bongo dili
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 12,350
- 25,180
Watu hawana huruma na wastaafu uwapa michongo ya pesa wanaishia kufa kwa pressure.
Ukistaafu idea nyingi sana unaletewa na ndugu.
Pana mstaafu alipata milion 250.
Shemeji yake akamwambia tufate pikipiki china ukileta kwa jumla pesa ipo,akampa pesa shemeji yake akalala nazo Kona China hadi wa Leo hata Kama alirudi nchini kimya kimya Siri yake.
Pana mstaafu aliambiwa trekta zinalipa akapigiwa hesabu na motivator akaingia dukani akachukua trekta mbili mpya kwa milion 90 Leo zipo juu ya mawe zinaliwa na kitu, amekosa pesa za kununua spea, mwingine aliambiwa daladala zinalipa akazinunua akaishia kushinda stand anahesabu tripu Kila ikipita.
Ukistaafu achana na biashara,nunua bond,au weka fixed nje ya nchi mfano Canada, USA au zile stable country ule gawio Kila baada ya mda umeshindwa sana Jenga chumba sebule chumba sebule gombana na wapangaji maisha yasonge.
Kisha tafuta shamba mikoani acha familia mjini weka kasikilize sauti za ndege tu porini unalima kilimo kisicho Cha biashara ili kufanya mazoezi tu utafika miaka 100,pia kaa mbali kabisa na Hawa mitume na manabii watakufilisi.
Pana mama yupo kitandani mwaka Sasa anaumwa aliambiwa biashara Fulani inalipa alikuwa na nyumba zake 4 alijinyima akiwa kazini kujenga,akaingia bank akazikopea milion 200 baada ya mda biashara ikawa hasara bank wanataka Hela zao.
Bora upoteze pesa ujanani una nguvu kuliko kupoteza uzee zikienda zimeenda.