Ushauri juu ya biashara ya kitimoto

Hiyo biashara sio ya kuuliza, ni wewe tu na pesa zako uanze kupiga hela. Cha msingi ni kuwepo kwenye pilika pilika za watu,ila hapo pa kutokuwepo kwa vinywaji vikali ndipo utakapokosea,maana mdudu mwenzie "ngumu kumeza"

Daaa! Asante mkuu, ngoja nijilipue kujaribu si kushindwa!
 
Habarini wana JF,

Mimi nina wazo hapa kuhusiana na biashara ya Kitimoto. Labda nifafanue vizuri kuhusiana na hii biashara yani ni nanunua nyama ya ngurue kwa wachinzaji halafu ninakuwa na kibanda kwa ajili ya kuipika au roasting kwa ajili ya watumiaji.

Location ya Biashara naifanyia Dar es salaam.

Napenda kuuliza labda mwenye experience na hii biashara yupo tuweze peana mawazo na changamoto mbalimbali zinazohusiana na hiyo biashara.

Asante
 
Hakuna namna, nenda kwa wanaokaanga kitimoto kawaulize maswali ya msingi, wapi wanapata nyama, kilo wananunua sh ngapi, n.k
 
soko ni tatizo kubwa sana dar es salaam, kama unabiahsara kubwa lazima upitie kwa middle men, hao watanunua nguruwe wako kwa 5000 hadi 6500. tatizo lingine nililoliona dar kwa wale wanaosafirisha nguruwe wakiwa hai, ukishamfikisha dar kwa watu wenye mabanda na machinjio wanafanya udanganyifu kwenye mizani yao na wakati wa kuchinjwa wanakatia mabegani ili sehemu kubwa ya nyama ibakie kama sehemu ya kichwa maana ujira wa wachinjaji ni kuwaachia kichwa na miguu. jamani naona kuna tatizo kubwa sana la nguruwe sasa hivi. lakini changamoto hii wadau tuine kama fursa kwa kufiria kufanya packaging au kusindika na kufanya biashara nje ya nchi. kama kuna mtu anajua wapi tunawweza kupata soko la uhakika la nguruwe aniibox ili tufanye biashara ninanguruwe wengi tatizo soko la uhakika
 
Hii nzuri mkuu go ahead cha kuzingatia eneo ukikosa mtu wa kukushauri kuhusu hii biashara njoo nikuelekeze nijuacho
 
MKUU,ULIFANIKIWA?
 
Jamani wadau naomba kwa mtu yeyote hasa wa maeneo ya Mbeya, Iringa na Singida anipe details kuhusu upatikanaji wa Kitimoto, nataka nianze biashara yakununua kitimoto nakuwasafirisha Dar es salaam.
MKUU,ULIFANIKIWA
 
MKUU,ULIFANIKIWA
 
Habari wakuu,

Mimi ni kijana mjasiriamali mwenye jiko la kupika kitimoto Kimara. Ninahitaji kupanua biashara yangu, yaani nifungue jiko lingine maeneo ya kimara mpaka mbezi mwisho. Hivyo ninaomba msaada kama una bar au unamfaham mtu mwenye bar eneo lililochangamka na anahitaji mtu wakufungua jiko. Please niPM

Natanguliza shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Astaghfirullah

sent from my Samsung S9 plus using jamiiforums mobile application.
 

Kwa Uungwana zaidi mwisho wa maelezo yako ungeomba radhi kwa Waislamu waliopo humu ambao hiyo kitu ni ' haram / mwiko ' Kwao ili wasikwazike na huu uzi wako. Huu Mtandao siyo tu wa Wakristo Mkuu hivyo ' busara ' kubwa mno inahitajika pale unapotaka kuwasilisha jambo ambalo lina sura mbili hasa ya Kimtizamo na ya Kiimani.

Nikutakie tu kila la kheri Mkuu katika Biashara yako hiyo ya Ng'ombe Katoliki / Ngurumwe / Kitimoto / Noah / ARV.
 
We kama mtakatifu....usingeifungua hii thread.....sahizi ungekua unahubiri huko mtaan kwenu
Wajina lolo123 na Mimi ni lolowapi. Usijali pamoja mkuu.

sent from my Samsung S9 plus using jamiiforums mobile application.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…