaga hapa madini zaidi kuhusu UTT
 
Mama yangu kastaafu utumishi.kapewa.mafao milioni 100.anataka ushauri ajenge.nyumba yakupangisha au aweke fixed deposit bank ambayo kwa urahisi itampa kama laki saba kila mwezi.

Ushauri please
Mwambie muje muwekeze apa saiti ya tofari inaripa sana
 
Hatifungani za BOT, na hasa za muda mrefu zenye riba nzuri zaidi, upatikanaji wake ni changamoto kwa vile huwa zinashindaniwa sana.

Utt Bond fund kama baadhi walivyoshauri ndipo patampa manufaa kuliko fixed deposit ya benki. Wala hapana ushindani. Ni kufungua akaunti na kuweka mzigo siku yoyote ya kazi.
 
Back
Top Bottom